Kati ya pombe, wasichana na kamari kipi kinarostisha Sana?

Wewe kama mimi tu. Huwa naweza kupitia sehemu nakunywa bia 2 tatu, zikishakolea nampigia rafiki yangu aje tunywe. Hata akisema yuko vibaya namlipia boda napenda kampani yake tu.
 
Vyote vinarostisha mkuu

Kupoteza hela ni kupoteza hela tu haijalishi chanzo cha kupoteza
Pombe ni zaidi mzee inakimbizana na kamari kwenye msimamo.

Binafsi sijawahi kujutia kutumia hela kwa ajili ya mwanamke, matumizi yote guwa yanakwenda kama yalivyopangwa.
Ila nimewahi kujutia asubuhi kwa ajili ya pombe. Unakuta ulikuwa na laki 6 jioni halafu unaamka na 83,400 asubuhi na zenyewe za kuokoteza mfuko huu na ule.
 
tiGo nayo imo?
 
Pombe na Mwanamke angalau kuna ka starehe unaambulia. Sasa sijui kamari unaambulia kitu gani
 
Wee mlevi..πŸ˜…
 
Wewe kama mimi tu. Huwa naweza kupitia sehemu nakunywa bia 2 tatu, zikishakolea nampigia rafiki yangu aje tunywe. Hata akisema yuko vibaya namlipia boda napenda kampani yake tu.
Mimi bila kampani hata chupa moja inaisha kwa tabu.
 
Na wengine sio walevi kama wewe tunakunywa tunajielewa
 
Hamna mimi hata pombe sizikubali wala nini sema napenda ma vibe vibe na hauwezi kutoka unywe fanta.
Una vibe vipi kama hujalewa?✌️✌️ Sema nimekuelewa unalewa ila mara moja moja kwa week.πŸ˜…
 
Vyote tu

Ila kamari ni namba moja
 
Na wengine sio walevi kama wewe tunakunywa tunajielewa
Sijafikia kuitwa mlevi. Nakunywa safari 3 kwa mangi kila siku kwa mwaka mzima isipokuwa ijuma na jumamosi naweza kunywa bia 9, nakuwa na likizo fupi ya kutokunywa mwezi wa 7 na 8 kisha nakiwasha tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…