Kati ya wabunge wa EALA waliochaguliwa ni wawili tu ndio wenye uwezo wa kupambana ktk mijadala. Tanzania inakwenda kushindwa na kuadhirika

Kati ya wabunge wa EALA waliochaguliwa ni wawili tu ndio wenye uwezo wa kupambana ktk mijadala. Tanzania inakwenda kushindwa na kuadhirika

Hivi,huwa najiuliza ni kweli kati ya wabunge waliopo bungeni yupo hata mmoja ambaye yeye ni mtetezi wa wananchi,mtoa hoja zenye mashiko na mfuatiliaji wa utejekezaji wa maagizo na maazimio?Au wanaanza na kuwaza mapesa halafu kwa mbaaaliii ukikaribia uchaguzi mwingine ndiyo wanajidai kujichachamalisha kwa vibweka tu?
 
..kama tunaitakia mema nchi yetu hili zoezi lirudiwe.
 
..inawezekanaje NCHI nzima tukachagua wagombea kama wale?

..hata wangezungumza kwa Kiswahili ujengaji hoja wao ni wa mashaka-mashaka.
Siasa wamegawana wenyewe. Tupambanie fursa nyingine
 
utaenda wapi sasa- mchezaji wa zamani Sunday Manara; Msemaji aliyefungia Haji Manara. Kocha Jamhuri Kiwelo; mchezaji wa akiba Kiwelo Jr.
Lol....labda uvuvi wa samaki Ziwa Tanganyika...Huku kote wamegawana wenyeee nao
 
Hii nchi imepoteza sifa ya ushindani kwenye mambo mengi sana, tena muda mrefu, sijui kwanini mnapigia kelele suala la ubunge wa Afrika Mashariki zaidi, ikiwa humu ndani tumekubali kuongozwa na akili ndogo za kujipendekeza zinazoteuliwa kuongoza kila sekta, au hofu yetu ni kuogopa ujinga wetu usijulikane nje? waache waujue.
 
Mkuu Mungunalishagawa taranta akamaliza sasa hivi anahangaika kuzuia mwezi, jua na nyota zisigongane basi
Hajamaliza bado...kuna moja au mbili hazinaga mwenyewe...ila hatujiongezi. Tunaopenda kujazana kuliko jaa tayari
 
Back
Top Bottom