Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

tempo_user1, kanuni ni rules of the game, hazihitaji kufanyiwa tafakari wala tafakuri, zinahitaji kufuatwa tuu, "rules must be obeyed" Mh. TL hakufuata kanuni, Chadema lost, na sio Chadema, wapenda demokrasia ya kweli wote pia wamewaangusha!.
Kama kanuni ilihitaji pingamizi, kwa nini Chadema hawakuweka pingamizi?. Au ndio walitafakari wakaona bora waendelee?.

Pasco,
Nakaribia kukubaliana na baadhi ya wanaJFkwamba unapenda kuendesha ligi tu zisizo na tija. Siwezi kuamini kwamba hujui pingamizi linawekwaje. Nimekuuliza masawali hapo kabla lakini umeyapiga chenga.
Mkuu nadhani unahitaji kujisomea vizuri matumizi ya sheria na kanuni za bunge, otherwise utakuwa umeamua tu kupotosha watu.
 
@Pasco, naomba niweke tena sehemu ya kifungu cha 86 ambacho ndio msingi wa hoja yako. Soma taratibu then naomba utupe tafsiri ya kipengele cha nne (in red & underlined) hapo chini.

86.-(1) Siku ambayo Muswada wa Sheria uliokwisha kujadiliwa na Kamati umepangwa kwenye Orodha ya Shughuli, Waziri,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mwenyekiti wa Kamati au Mbunge mwenye Muswada husika atawasilisha hoja kwamba Muswada wa Sheria ambao atautaja kwa jina Kusomwa Mara ya Pili.
(2) Hoja ya Muswada wa Sheria Kusomwa Mara ya Pili itakuwa
kama ifuatavyo:-
"Kwamba, Muswada wa Sheria uitwao….. sasa usomwe mara ya pili". Au kadri itakavyokuwa; "Kwamba, Muswada uitwao ……………… kama ulivyorekebishwa kwa mujibu wa jedwali la marekebisho au kama ulivyochapishwa upya sasa usomwe mara ya Pili."
(3) Haitakuwa halali katika hatua hii kuleta hoja ya kufanya mabadiliko katika hoja isipokuwa tu kwamba:-
(a) mabadiliko bila kutoa sababu yanaweza kutolewa kwa kusema: "Kwamba, Muswada huu usisomwe mara ya Pili sasa na badala yake usomwe baada ya ….. kuanzia …..", na hapo muda ambao Muswada huo unaokusudiwa kusomwa utatajwa.

(b) mabadiliko yenye kutoa sababu yanaweza kutolewa kwa kusema: "Kwamba, Bunge hili likatae Muswada huu Kusomwa
Mara ya Pili kwa sababu zifuatazo …….", na hapo sababu za kupinga Muswada Kusomwa Mara ya Pili zitatajwa kwa ukamilifu.
(4) Iwapo hoja itatolewa chini ya fasili ya 3(a) na (b) ya Kanuni hii, Spika atalihoji Bunge ili kufikia uamuzi.
FJM, nimeuliza swali, na nitaelea kuliuliza mpaka kesho na kesho kutwa, kwanini Chadema hawakuwasilisha pingamizi la muswada ule kwa mujibu wa kanuni?.

The rest ni immaterial, eti kwa vile spika atalihoji bunge, ndio sababu msiwasilishe pingamizi?. Pia nimeuliza sheria imepita, Chadema wamepata nini?, nothing!. Washabiki wenu humu wanataka kuwahamasisha muisusie na tume ya kukusanya maoni!, mtapata nini?. Ila pia nakubali ule msemo wa 'zimwi likujualo' labda mnaona inafaa katiba hii hii iendelee, mkisusia mchakato, ua mkipiga kura ya hapana, katiba iliyopo itaendelea!
 
Mzee Mwanakijiji, mtu anapotaka kuvuka mto, kina cha maji hakipimwi kwa macho, bali mtu huingiza mguu kidogo kidogo na akifika mahali maji yakamfikia magotini huku hata nusu ya safari hajafika, ndipo hurudi alipotoka kwa kuogopa akiendelea ataweza kuzama.

Mhe. Tundu Lissu hakupaswa kuisoma ile hotuba yake ya kambi ya upinzani, alipaswa kwanza atoe pingamizi, na mano ya kuyasema kwenye pingamizi hilo yameainishwa, baada ya kutoa pingamizi, hatua ya kwanza, muswada ungesitishwa, baada ya hapo Lissu angetakiwa sasa kutoa sababu zake ambazo zingekuwa seconded na wabunge wengine wowote.

Uamuzi wa kuendelea au kutoendelea ungetegemea Lissu ametoa hoja gani kwenye pingamizi hilo, naamini pamoja na uchache wa wabunge wa upinzani bungeni, wanapotoa hoja ya msingi kwa maslahi ya taifa, na hoja yenyewe ikawa na mashiko, wako wabunge makini wa CCM, kama kina Deo Filikunjombe and the like, lazima wangewaunga mkono upinzani, na kwa vile issue yenyewe ni ya kisheria, naamini wabunge wengi wa ukweli, wangewaunga mkono. Tena kwenye utoaji wa pingamizi hilo, wangebanana na kanuni tuu, Mama Spika angekuwa hana pa kotokea.

Mwisho wa siku, bunge zima sasa ndipo lingepiga kura kuunga mkono, hoja ya pingamizi au laa, kwenye kura sasa, ndipo kama hoja ya Chadema ingekataliwa, hapo sasa, ndipo palipostahili kuwasilishwa kwa hotuba ya kambi rasmi ya upinzani ikifuatiwa na honarable walkout!.


Mhe. Lissu baada ya kufika kando ya mto na kuyatazama tuu yale maji, akaamua hapa hatuwezi kuvuka, na kuamua kurudi alikotoka, angepaswa kuingiza kwanza huo mguu na kuona kina cha maji.

Mpaka sasa, hoja yangu ya msingi, haijajibiwa, kwanini Chadema hawakutoa pingamizi kwa muswada ule kwa mujibu wa kanuni?.

Kwanini badala ya kutoa pingamizi, wao ndio kwanza wakatoa go ahead ya majadiliano kuendelea kwa hotuba yao?.

Hivi nikisema kumbe waliotuangusha pale bungeni kwa kuruhusu muswada ule upite kiurahisi vile ndio wenzetu hawa hawa tuliowategemee kupinga kwa kutumia, wao wakapinga kwa kususa?.

Baada ya kusomwa kwa hotuba ya Mhe. Lissu, ndipo wabunge wanasimama kutaka miongozo?, miongozo ya nini tena wakati nafasi ya pingamizi walipewa na hawakuitumia?!. Hata kama spika ningekuwa ndio mimi, ningewazuia ili muswada usonge mbele, na ndicho alichokifanya madam speaker.

Kwa wale wote wanaomshutumu speaker kwa ubabe, hebu someni kanuni, kuna wakati kanuni inamuelekeza speaker asikubali kusikiliza hoja yoyote na anachofanya ni kufuata tuu kanuni.

Nadhani, tufike mahali, tukubaliane kutokubaliana, mimi nikisisitiza Chadema were wrong, they failed us na sasa sheria imeshapitishwa, ikishasainiwa, kuipinga ni criminal offence, na at this jancture, nakuhakikishia Mzee Mwanakijiji na wapenzi wote wa Chadema, there is nothing Chadema can do, wala hao wanaharakati!.

Ndipo hapa ule ushauri wangu unaporudi tena, Chadema wakubali, makosa, sio lazima watubu hadharani, hata kimoyo moyo kama walivyosema hadharani hawamtambui rais, lakini kwa vile ana exist, umtambue usimtambue, yeye anabaki kuwa ni rais!.

Pasco, hivi kweli unaamini wabunge wa ccm wangeunga mkono hoja ya pingamizi ya CDM,
Hakuna mbunge hata mmoja wa CCM + CUF ambaye ambaye hakuunga hoja ya mswada. Hii inaonesha kama waliusoma mswada basi wamekubaliana nao, na kama kuna mbunge makini ndani ya ccm kama unavyosema angejitokeza hata yeye kutoa hiyo hoja. Lakini tumeshuhudia mazingira halisi ya bunge yalivyokuwa, kwanza spika kuusifu mswada kabla ya kuwasilishwa, then matusi na kashfa zilizoendelea, katika mazingira kama hayo bado unaamini upinzani unasauti ?

Hapa inaonekana unazungumzia itifaki kutimizwa, ingawa unajua kabisa matokeo yake.

CDM hawakukosea chochote, wangeshiriki mswada hadi hatua ya kupiga kura, ama kutokuhudhuria kikao kizima cha bunge ama kutumia njia unayoisema wewe, bado mswada ungepita.
 
Usisahau tume ya uchaguzi ya sasa nayo itaendelea.

FJM, nimeuliza swali, na nitaelea kuliuliza mpaka kesho na kesho kutwa, kwanini Chadema hawakuwasilisha pingamizi la muswada ule kwa mujibu wa kanuni?.

The rest ni immaterial, eti kwa vile spika atalihoji bunge, ndio sababu msiwasilishe pingamizi?. Pia nimeuliza sheria imepita, Chadema wamepata nini?, nothing!. Washabiki wenu humu wanataka kuwahamasisha muisusie na tume ya kukusanya maoni!, mtapata nini?. Ila pia nakubali ule msemo wa 'zimwi likujualo' labda mnaona inafaa katiba hii hii iendelee, mkisusia mchakato, ua mkipiga kura ya hapana, katiba iliyopo itaendelea!
 
Pasco,
Nakaribia kukubaliana na baadhi ya wanaJFkwamba unapenda kuendesha ligi tu zisizo na tija. Siwezi kuamini kwamba hujui pingamizi linawekwaje. Nimekuuliza masawali hapo kabla lakini umeyapiga chenga.
Mkuu nadhani unahitaji kujisomea vizuri matumizi ya sheria na kanuni za bunge, otherwise utakuwa umeamua tu kupotosha watu.
Mwita Maranya, Asante, nimekuelewa, nitajisomea zaidi matumizi ya sheria na kanuni ili nisipotoshe tena. Pia naomba hamia huko kwenye ligi zenye tija, naomba uniache nimalizie kuwajibu members hoja zao ili tuimalize hii ligi isiyonatija, au kama vipi muombe mode aifunge, ili twende kwenye tija!
 
Pasco,
Nakaribia kukubaliana na baadhi ya wanaJFkwamba unapenda kuendesha ligi tu zisizo na tija. Siwezi kuamini kwamba hujui pingamizi linawekwaje. Nimekuuliza masawali hapo kabla lakini umeyapiga chenga.
Mkuu nadhani unahitaji kujisomea vizuri matumizi ya sheria na kanuni za bunge, otherwise utakuwa umeamua tu kupotosha watu.



hujasoma mahali anasema yeye ni mtaalamu wa international law!!!!...huyu bwana ni mbishi ajabu
 
Pasco,

Hivi ni CHADEMA peke yao ndio waliokuwa na wajibu wa kuukataa muswada ule??
 
Mwita Maranya, Asante, nimekuelewa, nitajisomea zaidi matumizi ya sheria na kanuni ili nisipotoshe tena. Pia naomba hamia huko kwenye ligi zenye tija, naomba uniache nimalizie kuwajibu members hoja zao ili tuimalize hii ligi isiyonatija, au kama vipi muombe mode aifunge, ili twende kwenye tija!


moshi wa nini sasa na povu lote hilo.......wewe admit kuwa umefunguliwa macho na michango ya watu mbali mbali humu juu ya hio kanuni yako ya 86.......kama jana ulipata nafasi a kumuuliza tundu lissu na akaujibu tena kwa ufasaha...bado ukawa huamini ukaja hapa jf na kuweka pthread hii ukiwa na povu lile lile...hivi ulipata nafasi ya kushiriki harusi ya muro jana sawa sawa??:focus:

sasa hivi hapa unaendelea kupotosha tu na kudanganya watu....
 
Pasco umenena vyema.

Hawa jamaa wa magwanda hawana wakitakacho zaidi ya "shortcut".

Hata Kikwete afanye nini kwao ni kosa tu, tatizo lao ni Kikwete na si Serikali. Hilo lipo wazi kabisa, lakini ukweli ni kwamba Kikwete ndiye aliyefanya mema Tanzania hii zaidi ya Rais yeyote mwingine wa kabla yake na hilo halina utata wala ubishi. Wakae wafikiri.

what??
 
Kikao cha kamati kuu cha CHADEMA kinaendelea, haya tu ni baadhi yatokanayo na kikao cha kamati kuu ambayo yatakuwepo kwenye Tamko rasmi la chama baadaye leo.
1. Chadema imeanika udhaifu na unafki wa CUF hadharani
2. CHADEMA kuomba kukutana na Rais kama Amiri jeshi mkuu na sio mwenyekiti wa CCM ili wamweleze ana kwa ana ukweli wa mambo kuliko kuwatumia watu wa kati wanaompotosha Rais ( inawezekana JK ana dhamira njema kwa Taifa ila tatizo ni watu wa kati.)
3. CHADEMA haikuwahi kuahidi kuleta katiba mpya ndani ya siku 100 ikipewa ridhaa ya kuunda serikali, bali iliahidi kuanza mchakato ndani ya siku 100.
stay tune: more to come
source: kainzi ndani ya kikao kinachoendelea cha kamati kuu ya CHADEMA.
https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/195212-chadema-cuf-ni-chama-dhaifu.html#
 
Mie sikubaliani kabisa na hoja yako. CHADEMA sasa hivi wafanye lolote lile wanaloweza kulifanya ili kuhakikisha kwamba utaratibu wa kuipata katiba mpya unakuwa na muelekeo ambao utahakikisha kwamba katiba mpya itakayopatikana itakuwa ni kwa maslahi ya Tanzania na Watanzania wote bila kujali wapo upande upi kiitikadi.

Magamba wanataka kuuteka nyara huu mjadala wa katiba na kuiandika wanavyotaka wao ili kuhakikisha katiba inaandikwa katika namna ambayo itawahakikishia magamba kuendelea kuwa madarakani milele.
BAK, kwenye bold ndicho nilichoshauri, baada ya Chadema kutukosesha ushiriki wao kwenye kuunda tume, sasa wakubali yaishe, waipe ushirikiano tume kuhakikisha tunaipata katiba mpya. Njia pekee ni kukubali kutoa maoni yao.
 
Pasco,

Hivi ni CHADEMA peke yao ndio waliokuwa na wajibu wa kuukataa muswada ule??

hakika jibu lake atakuletea kanuni ya 86 ambayo hata kuielewa haielewi wakati ni mwanasheria,
sijui ni kwanini hataki kukubaliana na hiyo sheria!! ajabu kweli kweli, hivi kama kweli wabunge wa CCM wangeusoma huo muswada na kuona una mapungufu mbona hakuna aliyesimama kuupinga zaidi ya kuponda wanaharakati wanaoupinga? sijaona popote kwenye vifungu vya kanuni hiyo ya 86 ikionyesha kuwa kambi ya upinzani na hasa CDM kama Pasco anavyotaka kutuaminisha kuwa ndo wanaopaswa kutoa pingamizi la kusomwa mara ya pili, kwanini Pasco ameamka na hii digit ya 86? kunanini nyuma ya pazia? kweli hiki ni kitendawili.
 
Pasco,

Hivi ni CHADEMA peke yao ndio waliokuwa na wajibu wa kuukataa muswada ule??
Mwalimu, sio Chadema tuu, ni mbunge yoyote, kwa vile CUF wana ndoa yao na CCM, usitegemee lolote kutoka kwao!.

Mrema wa TLP na Cheyo wa UDP wote hawa ni spent force, hivyo hope ikabaki kwa Chadema na NCCR-Mageuzi, wale vijana wali bank on Chadema kwa sababu ndio kambi rasmi ya upinzani!.
 
MMM,

Nilivyomwelewa Pasco,ni kwamba CHADEMA wame imiss opportunity ya kuusimamisha na kuuzuia usisomwe mara ya pili kwa kutumia kifungu cha 86.

Wewe kwa upande wakonaona unapinga kwa kusema lisingewezekana.

Kwangu mimi hapo ndipo penye msingi wa hoja.

Je nani mkweli,nasubiri kuona kama ni kweli kuna namna ambayo CDHADEMA wangeweza kuzuia kama alivyosema Pasco.
JMushi, nakushukuru kwa kuelewa hoja yangu, ila pia nikasema, that was a loss, nikashauri maadam sheria imepita, tuvunje kambi ya msuso, tusonge mbele, waipe tume ushirikiano wa kutosha, tupate katiba nzuri!.
 
Haswa CDM wakisusia tena tume tutarajie katiba mbovu kuliko hii ya sasa.

JMushi, nakushukuru kwa kuelewa hoja yangu, ila pia nikasema, that was a loss, nikashauri maadam sheria imepita, tuvunje kambi ya msuso, tusonge mbele, waipe tume ushirikiano wa kutosha, tupate katiba nzuri!.
 
Pasco, hata sikuelewi. Unachotaka kusema hapa ni kwamba kwa kuwa mswada wa sheria umeshapitishwa na rais amesema atautia sahihi basi wale wote wasiokubaliana na utaratibu uliotumika basi wasalimu amri na kunyamaza. How strange! Hicho unachokipigia chapuo hapa ni kwamba, serikali ikipitisha sheria ya aina yoyote, haijalishi sheria hiyo ni kandamizi kiasi gani, basi watu wote wanyamaze na kufuata sheria kama kondoo. It doesn't make sense to me.
Chadema wanatakiwa kukomaa na kuja na plan B.
UmkhontoweSizwe, kwenye option ya utii wa sheria, kumbe wananchi tuna option ya kutii sheria zilizotungwa vizuri tuu?.
Haya muswada umepita, unakuwa sheria, na tuisubire hiyo plan B ili ituletee katiba tuitakayo!.
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
MAAMUZI YA KAMATI KUU YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA MPYA.


Kamati Kuu ya CHADEMA katika kikao chake maalum kilichofanyika siku ya Jumapili, tarehe 20 Novemba 2011 katika Ukumbi wa Hoteli ya Mbezi Garden, Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine, kimepokea na kujadili kwa kina taarifa ya majadiliano na kupitishwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011. Aidha, Kamati Kuu imejadili kwa kina hatua za kuchukua baada ya Serikali, kupitia wabunge wa CCM, kulazimisha kupitishwa bungeni kwa Sheria hiyo bila kuzingatia maoni ya Wananchi na wadau wengine mbalimbali. Baada ya kuyatafakari mambo haya kwa kina, Kamati Kuu imeazimia yafuatayo:

  1. Kamati Kuu imewapongeza wabunge wote wa CHADEMA kwa hatua thabiti na sahihi walizochukua, kwa niaba ya wananchi wa Tanzania, kupinga Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 kusomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa Bungeni bila ya wananchi kushirikishwa kwa ukamilifu kutoa maoni yao na muswada kuboreshwa kwa kuzingatia muafaka wa kitaifa. Kamati Kuu imewapongeza wabunge wa CHADEMA na wale NCCR Mageuzi kwa kususia vikao vya Bunge vilivyojadili na kupitisha Sheria hiyo kwani kushiriki kwao kungeipa uhalali wa kisiasa na kijamii Sheria ambayo haikuzingatia nia na haja ya dhati ya kuweka utaratibu wa kisheria utakaoiwezesha nchi yetu kupata Katiba Mpya yenye kuzingatia na kukidhi matakwa ya umma wa Watanzania;

  1. Kamati Kuu imezingatia kuwa Sheria iliyopitishwa na Bunge ina mapungufu mengi na ya kimsingi ambayo hayatajenga muafaka wa kitaifa juu ya Katiba Mpya na hayataleta mabadiliko yoyote ya kimsingi ya Katiba:

  1. Mchakato wa kuipitisha Sheria ndani ya Bunge ulikiuka Kanuni za Kudumu za Bunge kwani Muswada uliosomwa mara ya kwanza Bungeni sio ulioletwa Bungeni kusomwa mara ya pili na baadae kupitishwa; Kamati ilizuiliwa kukusanya maoni ya wananchi katika mikoa na maeneo mbali mbali; Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano aliingilia kazi na majukumu ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ikiwa ni pamoja na yeye mwenyewe na baadhi ya wajumbe wa CCM kukusanya maoni nje ya utaratibu wa Kamati na baadae kuingiza wajumbe wengine wa CCM na CUF kwa lengo la kupitisha matakwa ya CCM na Serikali ndani ya Kamati bila kuushirikisha wananchi kwa ukamilifu;

  1. Sheria inampa Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mamlaka makubwa ya kuunda Tume ya Katiba na Sekretarieti yake ambayo sio tu itakusanya maoni ya wananchi na kuandaa ripoti, bali pia ndiyo itakayoandaa na kuandika Rasimu ya Katiba Mpya na kusimamia mchakato wote wa wananchi kuijadili na kuipitisha katika Bunge la Katiba;

  1. Sheria inampa Rais na Mwenyekiti wa CCM mamlaka makubwa sio tu ya kupokea ripoti ya Tume ya Katiba bali pia ya kuifanyia mabadiliko ambayo yeye na Serikali yake wataona yanafaa kwa kutumia taratibu za kiserikali za kutunga sheria;

  1. Sheria inampa Rais na Mwenyekiti wa CCM mamlaka makubwa ya kuliitisha tena Bunge la Katiba kwa lengo la kufanya mabadiliko kwenye Katiba Mpya endapo litapitisha Katiba Mpya ambayo yeye Rais, au Serikali yake, au chama chake wataona hailindi maslahi yao;

  1. Sheria inaunda Bunge la Katiba ambalo litakuwa na Wajumbe hadi 400 wa CCM kati ya wajumbe 545 wa Bunge la Katiba. Idadi hii ya wajumbe itaiwezesha CCM kupata theluthi mbili ya wajumbe wanaohitajika chini ya Sheria hii ili kupitisha jambo lolote katika Bunge la Katiba na kwa hiyo Katiba Mpya itakuwa ni ile inayolingana na matakwa na maslahi ya CCM na itakuwa mpya kwa jina tu;

  1. Sheria inatoa nafasi kubwa kwa Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM na vyombo vya uwakilishi vya Zanzibar kushiriki kutunga Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano kinyume na Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 na Katiba ya sasa ambayo imevipa mamlaka ya kutunga Katiba ya Jamhuri ya Muungano vyombo vya Muungano kama Serikali na Bunge ambako Zanzibar ina uwakilishi wa kutosha;

  1. Sheria inahakikisha kwamba muundo wa sasa wa Muungano wa Serikali hautaguswa bali utadumishwa na kutiliwa nguvu licha ya madai ya miaka mingi ya wananchi na mapendekezo ya Tume za Kiserikali kwamba muundo wa Muungano uwe ni wa Serikali tatu;

  1. Sheria inaipa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyoteuliwa na Rais na Mwenyekiti wa CCM mamlaka ya kusimamia mchakato mzima wa kura ya maoni ya kuipa Katiba Mpya uhai wa kisheria. Tume ya Taifa ya Uchaguzi haina uhuru na imeshindwa mara nyingi kusimamia chaguzi huru na haki katika nchi yetu na haiwezi kusimamia kura ya maoni kwa uhuru unaohitajika;

  1. Kamati Kuu ya CHADEMA imesisitiza siku zote kwamba mchakato wa kupata Katiba Mpya unahitaji mwafaka wa kitaifa ambao utazingatia maoni mapana ya makundi mbalimbali ya kijamii. Kamati Kuu inasikitishwa na hatua za makusudi za kufifisha juhudi zote zilizofanyika na wadau mbalimbali katika kufikia mwafaka wa kitaifa juu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Aidha, Kamati Kuu imesikitishwa na upotoshaji wa makusudi wa hotuba ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni uliofanywa na wabunge wa CCM na CUF, wakiongozwa na Spika wa Bunge, Anna Makinda, kuhusu msimamo wa CHADEMA juu ya Muungano;
  2. Kamati Kuu inasisitiza kwamba njia pekee ya kuunusuru Muungano wetu ni kwa wananchi wa pande zote mbili kupiga kura ya maoni kuamua kwamba wanataka kuendelea na Muungano na kama jibu ni ndio, muundo gani wa Muungano huo wanaoutaka. Aidha, Kamati Kuu inarudia msimamo wa CHADEMA kwamba ili kuondoa kero na malalamiko ambayo yameuandama Muungano wetu tangu kuzaliwa kwake, muundo unaofaa ni wa Serikali tatu kama ilivyopendekezwa pia na Tume ya Nyalali mwaka 1991 na Tume ya Kisanga mwaka 1998;

  1. Kamati Kuu inaamini kuwa pamoja na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kupitishwa, bado kuna fursa za kisiasa na kijamii katika kujenga mwafaka wa kitaifa juu ya haja, nia, mchakato na misingi ya Katiba Mpya. Hata hivyo, Kamati Kuu imeshangazwa na kusikitishwa na uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete wa kutozitumia fursa hizo na badala yake kujiingiza katika jalala la taka za upotoshaji uliofanywa na Wabunge wa chama chake juu ya misingi na maudhui ya Sheria hiyo. Kamati Kuu inaamini kwamba badala ya kuwaunganisha Watanzania na kujenga muafaka unaohitajika katika mchakato wa Katiba Mpya, hotuba ya Rais Kikwete kwa wazee wa CCM wa Dar es Salaam imezidi kuwagawa Watanzania kwa misingi ya ushabiki wa vyama badala ya kuwaunganisha kwa misingi ya utaifa;

  1. Baada ya kutafakuri mambo yote haya, Kamati Kuu imeazimia yafuatayo:

  1. CHADEMA itaendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau wote juu ya ubovu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na juu ya haja ya kuwa na sheria itakayoweka utaratibu bora zaidi wa kuunda Tume Shirikishi ya Katiba kwa lengo la kukusanya maoni ya wananchi, kuandaa ripoti na Rasimu ya Katiba Mpya, Bunge Maalum la Katiba na usimamizi wa kura ya maoni itakayowezesha wananchi kufanya maamuzi kwa uhuru na kwa haki;

  1. Ushiriki wa CHADEMA katika mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya uliowekwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba utategemea utayari wa Serikali ya Rais Kikwete kufanya mabadiliko makubwa na ya kimsingi katika sheria hiyo kwa lengo la kujenga muafaka wa kitaifa juu ya mchakato huo;

  1. Kamati Kuu inawaagiza wabunge na viongozi wote wa chama katika ngazi zote kufanya mikutano ya ndani na ya hadhara yenye lengo la kuwaelimisha wananchi juu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na madhara yake kwa mchakato wa kupata Katiba Mpya na bora kwa nchi yetu kwa lengo la kuunganisha umma wa watanzania kuweza kufanya mabadiliko ya msingi;

  1. Kamati Kuu inaamini kwamba uamuzi wa Serikali ya CCM kulitumia Jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya hadhara na maandamano ya amani ya wananchi wanaopinga mchakato uliopitishwa kuwa Sheria sio tu ni kwenda kinyume na haki za kimsingi za kikatiba bali pia unahatarisha moja kwa moja amani, utulivu na umoja wa nchi yetu. Kamati Kuu inasikitishwa na msimamo huu wa Serikali ya CCM kwani unashindwa kutambua ukweli kuwa matumizi ya nguvu za dola hayajawahi kuokoa serikali za kidikteta kuondolewa madarakani na Katiba Mpya kupatikana katika nchi mbali mbali duniani na katika Bara la Afrika;

  1. Kamati Kuu inasisitiza kwamba CHADEMA itaendelea kutumia njia zote za amani, ikiwemo mikutano ya hadhara na maandamano kama ilivyoainishwa na Katiba na sheria husika za nchi yetu kuunganisha nguvu ya umma kupinga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na mchakato wake utakaopelekea Tanzania kutopata Katiba Mpya na bora;


Freeman A. Mbowe (MB)
MWENYEKITI WA TAIFA

Novemba 21, 2011
 
Haswa CDM wakisusia tena tume tutarajie katiba mbovu kuliko hii ya sasa.
Mkuu Ngongo, niliwahi kuchangia mahali kuhusu watumizi ya misuso haswa kwa jamii za kiasiri za kiafrika, mnajua tabia za mususo ni za kina nani, na siku zote huwa sikubaliani na baadhi ya misuso yao, na kwa vile niko very frank, huwa nawaeleza, na kinachofuatiwa ni kushukiwa kwa nguvu zote.
 
Mwalimu, sio Chadema tuu, ni mbunge yoyote, kwa vile CUF wana ndoa yao na CCM, usitegemee lolote kutoka kwao!.

Mrema wa TLP na Cheyo wa UDP wote hawa ni spent force, hivyo hope ikabaki kwa Chadema na NCCR-Mageuzi, wale vijana wali bank on Chadema kwa sababu ndio kambi rasmi ya upinzani!.

Sasa kama unajua ni CHADEMA tu; kwa uchache wao wangewezaje kuwazidi majority ccm+cuf pale spika angewauliza kama hoja ya kuupinga mswada ipite au isipite?????
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, with due respect, Bunge linaendeshwa kwa sheria, taratibu na kanuni, kama kanuni inasema mbunge alete pingamizi, spika is obliged kusitisha na kusikiliza pingamizi, ndivyo kanuni inavyotamka, Mhe. Lissu hakutoa pingamizi na badala yake katoa hotuba ya kambi ya upinzani, kinachofuatia hotuba ya kambi ya upinzani ni majadiliano, mlitaka spika afanye nini?..

Nimeuliza kwa nini Mhe. Lissu hakutoa pingamizi?. hakuna jibu!. Nimeuliza kwa nini Lissu amesoma hotuba ambayo hakupaswa kuisoma in the first place?. Pia hakuna majibu!. Hivi Mzee Mwanakijiji unajua hotuba ile ni passport ya mjadala kuendelea?. Hivi unaelewa hotuba ya kambi ya upinzani ni pre requisite kwa muswada wa serikali kupita?. Jee unajua bila hotuba hiyo muswada unasitishwa na kurudishwa kwenye kamati?.

Pingamizi alitaka kutoa Mnyika, Speaker akakataa, au kwako pingamizi mpaka atoe Lisu?
 
Back
Top Bottom