Kati ya Toyota Brevis na IST ipi inaweza kuishi miaka mingi?

Kati ya Toyota Brevis na IST ipi inaweza kuishi miaka mingi?

Cresta niliyotumia mimi ni ya 2.0L na ambayo ndio engine common kwa cresta nyingi zikizoko bongo,ingawa pia cresta ana version zake nyingine zinazotumia engine the same na zilizoko huko kwny brevis za(2.5L&3.0L).

Brevis ziko za 2.5L(IJZ-GE/1JZ-FSE) na 3.0L(2JZ-GE/1JZ-FSE).


Hio Brevis ya 2.5l inakula wese juu kidogo ya Cresta ya 2.0L,hio brevis ya 3.0L kwny wese jiandae mzee vzr baba maana inakula kuliko zaidi boss.
Ahsante kiongozi 👏
 
Matumizi ya gari na uhai wake inategemeana na geografia ya eneo unapolitumia...
Brevis tulitoka nayo home Ile gari ni balaa mafuta ya Lita 10 inanusa Tu yamekata.. na services yake hata spare zake ni gari...
Mkuu swala la kupitwa na gari ni mguu wako na woga wako kwenye kuendesha,hiyo IST unayosema ilifika 160 na bado ilikuwa mbele yako inawezekana mwenzio alikuwa kwenye 180 ambayo ni max.speed,wewe ukawa unaiogopa lakini hapo usingekuwa muoga ukazidi kukanyaga mafuta obvious ugeikuta,na hasa kwenye miinuko,yenyewe pale lazima ingekuwa inapoteza na wewe ungeicha...
 
Ile ngoma inachezea 6km/L mkuu.
umenishawishi niachane, niiweke pembeni Harrier (2003)
hili dude Brevis huwa linanifyeka barabara kn nimesimama, ila kwangu milimani
km Corona limeishusha bei kweli nitajitumbukiza
nihabarishe ajali iliyoipata hiyo Brevis na wewe ulikuwemo ndani? maana madhara yake haona ni kidogo kutokana na muundo wake, km vile halianguki hovyohovyo (stable sana barabarani)
 
Huo mchuma uko poa niliwahi kupiga nao masafa japo sikua dereva ila niliukubali.
Kama uwezo wa kujaza wese ni uhakika komaa na brevis,sababu engine kubwa pia maana yake maisha marefu, hizi gari zenye engine ndogo maisha yake hua sio ya muda mrefu saana.

Nilinunua Cresta mwaka 2008(1G-FE beams,2.0L,6 clyinders),baadae madalali wakaanzisha story za jini mafuta sijui nini lkn ile gari ilikua ni the best na haikuwahi kua na magonjwa aisee, ingawa wese kila mwezi nilikua natumia 400,000 (mafoleni) nikiwa dar lkn nikiwa mikoani ilikua 250,000 kwa mwezi.

Isingekua kupiga nayo mzinga 2015 ile gari nisingeiuza maisha yote maana ilikua ni back up car ya uhakika,any time any where.Na wkt inakula mzinga ilikua inasoma Km 267,000 lkn haikuwahi kua na shida hata moja.

Kwa mtu anayetaka magari ya kudumu lkn akijua resell value yake itakua ni ndogo hayo magari yanayoitwa majini mafuta ndio muafaka kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye maisha Yangu hata iweje sitaweza kununua IST,vitz na passo. Sisi wabongo ni watu wa kukariri Sana unakuta mtu ananunua Passo eti Kwa ajili ya kubana matumizi bila kujua engine yenye cc ndogo ni majanga na huwa haiwezi kuvumilia Safar ndefu.
Safari ndefu ya wapi hizo gari zisifike?
Kwani una ndoto ya kumiriki gari moja tuu?
 
Kwenye maisha Yangu hata iweje sitaweza kununua IST,vitz na passo. Sisi wabongo ni watu wa kukariri Sana unakuta mtu ananunua Passo eti Kwa ajili ya kubana matumizi bila kujua engine yenye cc ndogo ni majanga na huwa haiwezi kuvumilia Safar ndefu.

Mkuu kila mtu anafanya jambo kwa uwezo wake na mapenzi yake pia


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ndio,sababu engine za mark X(3GR/4GR) zili replace IJZ/2JZ zinazopatikana kwny Brevis so hata kwny wese mark-x ina improvement lkn kwny reliability Brevis iko more reliable.
Ahsante kiongozi,udadisi na maswali kuhusu brevis yamekua meengi maana kuna brevis inanitoa udenda,sasa nikisikia story napata wasi kidogo 😀
 
Mkuu umesahau gari kwenda mbio ni ujasiri wa dreva sio chombo.
Matumizi ya gari na uhai wake inategemeana na geografia ya eneo unapolitumia...
Brevis tulitoka nayo home Ile gari ni balaa mafuta ya Lita 10 inanusa Tu yamekata.. na services yake hata spare zake ni gari... Na brevis haitaki mahali penye tope, minemba na mchanga hapa utaichukia...

Ila kwenye Rami na barabara nzuri, safari ndefu, nashindano, drift unawez ukasema Kweli Dunia tamu.. hata body yake ni ngumu na imara, mziki ukifunga gari kinu kinagonga hatari, Upande wa speed brevis inafyatuka kama lisasi inachanganya haraka Sana na hata ukiwa mwendo ina balance nzuri, tamu Sana...

Kwa upande wa IST Kwa Mtu unayependa gari na uwezo unao sio gari ya kutumia.. mikiki mizito haiwezi na sio gari ya luxury.

Ila hajabu kuna siku nilikuwa naelekea bagamoyo nimeshavuka bunju nikiwa na Toyota TX ya 2015 na nikiwa speend 100, nilipitwa na IST nikaanzisha ligi Ila Huwez amini mpk nafika 160km/h IST bado iko mbele yangu na sikufanikiwa kuipita.


Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom