Kati ya Pharmacy, Shop na Haircut salon ni biashara gani inayoweza kumletea mtu mafanikio ya haraka na ya uhakika?

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
7,799
Reaction score
14,215
Habari zenu wana JF wenzangu.. Ndugu zang kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, ni biashara gani mtu akifanya ataweza kufikia au hata kukaribia ndoto zake za ki maisha haraka haraka? Hasa kwa mkoa wa Dar es Salaam. Kama kawaida natanguliza shukran kwa wote watakaochangia, na hata watakaopitia uzi huu kimya kimya.
 
Sio kila pharmacy itakuhakikishia faida,sio kila duka litakuhakikishia faida,sio kila saloon itakuhakikishia faida. Ninachojaribu kusema ni kuwa faida na mafanikio yanategemea wewe.
 
Mfanyabiashara ni mtu anayenunua na kuuza bidhaa alizotengeneza mwingine na kupata faida kidogo

Mjasiriamali ni mtu anayetengeneza bidhaa zake mwenyewe na kuziuza na hivyo ana uhakika wa kupata faida kubwa

Tafuta biashara ambayo kuna uwezekano wa kuuza bidhaa ulizoandaa au kuzitengeneza mwenyewe hata kama ni kwa asilimia 90 ndipo utakuwa na uhakika wa biashara yako kukulipa lakini siyo kwa haraka haraka
 
Shukran mkuu kwa ushauri wako uliotukuka.
 
Mfanyabiashara ni mtu anayenunua na kuuza bidhaa alizotengeneza mwingine na kupata faida kidogo

Mjasiriamali ni mtu anayetengeneza bidhaa zake mwenyewe na kuziuza na hivyo ana uhakika wa kupata faida kubwa

Tafuta biashara ambayo kuna uwezekano wa kuuza bidhaa ulizoandaa au kuzitengeneza mwenyewe hata kama ni kwa asilimia 90 ndipo utakuwa na uhakika wa biashara yako kukulipa lakini siyo kwa haraka haraka
Nimekuelewa mkuu... Je ikitokea mimi nikafungua salon na kuanza kufanya kazi mwenyew kama kinyozi wa salon yangu. Je huo sio ujasiriamali?
 
NDIYO ni ujasiriamali

Siri ya biashara ya saloon ni eneo

Kama mtaa ni mpya na hakuna saloon zingine uhakika wa kupata hela ni mkubwa ila kama ni mtaa wa zamani na tayari kuna saloon zingine kadhaa hapo tegemea kupata tu hela ya kutosha kulipa Bill ya umeme
 
Hahahaha.. sawa mkuu nimekuelewa vizuri.
 
Mafanikio ya haraka?
Unawahi wapi kwani?
Mkuu ukweli ni kwamba.. kila mfanya biashara hupenda kuona biashara yake inakwenda haraka ili na yeye apate mafanikio ya haraka. Lakini hata kama hakuna mafanikio ya haraka, basi bora mtu uone faida ya biashara husika.
 
Back
Top Bottom