Kati ya timu ya Brasil na ya England ipi inapendwa zaidi.

Brazili kwa muda mrefu imekuwa na mpira mzuri wa kuvutia (samba), hata kama huipendi basi unakuwa na shauku ya kuona vile wanatandaza soka. Kwa tuliobahatika kumwona nabii wa mwisho wa soka, Ronaldinho, alipokuwepo tulikuwepo.
England ni kama simba, ukimsikia Haji Manara akiongea, hutaamini timu anayoizungumzia haiweezi Prisons.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Sasa unataka wote washabikie kile unachoshabikia wewe!!
Sio mimi ni Lwambano anae tulazimisha kuamini eti England ni timu pendwa. Na hii kama ungeelewa kile nilichokiandika hapo juu.
 
England huwa wanahakikisha kitu chao kinatangazwa kwa kila juhudi ili kionekane kizuri hata kupita chako, na ukijitambua utapigwa vita kila kona.
 
Sio mimi ni Lwambano anae tulazimisha kuamini eti England ni timu pendwa. Na hii kama ungeelewa kile nilichokiandika hapo juu.

Wapo wanaoipenda na wasioipenda pia wapo. Ni kama Argentina na Brazili wako wanaozishabikia na wapo wasiozishabikia.

Mimi sikufichi, katika timu ambazo hazipo akilini mwangu, na haitatokea nishabikie ni England, Marekani na Brazil.
 
Duh, kaazi kweli kweli! Mie sijazungumzia ubingwa hata Lwambano vilevile. Alichozungumzia Lwambano ni UPENZI kwa timu ya England kwa kuongeza SANA ilhali bila tafiti tu pana timu za taifa kama Brasil zinazopendwa mno na wanasoka dunia nzima.
 
Pole sana, kwanini uwe na 'stress' ndugu yangu kwa hao wapenda misifa?

Ndio maana nikasema, usilazimishe wote wakufuate wewe, kila mmoja na mapenzi yake. Mimi hapa ni shabiki wa kutupwa wa Argentina na Spain, but siwapi asilimia zote.
 
Walicho fanikiwa Ulaya ni kuua aina ya mchezo wa Latin America. Nilipata habari kuwa kila mchezaji yeyote atakaeibuka huko lazima aende Ulaya kwa njia yoyote, ndo maana utakuta siku hizi timu za taifa siku hizi zinzcheza soka la Ulaya.
 
Ndio maana nikasema, usilazimishe wote wakufuate wewe, kila mmoja na mapenzi yake. Mimi hapa ni shabiki wa kutupwa wa Argentina na Spain, but siwapi asilimia zote.
Lah! Nielewe, mie silazimishi watu waipende timu ya taifa ya soka ya Brasil ila kitendo anachofanya mtangazaji wa Clouds FM ya kutulazimisha anachokiamini yeye kuwa ndo cha dunia nzima ndo nakihoji hapa.
 
Poa mkuu Jacobus
 
England ni over rated tena na vyombo vyao vya habari. Hawana lolote wale. Tena ngoja wakutane na timu kama France, Italy, Belgium hapo ndo utaona ubovu wa England.
 
England ni Kenya iliyochangamka [emoji41][emoji41]
 
Heh, hivi mara yako ya kwanza kuangalia kombe la soka la dunia ilikuwa mwaka gani?
Nikwambie tu brazil ilikuwa inapendwa zamani lakini sio sasa, timu za taifa unaweza hamisha mapenzi, kwa mfano mimi kipindi brazil inapendwa karibia na kila mshabiki wa soka duniani nilikuwa nashabikia brazil na Germany lakini sasahivi naangalia wanacheza nani na nani nachagua upande, pia naangalia ni timu gani ya taifa inawachezaji wa club yangu ndio nashabikia
 
Duh, kaazi kweli kweli! Mie sijazungumzia ubingwa hata Lwambano vilevile. Alichozungumzia Lwambano ni UPENZI kwa timu ya England kwa kuongeza SANA ilhali bila tafiti tu pana timu za taifa kama Brasil zinazopendwa mno na wanasoka dunia nzima.
Duh umgumu kuelewa. Luambano kazungumzia uwezakano wakupendwa zaidi kwa england kwa sababu ya ligi yake kufuatiliwa zaidi. Ukiachana na England , huamini kama timu za taifa zinapendwa zaidi kutokana na mafanikio ya mara kwa mara kwa taifa hilo? Je huamini kama brazil ilikuwa inapendwa zaidi hiyo miaka ya 90 kutokana na mafanikio yake ya mara kwa mara kama vile 1998 kufika fainali na 2002 kuwa bingwa. Sasa kile kizazi ambacho hakijawahi shuhudia mafanikio ya brazil ni utafiti upi unakuaminisha kuwa kinaipenda zaidi brazil kuliko mataifa mengine?
 
Ulimsikiliza au unazungumzia nilichokiandika kiushabiki tu? Mie nilimsikiliza na ndo maana nimehoji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…