The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,709
Ukisoma biblia, kwa makini bila mawenge na uzwazwa wa imani, hutakuta mstari hata mmoja ulioandikwa na Yesu. Ni mara moja tu Yesu aliandika.
Ni pale alipoletewa mwanamke 'kahaba'. Alipoulizwa nini kifanyike, Yesu aliandika kwenye mchanga akiwataka waliokowa wakimtuhumu wampige mawe kama alikuwapo ambaye hakuwa na dhambi (Yohana 8.7).
Zaidi ya. hapo, tunachoambiwa au kusoma kwenye biblia ni maneno ya kuambiwa au kuandikwa na wengine hata wale ambao hawakumuona Yesu mmojawapo akiwa Paulo wa Tarso jambazi aliyefisika kwa kuua wanafunzi wa Yesu hadi alipozidiwa kete tokana na kuongezeka na kuwa na nguvu mbali na kukubalika kwa Yesu akajifanya kakutana na Yesu wakati hakuwa amewahi kuonana naye uso kwa uso. Je, alimjuaje wakati hawakuwa wamewahi kukutana?
Mwingine ambaye hakuwahi kukutana na Yesu ni Luka yule aliyeandika injili kama ilivyoandikwa na Luka. Ajabu ya maajabu, Luka anaandika juu ya maisha ya Yesu kwa kusikia siyo kuona. Anyaways. Kwa vile biblia ni mkusanyiko wa vitabu, lolote linawezekana.
Mwisho, Biblia iliandikwa takriban miaka 30 hadi 70 baada ya Yesu kufariki. Je, biblia ni maneno ya Mungu au ya waandishi waliotunga walichoandika na kukipa uungu? Ina maana 'Mungu' hakuwa na njia nyingine ya kuwasiliana na viumbe wake au aliishiwa?
Mbona, tumeumbwa wote na mahitaji na viungo sawa na hakuna maandishi ya kufanya hivyo? Hata ukichunguza korani iliyoandikwa baada ya kifo cha 'Mtume' Muhammad baada ya mrithi na mkwe wake Abu Bakr kumuamuru Zayd ibn Thabeet kuiandika, unagudua hali ile ile kutokana na ukweli kuwa Muhammad alidukua biblia na kuiandika kishairi badala ya free prose mbali na kudukua karibu kila kitu.
Huu utapeli, we acha tu. Watu wangu wanaponzwa na ukosefu wa maarifa kama Yesu alivyowahi kusema akiwaonya waisraeli wenzake ambao alitumwa tu kwa ajili yao na siyo wamakonde waliopwakia mambo ya wengine wakitapika na kupuuzia yale yaliyo yao ili waangamie uzuri.