Hassan Mambosasa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2014
- 3,359
- 4,528
Yule jamaa alikuwa ana dharau hadi anatembea na mpira na si kukimbia, kuuchukua ni kazi mno. Alikuwa na chenga nyingi kichwani hadi anasema akiwa mbele ya mpinzani hajui ampige chenga gani anajikuta tu katumia mtindo fulani. Hao kina Messi na Maradona asilimia kubwa wanatumia mbinu zake chacheWote uliowataja bado hawajamfikia fundi wa mpira, Manuel Francisco dos Santos maarufu kama " Garrincha " au Furaha ya Watu.
Alijaaliwa kipaji cha hali ya juu sana livha ya mguu wake mmoja kuwa mfupi na kujikunja ( tege ) anatajwa kama mkokotaji mahiri wa mpira kuwahi kutokea Ulimwenguni sahau kuhusu upigaji wa chenga za maudhi kwa wapinzani.
Ndiye staa aliyeipa Brazil taji la Kombe la Dunia la mwaka 1962 lililofanyika pale kwa Wahuni na watukutu nchini Chile.
Aliibeba Brazil kwenye makwapa yake mara baada ya kuumia kwa Pele kwenye mechi ya pili tu hivyo Garrincha akavaa vyema viatu vya Pele. Na ndio aliyekuwa mchezaji bora wa michuano hiyo.
Sema kutokana na ulevi uliopindukia wengi hawakumpa heshima yake na haishangazi alipofariki mapema kutokana na ulevi.
Ni kama stori ya George Best tu.
Hivyo unapolinganisha hao jamaa zako tafadhali naomba umkumbuke na Garrincha katika orodha yako!