Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Big Meech keshatoka gerezani na sasa hivi yupo kwenye halfway house.Nikiangalia movie kama BMF ya maisha ya Big Meech bila subtitles natoka kapa.
mmmh hii mada wabongo tuachane nayo tukutane kwenye ku bet na mpira, uganda nako kuna kiingerezaKwa hapa Afrika napenda mno kiingereza cha waganda na wazambia.
Zambia sio kizuri kama Zimbabwe.Kwa hapa Afrika napenda mno kiingereza cha waganda na wazambia.
Ila movie za NY hasa hasa za Tupac nazielewaBig Meech keshatoka gerezani na sasa hivi yupo kwenye halfway house.
Ila naona ana lay low kwa sasa.
View attachment 3176209
View attachment 3176210Detroit walifutahi sana. Hasa wasanii wa pande zile. Namaanisha lafudhi yao wanayotumia iko tofauti sana. ATL,South West Detroit na Philadelphia.
Mbona Terry (South West Tee) yeye havumi? Kaka yake?Big Meech keshatoka gerezani na sasa hivi yupo kwenye halfway house.
Ila naona ana lay low kwa sasa.
View attachment 3176209
View attachment 3176210
Deep deep deepHilo ni kweli, lakini si ukweli wote.
Hata weusi kwa weusi [Foundational Black Americans] wana lafudhi tofauti tofauti kulingana na eneo watokalo.
Kwa mfano, weusi [Foundational Black Americans] wa Texas wana lafudhi tofauti kabisa na weusi wa Georgia.
Weusi wa Maryland wana lafudhi tofauti kabisa na weusi wa Mississippi.
Weusi wa Virginia wana lafudhi tofauti kabisa na weusi wa Alabama.
Malcolm X na Martin Luther King walikuwa na lafudhi tofauti.
Malcom X alizaliwa Omaha, Nebraska na akakulia Milwaukee, Wisconsin, Lansing, Michigan, na Boston, Massachusetts.
Martin Luther King Jr., alizaliwa na kukulia Atlanta, Georgia.
Hawa wawili ukizisikiliza hotuba zao utagundua walikuwa na lafudhi tofauti.
Pia, hata wazungu kwa wazungu nao wana lafudhi tofauti.
Wazungu wa Arkansas na Kentucky wana lafudhi tofauti na wazungu wa South na North Dakota.
Wazungu wa Kansas wana lafudhi tofauti na wazungu wa Alaska.
Sababu hasa ya tofauti hizo siijui au sizijui. Ila ninachojua elimu nayo huwa na mchango mkubwa sana.
Mambo mengine ambayo huchangia utofauti huo ni maeneo ya kijiografia na labda exposure na contact na watu wa sehemu zingine.
Kwa mtu ambaye hujaishi na Wamarekani kwa muda mrefu, baadhi ya tofauti hizo za kilafudhi ni ngumu kuzibaini.
Ni kama vile ambavyo wao wakija huku kwetu, itawawia vigumu kuzibaini lafudhi za wazungumzaji wa Kiswahili ambao ni Wasukuma, Wachaga, au Wahehe.
Ila mimi na wewe haitotuwia vigumu kumbaini Ngosha ni yupi na Mangi ni yupi.
Na hata kwa Wasukuma, sisi kwa sisi kupitia lafudhi huwa tunagunduana kirahisi yupi ni Mnyantuzu, yupi ni wa Shinyanga, na yupi ni wa Mwanza.
Ila Mnyakyusa ambaye hajaishi na Wasukuma, kwake atasikia lafudhi tu ya Kisukuma.
Wanaijeria na wajamaika ni funga kazi.😄😄😄Scotland aka Scottish, Australians
Kiingereza ni lugha ya kuungaunga sana.
Lugha gani ambayo watu kutoka maeneo tofauti wanaongea tofauti na unaweza usielewe.
Sasa kuna wahindi, wanijeria, wajamaica nao wamekuja na kiingereza chao basi kazi kwelikweli.
Ngoja nasisi wa mtoni mtongani tuanze kuongea English yetu mixer kimakonde, kimakua, kizaramo, unaweka na kisukuma inakuwa getegete kabisa.
Huwa napata ugumu kidogo nikiwa namsikiliza Mmarekani ila namuelewa kwa urahisi zaidi mwingereza.
Wataalam wa kingereza karibuni.
Kiswahili cha Mkenya na Mtanzania huwa unawahi kukielewa kipi?Au kiingereza cha Mganda na Mnaigeria huwa unakielewa kipi zaidi?Huwa napata ugumu kidogo nikiwa namsikiliza Mmarekani ila namuelewa kwa urahisi zaidi mwingereza.
Wataalam wa kingereza karibuni.
Ukienda Kilimanjaro ndio kichekesho zaidi. Sio tu kuna tofauti kubwa ya lafudhi na lahaja kati ya wilaya za Siha, Hai, Moshi, na Rombo zilizo ndani ya umbali usiozidi km 100, nenda wilaya kama Rombo isiyozidi sq. km 1,450 kutoka kijiji hadi kijiji kuna tofauti kubwa mno ya matamshi kiasi cha wao kwa wai kutoelewana kabisa.Kwanini msijiulize, Zanzibar wanaongea Kiswahili lakini lafudhi na lahaja ni tofauti? Ukizingatia ni sehemu ndogo.
Wakojani
Wanungwi
Watumbatu
Wamakunduchi
Wapemba
Waunguja n.k
Hayo ni maeneo na sio Kabila,lakini wanatofautiana matamshi na lafudhi. Sembuse America ambayo jimbo moja ni kubwa zaidi ya nchi yetu,washindweje kutofautiana?
Aah wapi waganda ni walugaluga tu, mambo ya “singingi, goingi “hahaaa, Zimbabwe is one of the best kwenye English. Hata watanzania wasio na accent za lugha za makabila wana pronouncing efficiency nzuri sana kuliko waafrika wengi.Kwa hapa Afrika napenda mno kiingereza cha waganda na wazambia.
Ni kwa sababu hawachanganyi na lugha zao za asili kama wanaigeria na waghana.Kwa hapa Afrika napenda mno kiingereza cha waganda na wazambia.