Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hizo A series zinatumia prossecor ya Mediatek?Niliwahi kutumia Samsung J7 prime, iko poa saaana, kulinganisha na hizi A, maana A nyingine ni jamii ya tecno, mfano A10s
Cheap is expensive
Okay thanks...vp s series za samsung?Niliwahi kutumia Samsung J7 prime, iko poa saaana, kulinganisha na hizi A, maana A nyingine ni jamii ya tecno, mfano A10s
Ndo ikoje mkuu???
Okay...s series ipi nzur kwa budget ya laki 7 au 8Samsung j series zilishatoka kwenye soko, na saivi zipo m series kwa ajili ya low end consumers, A series kwa ajili ya midrange consumers na S series zimekuwa kwa ajili ya high end consumers
Carrier unlocked maana yake nin?J-series wamethitisha Production zake...
Tangu mwaka 2018.... matoleo ya J6+, J8 J7 Crown n.k ndio yalikua ya mwisho
Kumbuka
S/Note - High end
A/C - Series - Mid range
J/M - Series - Low end..
C & J hazipo tena kwenye market..
kwenye Mid-range imebaki A - series
Katika low end wameweka M-series...
Japo kdg wanachanganya watu maana M-Series za mwaka huu na mwaka jana zina bei zaid ya A-series.....
Kwa hela hio Nakushauri usije ukanunua Ma A-series ya Mwaka jana au mwaka huu...
Utakua disapointed sana kwenye Camera, speaker na Plastic body zao....
Bora za mwaka 2018.....
Japo m nakushauri kwa hela hio (800k) Mjini unapata S9+ na ukitulia zaidi Note 9..
NOTE : Jitahidi Upate Global/international Model/version.. epuka carrier unlocked..
Watu tununue simu laki 7 halafu mseme sisi ni low end? Kueni na adabu aisee...J-series wamethitisha Production zake...
Tangu mwaka 2018.... matoleo ya J6+, J8 J7 Crown n.k ndio yalikua ya mwisho
Kumbuka
S/Note - High end
A/C - Series - Mid range
J/M - Series - Low end..
C & J hazipo tena kwenye market..
kwenye Mid-range imebaki A - series
Katika low end wameweka M-series...
Japo kdg wanachanganya watu maana M-Series za mwaka huu na mwaka jana zina bei zaid ya A-series.....
Kwa hela hio Nakushauri usije ukanunua Ma A-series ya Mwaka jana au mwaka huu...
Utakua disapointed sana kwenye Camera, speaker na Plastic body zao....
Bora za mwaka 2018.....
Japo m nakushauri kwa hela hio (800k) Mjini unapata S9+ na ukitulia zaidi Note 9..
NOTE : Jitahidi Upate Global/international Model/version.. epuka carrier unlocked..
Ndugu Kuna sehemu nimemwita mtuWatu tununue simu laki 7 halafu mseme sisi ni low end? Kueni na adabu aisee...
Mimi natumia A8 + ya 2018 na niliinunua kipindi hicho hicho zilivyotoka around april 2018.. mpakw leo almost 2 years simu bado ni mpyaa na sina complain. Sijui kwa wengine.
A10s ni MTK ila A10 kavu ndo nzuri sema haina fingure print
HII KITU WATU WANAICHUKULIAGA POA ILA MATOKEO YAKE NDIO UMENUNUA LIJISIMU LINASUMBUA NETWORK AU UNAUZIWA SIMU ILIYOTUMIKA UKIDANGANYWA NI MPYA...Carrier unlocked maana yake nin?
Mkuu hembu Nisomee herufi ya mwisho kwenye model ya hio simu.....pengne hapo ndio tatzo lilipo... labda ulinunua unlocked....Mi natumia A10, kwa baadhi ya maeneo ya vijijini kwa kweli hii simu ni changamoto kwani suala la network inasumbua sana. Utakuta simu nyingine inanetwork lakini yakwangu inakwandikia net work not registered. Yani huwa nachukia sana kuona tecno ya laki moja inaizidi sumsang ya laki 3
Nishawahi kupoteza dili kisa network sim ipo hewani watu wananitafuta wanipe mchongo eti sipatikani. Yaani niliiichukia sana siku hiyo.
Thanks mkuuuHII KITU WATU WANAICHUKULIAGA POA ILA MATOKEO YAKE NDIO UMENUNUA LIJISIMU LINASUMBUA NETWORK...
Si unajua Kuna hizi simu zinauzwa Na Makampuni ya Mawasiliano Mfano Tigo shop?
Ni mara nying sana Tunasikia sijui tigo Anatangaza anauza Tecno mfnao spark 3 n.k n.k kwa promoshen..
Tunajua kbsa tigo hatengenezi simu ila anatoa chip ya sim na huduma zote kutokana na ile chip....
Sasa basi....Kinachotokea Tigo anaingia ubia na Tecno....
Tigo anamsaidia tecno kutangaza simu zake kiurahisi.....Kupitia matangazo yao, wakati huo huo tigo anauza hizo/hio simu kwenye maduka yao kwa bei rahisi zaidi ya Maduka ya kawaida na Anakupa na kifurushi zaidi
Sharti kubwa la tigo analompa tecno ni kwamba....Lazima laini Moja Ifungwe (locked) itumie laini ya Tigo pekeee....
Hii sasa inaitwa CARRIER LOCKED
Sasa sbb Mtu anahitaji urahisi.....
Ameona Atapata hio simu Tigo shop kwa bei rahisi....Pili atapewa na vifurushi vya bure kwa mda flan....Basi naye anaenda kununua simu tigo shop Ambapo Lazima SIM 1 Isome laini ya tigo.....
Sasa ikafika kipnd amechoka kutumia laini ya Tigo kiulazima.....
Anachokifanya anaenda kwa wataalam Ana i UNLOCK ule Mtandao(CARRIER) uliofungwa kwa ulazima.....Kibongo bongo Tunaita Kuflash...
Hili Neno tumelisikia sana hasa miaka ya nyuma kdg
'Nataka ni flash simu yangu Itumie laini zote'
Ku UNLOCK ni kufungua kitu...
CARRIER ni ule mtandao...
Hii sasa ndio CARRIER UNLOCKED sasa...
Hicho ndio kinachotokea Hata huko ulaya/usa n.k
Samsung Anaingia ubia na Makampuni ya simu km Verizon, AT&T, T-Mobile n.k n.k...
Mtumiaji akichoka kutumia ile simu anataka aiuze nje ya USA inabidi aipeleke waka i Unlock ili isome laini zote la sivyo Ndio zile ikija huku simu haisomi laini mpk uipeleke kwa wataalam...
Kwa nini nasema iepuke?
Kwanza Ijulikane kbsa ku flash simu iliyokua imefungwa ni illegal....Hata hao tigo ukiwaambia masuala ya ku flash watakumaind....
Wenzetu ulaya wao wana mda maalumu kutokana na mkataba... ni angalau miaka miwili Ndio unaweza uka i unlock na sheria isikubane
Haiwezekani unitumie mm nikuuzie simu kwa bei chee na kukupa vifurushi vya bure halaf laini yangu huitumii...
Sasa Unapo i flash kuna mawili....
Either Isisome laini kbsa au isome kwa shida...
Kwa ufupi mara nyingi zinazingua network...
NA HIKI NDIO SBB NAKUAMBIA ZIEPUKE...
Unaweza utumie unaona iko poa lkn ukipata simu nyingne km hio hio ambayo ni free utaona utofaut mkubwa...
Wengi washakutana na hili tatzo hasa kpnd kile tunatumia visimu vya vodafone au vile vibatan vya tigo..
UTAJUAJE HII SIMU NI UNLOCKED?
Simple Tu...
simu nyingi zinazokua Locked na mtandao flan...
Zinakua na symbol flan za ule mtandao...
Mfano unakuta imeandikwa tigo juu au nyuma ya simu...
Nyingne ukiiwasha inaakuandikia Vodacom n.k n.k
Kwa zile za US utakua mfano simu imeandikwa au ukiwasha inaandika
VERIZONI, T-MOBILE AU AT&T ukiona hivyo tuu jua Ni unlocked.....
Sasa nying za sikuhz hawaandiki...
Ukiona hivyo njia rahisi ni kusoma Model number...Ambayo inakua nyuma ya simu au ingia ndani kwenye about phone....
kwa Samsung S-series Utaona
Imeandikwa hivi SM-G.... hapo kwenye hivyo vidoti Vinne Ni namba kutokana na simu husika....
Mfano wewe nimekwambia Kwa hela hio Unaweza ukapata S9+ ...
Basi model namba yake PIGA UA
itaanza hivi SM-G965. hicho kidoti cha mwisho sasa namba au herufi itakayomaliziwa hapo ndio muhimu kujua km simu ni Free au Carrier unlocked sasa
Mfano km hio S9+ ilikua locked kwa Mtandao wa Verizoni Utaona imeandikwa hivi
SM-G965V, Kama ni T-Mobile Utaona imeandikwa SM-G965T km ni AT&T utaona
SM-G965A...
Nzuri ambayo haijawa locked.....
Wanaita
Global/international - Model/version..
LAZIMA MWISHO IISHIE NA....F/DS/FD
kwahio Itakuwa hivi
SM-G965F/DS/FD....
Inaweza ikawa chochote kati ya hivyo vitatu.. ila mara nyingi ni F & DS....
Ukiona kwenye hio model Amekuandi DS
Hii inamaanisha hio simu ni Dual Sim(laini mbili)
Kwa samsung Note-series utaona
Imeandikwa hivi SM-N....
Mfano Note 9 Unatakiwa uchukue yenye
SM-N965F/DS
Kwa Samsung Joy a.k.a J-Series Utaona
Imeandikwa hivi SM-J....
Kwa Samsung Alpha a.k.a A-Series utaona
Imeandikwa hivi SM-A....
Hii ni kwa simu zote za samsung hasa matoleo ya miaka hii Global model...
Inatakiwa iishie na ......F/DS
Ila ukipata Model inayoishia na .....0 Au .....U
hizo sio mbaya zinakuwaga vizuri,
Ila sio hayo ma T,V & A.... Japo nazo waweza upate ambayo imekua unlocked vizuri ila PIGA UA jua hio simu ni Used sasa....
Mara nyingi Ukipata Samsung Yenye Laini mbili basi usiwe na shaka ni hii inshu....
ILA ukiona tuu Samsungu Kwa nyuma Chini Imeandikwa jina la Simu......
Mfano Galaxy S6+, Galaxy S7, Galaxy S7 plus,
Galaxy S8+, Galaxy S9+ n.k n.k
Hio kimbia ni Unlocked.....
International model haziandiki Jina kwa nyuma zaidi ya Brand
Inatakiwa uone neno Samsung tuu kwa juu....
Chini labda uone neno DUOS kwa zile za laini mbili au yale maelezo meng kwa maandishi madogo....ambayo yanakua ya model, imei n.k