Kati ya Mwingereza na Mmarekani Ni yupi huwa unamuelewa kwa urahisi akiwa anaongea kingereza?.

Scotland aka Scottish, Australians

Kiingereza ni lugha ya kuungaunga sana.
Lugha gani ambayo watu kutoka maeneo tofauti wanaongea tofauti na unaweza usielewe.

Sasa kuna wahindi, wanijeria, wajamaica nao wamekuja na kiingereza chao basi kazi kwelikweli.

Ngoja nasisi wa mtoni mtongani tuanze kuongea English yetu mixer kimakonde, kimakua, kizaramo, unaweka na kisukuma inakuwa getegete kabisa.
 
De
Ila movie za NY hasa hasa za Tupac nazielewa
Juice
Above the rim
Poetic justice
All eyes on me
Resurrection pia hawa kina Ice Cube ya Straight outta Compton.
 
Wote huwa siyaelewi..
Tatizo huwa yanaongea mcharango sana....ila cha ajabu sasa wachozungumza kikiandikwa ni English ya kawaida sana.

Mzee Arsene Wenger au Mourinho wao wanawaelewa bila shida..

Wakiimba au ku-rap ndiyo zero kabisa huambulii kitu..
Kiufupi, Kuelewa Kiingereza ni jambo moja..kumwelewa mzungu akizungumza kiingereza hichohicho ni shule nyingine ngumu mno..Tunajipa mitihani migumu sana WatZ.
 
Deep deep deep
 
Wanaijeria na wajamaika ni funga kazi.😄😄😄
 
Huwa napata ugumu kidogo nikiwa namsikiliza Mmarekani ila namuelewa kwa urahisi zaidi mwingereza.

Wataalam wa kingereza karibuni.

unajua na Wazungu nao wana kiingereza tofauti tofauti kama sisi usikilize Kiswahili cha Zanzibar, Cha usukumani nk nk. Wewe kama unaelewa kiingereza cha uingereza nafikiri unaongelea cha London
Jaribu na cha South Wales!

Ila kwa ujumla ukishazoea ile accent yao na ukawa na msamiati wa kueleweka...utawaelewa na kukufanya usiwe mtu wa kujichekesha chekesha na kupiga makofi hata mzungu akiongea kitu cha kijinga....
 
Ukienda Kilimanjaro ndio kichekesho zaidi. Sio tu kuna tofauti kubwa ya lafudhi na lahaja kati ya wilaya za Siha, Hai, Moshi, na Rombo zilizo ndani ya umbali usiozidi km 100, nenda wilaya kama Rombo isiyozidi sq. km 1,450 kutoka kijiji hadi kijiji kuna tofauti kubwa mno ya matamshi kiasi cha wao kwa wai kutoelewana kabisa.

Nadhani permanent settlement inachangia sana hili kwani watu hawachangamani vya kutosha ku-harmonize lugha. Ni tofauti na pastoralists like Maasai lugha ni moja throughout.
 
Kwa hapa Afrika napenda mno kiingereza cha waganda na wazambia.
Aah wapi waganda ni walugaluga tu, mambo ya “singingi, goingi “hahaaa, Zimbabwe is one of the best kwenye English. Hata watanzania wasio na accent za lugha za makabila wana pronouncing efficiency nzuri sana kuliko waafrika wengi.
 
Ni sawa unauliza watanzania na kuongea Kiswahili..., Uki dig Deep, Kuna Wahaya Wachagga, Wasukuma, watu wa Pwani n.k. na ukiwaweka pamoja ni sawa na watu kutoka mataifa tofauti....

Sasa tukija England kuna watu wa Liverpool Scousers (Rooney, Owen na Steve Gerald) kuna watu wa London (Cockneys) kina Jason Statham, kuna watu wa Midlands kuna watu wa Newcastle (kina Allan Shearer) n.k. ila kwa watu ambao English yao ni balaa ni Scottish People wengine wote ni cha mtoto..., na bado ukija watu wa Wales, au Ireland pia kuna vionjo tofauti...

Ila on average USA wanaeleweka na Uingereza depends ni mtu wa wapi... Ingawa Scotland ni balaa wote yaani karibia wote ni vigumu kuwaelewa (Yaani hata Waingereza wenyewe hawawaelewi); Case in Point angalia hapo chini na huyo ni mbunge sio average Joe...


View: https://youtu.be/1jHfY0dDZxA?si=d6lCR6boYF01OhQt
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…