Mzee Mwanakijiji, mtu anapotaka kuvuka mto, kina cha maji hakipimwi kwa macho, bali mtu huingiza mguu kidogo kidogo na akifika mahali maji yakamfikia magotini huku hata nusu ya safari hajafika, ndipo hurudi alipotoka kwa kuogopa akiendelea ataweza kuzama.
Mhe. Tundu Lissu hakupaswa kuisoma ile hotuba yake ya kambi ya upinzani, alipaswa kwanza atoe pingamizi, na mano ya kuyasema kwenye pingamizi hilo yameainishwa, baada ya kutoa pingamizi, hatua ya kwanza, muswada ungesitishwa, baada ya hapo Lissu angetakiwa sasa kutoa sababu zake ambazo zingekuwa seconded na wabunge wengine wowote.
Uamuzi wa kuendelea au kutoendelea ungetegemea Lissu ametoa hoja gani kwenye pingamizi hilo, naamini pamoja na uchache wa wabunge wa upinzani bungeni, wanapotoa hoja ya msingi kwa maslahi ya taifa, na hoja yenyewe ikawa na mashiko, wako wabunge makini wa CCM, kama kina Deo Filikunjombe and the like, lazima wangewaunga mkono upinzani, na kwa vile issue yenyewe ni ya kisheria, naamini wabunge wengi wa ukweli, wangewaunga mkono. Tena kwenye utoaji wa pingamizi hilo, wangebanana na kanuni tuu, Mama Spika angekuwa hana pa kotokea.
Mwisho wa siku, bunge zima sasa ndipo lingepiga kura kuunga mkono, hoja ya pingamizi au laa, kwenye kura sasa, ndipo kama hoja ya Chadema ingekataliwa, hapo sasa, ndipo palipostahili kuwasilishwa kwa hotuba ya kambi rasmi ya upinzani ikifuatiwa na honarable walkout!.
Mhe. Lissu baada ya kufika kando ya mto na kuyatazama tuu yale maji, akaamua hapa hatuwezi kuvuka, na kuamua kurudi alikotoka, angepaswa kuingiza kwanza huo mguu na kuona kina cha maji.
Mpaka sasa, hoja yangu ya msingi, haijajibiwa, kwanini Chadema hawakutoa pingamizi kwa muswada ule kwa mujibu wa kanuni?.
Kwanini badala ya kutoa pingamizi, wao ndio kwanza wakatoa go ahead ya majadiliano kuendelea kwa hotuba yao?.
Hivi nikisema kumbe waliotuangusha pale bungeni kwa kuruhusu muswada ule upite kiurahisi vile ndio wenzetu hawa hawa tuliowategemee kupinga kwa kutumia, wao wakapinga kwa kususa?.
Baada ya kusomwa kwa hotuba ya Mhe. Lissu, ndipo wabunge wanasimama kutaka miongozo?, miongozo ya nini tena wakati nafasi ya pingamizi walipewa na hawakuitumia?!. Hata kama spika ningekuwa ndio mimi, ningewazuia ili muswada usonge mbele, na ndicho alichokifanya madam speaker.
Kwa wale wote wanaomshutumu speaker kwa ubabe, hebu someni kanuni, kuna wakati kanuni inamuelekeza speaker asikubali kusikiliza hoja yoyote na anachofanya ni kufuata tuu kanuni.
Nadhani, tufike mahali, tukubaliane kutokubaliana, mimi nikisisitiza Chadema were wrong, they failed us na sasa sheria imeshapitishwa, ikishasainiwa, kuipinga ni criminal offence, na at this jancture, nakuhakikishia Mzee Mwanakijiji na wapenzi wote wa Chadema, there is nothing Chadema can do, wala hao wanaharakati!.
Ndipo hapa ule ushauri wangu unaporudi tena, Chadema wakubali, makosa, sio lazima watubu hadharani, hata kimoyo moyo kama walivyosema hadharani hawamtambui rais, lakini kwa vile ana exist, umtambue usimtambue, yeye anabaki kuwa ni rais!.