Kati ya timu ya Brasil na ya England ipi inapendwa zaidi.

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Hizi ni timu za taifa za soka. Pana mtangazaji pale Clouds FM aitwae Lwambano, sijui utafiti huwa anaufanya vipi, yeye anaamini ligi ya England ndio inapendwa zaidi eti duniani na hii huwa anaisemasema.

Leo kaja na timu ya taifa ya England eti inapendwa. Kwa kweli kanichanganya na kujiuliza hivi Brasil inaionaje? Ukiachilia tu timu ya nchi yake yaani Tanzania?
 
England inachukiwa wana mpira wa mdomoni sio kwenye pitch, Brazil ilikuwa favourite ya wengi hususan generation zilizokuwa zinamtambua au kumsikia Pele as well as aina ya mchezo wao ni wa kuvutia, England na mashabiki wao walevi na hooligans people love to hate them.
 
Naweza kukubaliana na wewe. Na yawezekana hata huyu mtangazaji ni wa aina hiyo.
 
Heh, hivi mara yako ya kwanza kuangalia kombe la soka la dunia ilikuwa mwaka gani?
Acha kukariri,hiyo Brazil yako tangu ichukue ubingwa mwaka 2002 miaka iliyofuata 2006, 2010, 2014, 2018 hakuna maajabu yoyote iliyofanya. Kuna kizazi kimeongezeka cha 2000 ambapo wakati brazil wanachukua ubingwa (2002) hawakuwa na idea yoyote na soccer lakini sasa wana miaka 20+.

Kwa hiyo jibu swali ni utafiti upi unaokuaminisha kizazi cha 2000 kinaipenda Brazil? Halafu pia ni utafiti upi unakuaminisha kizazi cha 1980 kushuka kilichokuwa kinaipenda brazil bado kinaipenda pamoja na kuchabangwa 7-1 na Germany mwaka 2014?
 
Mimi huwa siipendi England na huwa naiombeaga mabaya siku zote,imetokea hivyo tu wala sina sababu.
 
Sijui nikoje, hakuna timu ya taifa duniani nisiyoipenda kama England wana kelele, lakini ligi yao naipenda sana.
 
Timu ya taifa ya England n overated Sana kwa ss wenye umri wa 33+wengi tunashabikia Brazil

Kiukwel timu ya England nimetokea kuichukia bila sababu za msingi

Ila ligi yao naielewa Sana na nakiri hakuna ligi yenye ushindan Kama EPL

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Timu za taifa zenye mashabiki wa kudumu kama vilabu vya ulaya zilivyo ni Brazil,Germany,Italy na France(nikiwemo mimi mwenyewe niliyeanza kushabikia taifa hili kuanzia EURO2000 France ilipoigaragaza Italy fainali)...timu zingine zinakuwaga na mashabiki wa kuzuka tu kwa sababu ya fomu ya timu husika kwa wakati huo....
 

Sasa unataka wote washabikie kile unachoshabikia wewe!!
 
Kama wewe ilikuwa inafika saa 12 jion mama yako hakwambiii kasafishe chemuli usiongee na sisi kwenye timu tunazopenda kama:
Senegal
Ghana
Nigeria
Cameroon
Brazil
France
German
Netherlands
Italy.....

Watoto wa mama wengi wapo ENGLAND...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…