Kati ya Mkapa na Magufuli nani anapaswa kufanyiwa kumbukizi?

Kati ya Mkapa na Magufuli nani anapaswa kufanyiwa kumbukizi?

Kwanza Holidays zilizopo zinapaswa kupunguzwa watu wafanye kazi.

Tukianza kuendekeza utamaduni wa kuwawekea Holidays Maraisi walioaga dunia, je wakifika 100? Ina maana watu watapumzika siku 100?

Achezi hizo.
 
Aisee!!, kwani kumbukizi (Anniversary) ina maana gani??

Ni lazima mtu afe ndipo ifanywe kumbukizi??,--- kumbukizi ni kuangalia mchango wa mtu katika jambo fulani jema alilolifanya ili tujifunze kwayo, ama awe hai au mfu haidhuru, tena akiwa hai ndio vyema kwani mnaweza kumualika naye akashiriki isitoshe hiyo itaonyesha appreciation yetu kwake kwa jambo alilofanya.
Hivyo ndivyo ilipaswa kuwa lakini sivyo ilivyo, ni ngumu sana kwetu binadamu!!
 
Kwa Bahati wengine mpaka sasa kwa sehemu tumebahatika kuona Marais wote baada ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kung'atuka madarakani. Wengine tumepata bahati kufanya uchaguzi kuanzia enzi Mwinyi akiwa Madarakani.

Kati ya Marais walioingia madarakani baada ya Mwalimu Kung'atuka yaani Ally Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa, Jakaya Mrisho Kikwete, John Pombe Magufuli, wawili kati yao wameshatangulia mbele ya haki. Benjamin Mkapa na John Pombe Magufuli.

Mkapa na Magufuli kila mmoja waliingia madarakani nchi ikiwa kwenye hitaji la kufanya mabadiliko ya kijamii na kiuchumi. Mkapa alikuwa ni Rais wa Kwanza kuchaguliwa baada ya mfumo wa vyama vingi kurejeshwa mwaka 1995. Na Mkapa aliingia wakati nchi yetu inatoka kwenye mfumo wa njia kuu za uchumi kumilikiwa na dola kwenda kumilikiwa na sekta binafsi.

Magufuli aliingia madarakani wakati Tanzania ikwa na hitaji kubwa la kufanya mabadiliko ya udhibiti wa matumizi ya madarakani ya umma kwa maslahi binafsi. Magufuli aliingia wakati ilikuwa inaonekana kama vile ukiwa na madaraka unakuwa na nguvu isiyohojika na unaweza kutumia madaraka ya umma kujitajirisha.

Kwa mitazamo mbali mbali inaonekana kama kuna shinikizo la kuweka kumbukuzi kwao kwa siku za vifo vyao iwe ni sikuk rasmi ya kitaifa. Jee wote wawili wawekewe kumbukuzi ama ni mmoja tu kati yao ndiye anayefaa kuwekewa kumbukizi?
Mkapa ndo aliyemwibua Magufuli hivyo mkapa ndo mwamba wa nchi hii kwenye uchumi.
 
Kwa Bahati wengine mpaka sasa kwa sehemu tumebahatika kuona Marais wote baada ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kung'atuka madarakani. Wengine tumepata bahati kufanya uchaguzi kuanzia enzi Mwinyi akiwa Madarakani.

Kati ya Marais walioingia madarakani baada ya Mwalimu Kung'atuka yaani Ally Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa, Jakaya Mrisho Kikwete, John Pombe Magufuli, wawili kati yao wameshatangulia mbele ya haki. Benjamin Mkapa na John Pombe Magufuli.

Mkapa na Magufuli kila mmoja waliingia madarakani nchi ikiwa kwenye hitaji la kufanya mabadiliko ya kijamii na kiuchumi. Mkapa alikuwa ni Rais wa Kwanza kuchaguliwa baada ya mfumo wa vyama vingi kurejeshwa mwaka 1995. Na Mkapa aliingia wakati nchi yetu inatoka kwenye mfumo wa njia kuu za uchumi kumilikiwa na dola kwenda kumilikiwa na sekta binafsi.

Magufuli aliingia madarakani wakati Tanzania ikwa na hitaji kubwa la kufanya mabadiliko ya udhibiti wa matumizi ya madarakani ya umma kwa maslahi binafsi. Magufuli aliingia wakati ilikuwa inaonekana kama vile ukiwa na madaraka unakuwa na nguvu isiyohojika na unaweza kutumia madaraka ya umma kujitajirisha.

Kwa mitazamo mbali mbali inaonekana kama kuna shinikizo la kuweka kumbukuzi kwao kwa siku za vifo vyao iwe ni sikuk rasmi ya kitaifa. Jee wote wawili wawekewe kumbukuzi ama ni mmoja tu kati yao ndiye anayefaa kuwekewa kumwewebukizi?
Unajinasibu kuwa wewe ni mkongwe kiumri na kutaaluma lakini kama unaweza kudiriki kulinganisha Mlima Kilimanjaro na mwinuko wa Sekenke basi wewe huna unachojuwa.

Msipende kuharibu CV/Taswira za watu kwa kuwalinganisha na vitu vya HOVYO. Huyo Magufuli wenu labda mlinganisheni na aki a Makonda, Sabaya, Kangi Lugora, Nkurunzinza au Kagame. Kama humfahamu Benjamin William Mkapa andika thread straight forward tutiririke hapa tukufahamishe
 
Naambiwa mke wa Ben Saa8 na Azory Gwanda na mjomba wa Akwilline wako humu. Waulize watoe maoni.
kuna mtu kaniambia sasa hivi wapo off line wanajiandaa na ibada ya kumuombea Hayati Mwamba apumzike kwa amani
 
Aliye tuvusha kipindi Cha lockdown ndiye anastahili kuwekewa kumbukizi
 
Liwe wazo. Lakini kumbukizi haliwezi kufanywa mtu akiwa hai kwa mantiki kwamba kumbukizi kwa marehemu ni kwa kuwa hawezi kubadili Historia mtu akiwa hai haiwezekani kufanya kumbukizi ya aliyoyatenda kwani bado anayo nafasi ya kubadilika!!

Sio liwe wazo bali ni mazoea yasiyofaa kufanya kumbukizi hadi muhusika awe kafariki.

Kumbukizi ni kwa ajili ya tukio ambalo muhusika hata akiwa hai hawezi kulibadilisha tena.
 
Hapo kuna mmoja alifariki baada ya kuondoka madarakani na kuna mwingine alifariki akiwa madarakani.
 
Watawala wa Kikristo wanakufa mapema kwa sababu wanaibeba dunia, hii Dunia ni nzima, fanya yako ondoka, tofauti na watawala wa kiislamu,
 
Back
Top Bottom