Kati ya Toyota Brevis na IST ipi inaweza kuishi miaka mingi?

Kati ya Toyota Brevis na IST ipi inaweza kuishi miaka mingi?

Ahsante kiongozi,udadisi na maswali kuhusu brevis yamekua meengi maana kuna brevis inanitoa udenda,sasa nikisikia story napata wasi kidogo [emoji3]

Yaani chuma kiko vzr mkuu,kwa reliability iko fresh kabisa ila kua makini wasikushikishe 1JZ-FSE/2JZ-FSE hizo zenye 'D4' maana kuna watu zimewashinda kuzitunza/kimeo wanawasukumia watu wengine kwa bei chee.

Kama ni 1J-GE/2JZ-GE hio fresh tu, ingawa kwa mazingira yetu ya kawaida hio 1JZ-GE cc 2500(ai 250) inatosha kabisa kwa safari/mambio/misele.

Na kua makini sa hivi wajomba wenye brevis cc 3000 hua wanatoa ile label kule nyuma(Ai 300) na kupachika (Ai 250) ili kumdanganya mnunuaji kwamba ni CC 2500.
 
4GR ili replace 1JZ-FE so ina improvents, hata kwny wese inakula vzr.
Sawa mkuu kwa uono wangu kabla sijaenda kwenye Crown, ngoja na mimi niendeshe yebo yebo za dsm nichukue 3S- (RS200) then Mark X halafu wakina EJ20 then huyo GRS180
 
Wakuu na mimi naomba kujulishwa kuhusu uimara wa Toyota Premio toleo la zamani (tangu mwaka 2000) kuhusu ulaji wa mafuta na upatikanaji wa vipuri maana kuna jamaa yangu analiuza nami nalitaka ila mimi siyo mtaalamu wa magari. kuhusu kipato changu ni cha kudunduliza maana nimejiajiri.
 
Yaani chuma kiko vzr mkuu,kwa reliability iko fresh kabisa ila kua makini wasikushikishe 1JZ-FSE/2JZ-FSE hizo zenye 'D4' maana kuna watu zimewashinda kuzitunza/kimeo wanawasukumia watu wengine kwa bei chee.

Kama ni 1J-GE/2JZ-GE hio fresh tu, ingawa kwa mazingira yetu ya kawaida hio 1JZ-GE cc 2500(ai 250) inatosha kabisa kwa safari/mambio/misele.

Na kua makini sa hivi wajomba wenye brevis cc 3000 hua wanatoa ile label kule nyuma(Ai 300) na kupachika (Ai 250) ili kumdanganya mnunuaji kwamba ni CC 2500.
Nikucheck card ya gari kwanza kabla ya mambo yote sio
 
umenishawishi niachane, niiweke pembeni Harrier (2003)
hili dude Brevis huwa linanifyeka barabara kn nimesimama, ila kwangu milimani
km Corona limeishusha bei kweli nitajitumbukiza
nihabarishe ajali iliyoipata hiyo Brevis na wewe ulikuwemo ndani? maana madhara yake haona ni kidogo kutokana na muundo wake, km vile halianguki hovyohovyo (stable sana barabarani)
Hapana sikuwepo
 
Matumizi ya gari na uhai wake inategemeana na geografia ya eneo unapolitumia...
Brevis tulitoka nayo home Ile gari ni balaa mafuta ya Lita 10 inanusa Tu yamekata.. na services yake hata spare zake ni gari... Na brevis haitaki mahali penye tope, minemba na mchanga hapa utaichukia...

Ila kwenye Rami na barabara nzuri, safari ndefu, nashindano, drift unawez ukasema Kweli Dunia tamu.. hata body yake ni ngumu na imara, mziki ukifunga gari kinu kinagonga hatari, Upande wa speed brevis inafyatuka kama lisasi inachanganya haraka Sana na hata ukiwa mwendo ina balance nzuri, tamu Sana...

Kwa upande wa IST Kwa Mtu unayependa gari na uwezo unao sio gari ya kutumia.. mikiki mizito haiwezi na sio gari ya luxury.

Ila hajabu kuna siku nilikuwa naelekea bagamoyo nimeshavuka bunju nikiwa na Toyota TX ya 2015 na nikiwa speend 100, nilipitwa na IST nikaanzisha ligi Ila Huwez amini mpk nafika 160km/h IST bado iko mbele yangu na sikufanikiwa kuipita.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hio TX si ni diesel engine mkuu 1KD bila shaka, kuipata 160kph kwa diesel ni shughuli pevu kidogo. Mchanganyo wake sio kama wa Petrol maana ukiipa pedeli ni ndani ya sekunde kadhaa tu unakuwa umegusa 100! Ukikomalia chini unafuta kisahani ndani ya dakika 3 tu.
 
Back
Top Bottom