Kati ya Sumbawanga na Singida Mji upi unafaa zaidi kiutafutaji na Kuishi?

Kati ya Sumbawanga na Singida Mji upi unafaa zaidi kiutafutaji na Kuishi?

Wewe ni kabila gani?
Huko kwenu hakunaga roho mbaya?
Mpaka unarecomend mwenzio aende ina maana ulineemeka, na huwezi neemeka bila mahusiano mazuri na wenyeji, kama uliishi salama na kutoka salama panafaa kuishi

Sent using Jamii Forums mobile app

ukitaka kuijua nchi na watu kaishi maeneo ya vijijini ukikaa mijini utaona kila kitu kipo vizuri,
 
Natumai wote ni wazima na mnachukua hatua za kujihami na corona virus

Moja kwa moja kwenye mada, tusaidiane nataka kufanya maamuzi ya kuweka makazi ya kudumu kwenye moja ya miji tajwa hapo juu sasa ni mji gani unafaa zaidi kwenye nyanja tajwa bila kupuuzia other factors?

Sumbawanga nimeambiwa kuna plenty of food na kilimo ni uhakika pia inapakana na DRC kwahiyo biashara ipo na kuna mzunguko wa pesa na wakazi ni wakarimu japo kuna tishio la ulozi wa radi.

Singida nimeambiwa kumechangamka kibiashara kwa kuwa ni junction ya barabara kuu na jirani na mji mkuu wa serikali Dodoma.

Maeneo yote nayapenda maana nimewahi kuishi kipindi nasoma kwa nyakati na muda tofauti. Hali ya sasa ikoje na future ya miji husika inasomekaje?

karibuni kwa tips

Nachojua mimi Singida kuna totozi kali sana,changamkia fursa mkuu

Sent using IPhone X
 
Wewe ni kabila gani?
Huko kwenu hakunaga roho mbaya?
Mpaka unarecomend mwenzio aende ina maana ulineemeka, na huwezi neemeka bila mahusiano mazuri na wenyeji, kama uliishi salama na kutoka salama panafaa kuishi

Sent using Jamii Forums mobile app
Haiondoi ukweli wafipa wana roho mbaya
 
siamini kama vigezo ulivyotoa vinaweza kukusaidia kufanya informed decision. kwa mfano sumbawanga kuna ardhi ya kutosha. lakini kwa kiasi kikubwa imechoka. Halafu sumbawanga wana msimu mmoja wa mvua kwa hiyo, when you think of farming in sumbawanga, you need also to think on how you will be able to tap water. asikudanganye mtu, kilimo cha kutegemea mvua ni kilimo cha ujima.
Ardhi ya sumbawanga imechoka?!! Ambako watu bado wanaweza lima mazao bila mbolea na wakavuna?!! Sumbawanga mvua za wasiwasi?? Hujawahi ishi huko, mimi mkoa mzima wa rukwa, na katavi nimetembea, naweza kusema ktk mikoa ya TZ, ambayo bado ina ardhi nzuri ya kilimo ni hiyo, na mvua za uhakika.
 
Wasukuma wengi wapo mpanda,Katavi.
Hiyo ya wenyeji kuwa na roho mbaya imekaaje mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
hili la roho mbaya kwa wenyeji lipo mikoa yote kasoro pwani na dar es salaam ambako wenyeji wameuza maeneo yao na kukimbilia mbali.
mji ukiwa na taa tu wamatumbi wanahama na kuingia mbali na mji
 
Ardhi ya sumbawanga imechoka?!! Ambako watu bado wanaweza lima mazao bila mbolea na wakavuna?!! Sumbawanga mvua za wasiwasi?? Hujawahi ishi huko, mimi mkoa mzima wa rukwa, na katavi nimetembea, naweza kusema ktk mikoa ya TZ, ambayo bado ina ardhi nzuri ya kilimo ni hiyo, na mvua za uhakika.
that is history, the only place in rukwa where you need a minimal use of fertiliser ni bondeni kandokando ya ziwa rukwa. kwingine kote ni majanga. white wizard, ninajua ninachokiandika
 
that is history, the only place in rukwa where you need a minimal use of fertiliser ni bondeni kandokando ya ziwa rukwa. kwingine kote ni majanga. white wizard, ninajua ninachokiandika
Lini hiyo, wakati mimi hadi leo kuna maeneo mengi wanalima bila mbolea, huko kote, kaoze, muze,,ambao. Ni ukanda wa ziwa rukwa, katavi ndio kabisa!! Asilimia karibu 80 halimaji mpunga hawajui mbolea kabisa, hiyo mikoa bado ina neema sana kwenye kilimo
 
Kuishi Dar labda maisha yanichagulie vinginevyo sipapendi kwa joto na uchafu na uwingi wa watu..Nimekaa huko miaka 4 kuanzia 2012-2016 saizi nikija ni kwenye shughuli maalum
Ulikua unakaa manzese au tandale mjomba
 
Back
Top Bottom