Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

PASCO huenda uanhoja ambayo hautaki kuiweka wazi. Hebu funguka, kwani kwa matazamo wangu kanuni hiyo ya 86 isingeweza kusaidia kuzuia msawda kusomwa mara ya pili. Pia huenda Lissu asingewasilisha maoni ya kambi rasmi huenda ungekuja na maoni mengine kwamba kwa nini hakusoma maoni yao ndio wapinge. Walichokifanya CHADEMA ninakiona kuwa ni sahihi sana na wameeleza na nimewaelewa kuwa kwanini mchakato mzima utakuwa hovyo na hivyo kunauwezkano mkubwa wa kupata katiba mpya ya hovyo pia
 
Mwenye macho haambiwi tazama! Unaweza kuwa na macho mazuri yanayokuwezesha kuona mbali na karibu.Unaweza kutazama kitu fulani na watu waliokuzunguka wakaamini pasipo shaka kuwa kitu hicho umekiona lakini kumbe macho yako yametua kwenye kitu hicho kijuujuu pasipo Mashiko.

Katika hali kama hiyo, haina maana kuwa wewe ni kipofu, la hasha! Ikitokea hivyo mambo mawili yanaweza kutokea inawezekana umeangalia(kutazama) kitu hicho kwa haraka ama hukuwa makini na hivyo kukosa muda wa kutafakari vizuri ili kuweza kutafsiri kwa usahihi kile ulichokiona.

Pasco, umejaribu kueleza kwa mtazamo wako jinsi CDM walipokosea. Naomba nikukumbushe kitu kimoja kama ulifatilia mjadala wa mswaada huo baada ya mh.Tundu Lissu kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani waliomba mwongozo wa spika bila kupatiwa fursa hiyo, mpaka wengine wakawa wanasikika wakimtaka chinichini "Hoja ja kupinga mswaada kujadiliwa" Lakini spika hakutaka kuwasikiliza! Sasa ktk hali kama hiyo watamwomba msamaha nani?
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, with due respect, Bunge linaendeshwa kwa sheria, taratibu na kanuni, kama kanuni inasema mbunge alete pingamizi, spika is obliged kusitisha na kusikiliza pingamizi, ndivyo kanuni iinavyotamka, Mhe. Lissu hakutoa pingamizi na badala yake katoa hotuba ya kambi ya upinzani, kinachofuatia hotuba ya kambi ya upinzani ni majadiliano, mlitaka spika afanye nini?..

Nimeuliza kwa nini Mhe. Lissu hakutoa pingamizi?. hakuna jibu!. Nimeuliza kwa nini Lissu amesoma hotuba ambayo hakupaswa kuisoma in the first place?. Pia hakuna majibu!. Hivi Mzee Mwanakijiji unajua hotuba ile ni passport ya mjadala kuendelea?. Hivi unaelewa hotuba ya kambi ya upinzani ni pre requisite kwa muswada wa serikali kupita?.
Jee unajua bila hotuba hiyo muswada unasitishwa na kurudishwa kwenye kamati?.
Pasco,
Unazunguka tu hujajibu swali la MMK. UNAAMINI KWA KUTUMIA KIFUNGU 86.3b TL pingamizi lake lingepita?
 
Sijui kwa nini Pasco unang'ang'ania hiki kifungu cha 86 kama ndio silver bullet bila kuangalia kwa ujumla wake. Umeshambiwwa ndani ya hicho kifungu kuna kipengele cha 4 na kinatumika kutoa hukumu ya hoja/pingamizi. Na kimetumika kuzima hoja huko nyuma. Na tayari nimekupa mfano ni jinsi gani kimetumika kupindisha sheria za nchi. Mfano huo ni bunge lililopita ambapo Lissu alitoa hoja ya kutoruhusu mhimili mmoja wa dola kuingilia mhimili mwingine, lakini Spika akatumia hicho kipengele cha 4 na pingamizi la Lissu likatupwa. Mifano iko mingi sana, sasa kama Spika amekuwa anatumia hicho kipengele una uhakika gani kwamba kwenye huu muswada asingetumia?

Lakini kubwa ambalo sijui kwa nini husemi ni kwanini Spika alikataa kumruhusu Mnyika kuongea? Pasco kifungu cha 86 kingekuwa na maana tu kwa nchi au nisema bunge linafuata sheria na taratibu zilizowekwa. Lakini sio hili bunge la Makinda. In fact kama Makinda angekuwa anaaongoza bunge kwa kufuata sheria na taratibu zake huu muswada usingesomwa kabisa kwa mara ya pili kabla maoni maoni ya wananchi hayajachukuliwa. Rejea hansard ya bunge usikie alisema nini Makinda wakati anawaambia wakerebishe muswada mwezi March.
 
Pasco, hivi wangetoa hoja kwa kutumia kanuni ya 86 mjadala ungesimamishwa automatically au Spika angeuliza Bunge na Bunge kuamua? Unafikiri Wabunge wa CCM wangekubali kusimamisha mjadala baada ya kuulizwa na Spika?Sidhani kama wame lose; ukiangalia zaidi utaona kuwa wao wamegain kwa sababu mstari umechorwa kati ya wale wanaoamini Rais na wana CCM wanaweza kufanya yote wayatakayo na wale ambao wanaamini the CCM government is in contempt of the people. Tofauti hii ya maoni ni ya muhimu. Rais na CCM wameweza kulazimisha sheria waitakayo wao kupita - kama walivyofanya kwenye sheria ya gharama za uchaguzi - lakini mwisho wa siku watajikuta ni wao pekee ndio wanaandika hiyo Katiba mpya na wale wanaowaamini au kuwafuata. Je kwa vile sheria imepitishwa ina maana mchakato utakuwa halali kwa kuangaliai first principle? Ukweli ni kuwa CCM hawakuhitaji hoja za CDM au za mtu mwingine yeyote juu ya mswada huu, walikuwa na mawazo yao na wameyatekeleza bila kuzuiwa kwani hakukuwa na mtu yeyote ambaye angeweza kuwazuia. Siyo lazima. Watanzania ambao hawaamini katika uhalali wa mchakato huu kwa sababu umevunja the First Principle wanaweza kuupinga, kukataa kushiriki na kuwahamaisha wengine wasishiriki kwa hoja ambazo zitaonesha kuwa mchakto mzima umekosewa toka mwanzo na haukuwa nafasi ya kufanikiwa kwa sababu ulikuwa ni wa kulazisha kwa kutumia tyranny of thte majority. Wananchi hawawezi kulazimishwa kuitii tume ambayo hawaamini ni halali. Tume kupitishwa na kuundwa hakuipi uhalali (legitimacy) kwani uhalali wa sheria hauji kwa kupitishwa tu bali pia kwa uhalali wa hoja zake na mantiki yake. Mwanadamu hawezi kulazimishwa kutii kitu ambacho ni kinyume na dhamira yake, ukweli na mantiki yake au kile ambacho kinaonekana kwa makusudi kimetengezwa ili kumkandamiza. Wanaoamini kuwa sheria hii ni halali na kuwa mchakato ni halali wanayo haki ya kujitokeza kwa furaha kwenda kutoa maoni yao. Wale ambao wanaamini mchakato huu umesurp power ya wananchi na kuwa umelazimishwa wanayo haki ya kukaaa kushiriki na kuhamasishana kutoshiriki hadi hoja zao zisikilizwe vinginevyo wanalo jukumu la kuhakikisha kuwa itakapokuja kura ya maoni wataenda na kuhamasishana kupigia kura ya "hapana" hiyo referendum na kuzuia Katiba Mpya itakayopitishwa na wana CCM. Wanaweza kukataa kusikiliza maoni juu ya mchakato na wanaweza kabisa kulazimisha watu waje kwenye tume yao lakini watakapoletwa swali hilo kwa wananchi hawana namna ya kuwazuia wale wasioshiriki mjadala kupiga kura ya hapana. Unless waseme watakaopiga kura ya maoni ni WALE TU walioshiriki kwenye kutoa maoni! Kitu ambacho hakimo kwenye mswada huu hadi waufanyie mabadiliko.
Mwanakijiji acha kutetea ubovu. Jamaa wameonyesha utoto wahali ya juu na hili likiachwa hivi hawa jamaa watakuja kututosa kwenye mambo ya msingi kwa sababu tu ya kuendekeza siasa za kitoto. Jamaa wametunyima fursa muhimu ya wao kutoa maoni yao kwenye floor ili tuweze kujua walichokusudia kuwaambia watanzania. Kama Spika angeyakataa basi tungewaunga mkono na kutufanya wote tuamini kwamba bunge hili ni kiini macho. Wamekimbia na hoja zao ili ku-justify maandamano waliyoyapanga. Wameukimbia mjadala kwa visingizio na sababu za kitoto na sasa wanahaha kutaka kumtuhumu kila mtu. Juvenile approaches kama hizi hazikubaliki na ni lazima wajue kwamba Chadema hawana focus yoyote kwenye mchakato huu. Kusoma mara ya kwanza au mara ya pili siyo kunakoboresha mswada. Ni ushiriki wa wabunge katika process ndiyo muhimu. Hawa wamekuwa kila siku wakijadili hoja hizi kwenye midahalo na hicho wanachoita maoni ya wanachi ndicho wamekuwa wakikichangia, kwa nini hawakukitoa bungeni, watu wakisikie, wakipime na kukitolea maamuzi?Hizi politics za brinkmanship hazikubaliki!
 
Pascol usijifanye kama hukuona kilichokuwa kinaendelea bungeni, hivi kwa jinsi Makinda alivyolichukulia hilo suala toka mapema, hivi CDM wangefika je kwenye hiyo kanuni? Mnyika aliomba mwongozo, Machali, Mkosamali wote wakakataliwa sasa unadhani ni kutamka tu kANUNI ya 86 na mswada unasitishwa? Mi nadhani CDM wamechukua hatua stahili kabisa tunasubiri watuletea plan B, C , D n.k ikishindikana CCM na wale wote wenye maslahi ya mda watatunga katiba yao, lakini iko siku hata kwa damu katiba itapatikana.Hata hivyo bado ni mapema mno, binafsi ningeshangaa CCM kama wangekubali jambo hili kirahisi rahisi tu, na wito wangu kwa CDM hakuna haja ya kukata tamaa Mungu yuko upande wenu, kama si leo itakuwa kesho, Kenya wamepata katiba mpya baada ya zaidi ya miaka 15 na kumwaga damu, hivi mnafikiri CCM wangetoa hiyo fursa kirahisirahisi tu, hapa ni kukomaa mbele ya ukweli utajidhihirisha
 
MUUNGANO wa Asasi za kiraia zinazounda Jukwaa la Katiba hapa nchini, umesema mpango wa maandamano yasiyo na kikomo kupinga muswada wa mabadiliko ya katiba kusomwa kwa mara ya pili uko palepale na sasa wanatarajia kutoa utaratibu wa kutimiza adhima hiyo kesho.

Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Deus Kibamba alisema kikao cha Kamati Tendaji kilichokaa juzi kilibariki maazimio yote yaliyokwishatangazwa awali na kusitiza kuwa kesho kitatangaza hatua za utekelezaji wake.

"Kamati tendaji iliyokutana jana (juzi) ilijadili kwa kina hutoba zote za viongozi, ile ya Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na ya kambi ya upinzani bungeni," alisema Kibamba na kuongeza;

"Baada ya kupitia yote hayo kamati hiyo ilibariki maazimio yote yaliyokwishatangazwa hivi karibuni kupitia vyombo vya habari na siku ya Jumanne (kesho) tutatoa tamkoa litakalohusu utaratibu utakaotumika kutekeleza adhima hiyo," alisema Kibamba.

Novemba 14 mwaka huu, jukwaa hilo liliitisha kongomano la Katiba jijini Dar es Salaam na kuelezea adhima yake ya kuitisha maandamano nchi nzima endapo Serikali ingepeleka muswada huo kusomwa kwa mara ya pili bungeni.

Pia likatumia fursa hiyo kuonya wabunge ambao wangeunga mkono na kupitishwa muswada huo uliosomwa kwa mara pili kuwa lingetangaza majina yao haradharani kama wasaliti wa wananchi waliowachagua.

Source: Mwananchi

Sijui kwa nini Pasco unang'ang'ania hiki kifungu cha 86 kama ndio silver bullet bila kuangalia kwa ujumla wake. Umeshambiwwa ndani ya hicho kifungu kuna kipengele cha 4 na kinatumika kutoa hukumu ya hoja/pingamizi. Na kimutumika kuzima hoja huko. Na tayari nimekupa mfano ni jinsi gani kimetumika kupindisha sheria za nchi. Mfano huo ni bunge lililopita ambapo Lissu alitoa hoja ya kutoruhusu mhimili mmoja wa dola kuingilia mhimili mwingine, lakini Spika akatumia hicho kipengele cha 4 na pingamizi la Lissu likatupwa. Mifano iko mingi sana, sasa kama Spika amekuwa anatumia hicho kipengele una uhakika gani kwamba kwenye huu muswada asingetumia?

Lakini kubwa ambalo sijui kwa nini husemi ni kwanini Spika alikataa kumruhusu Mnyika kuongea? Pasco kifungu cha 86 kingekuwa na maana tu kwa nchi au nisema bunge linafuata sheria na taratibu zilizowekwa. Lakini sio hili bunge la Makinda. In fact kama Makinda angekuwa anaaongoza bunge kwa kufuata sheria na taratibu zake huu muswada usingesomwa kabisa kwa mara ya pili kabla maoni maoni ya wananchi hayajachukuliwa. Rejea hansard ya bunge usikie alisema nini Makinda wakati anawaambia wakerebishe muswada mwezi March.
Shukran kwa maelezo FJM.
Ninachokiona mjadala umekwama mahali hapa, kwanza Pasco anasema kama kifungu hicho kingetumika basi uwezekano wa mswada kwenda mbele usingekuwepo. Ana maana Lissu aweke pingamizi halafu spika aombe wabunge wapige kura.
Mimi si mtaalamu wa sheria lakini nimesoma maoni ya 'sooth' aliyesema je Tanzania tunakifungu cha kulazimisha minority wasikilizwe kabla ya mswada kwenda mbele kama US?

Mwanakijiji anasema kwa njia yoyote bado suala hilo lisingezuilika kwasababu hakuna kifungu kinachosema wapinzani wakikataa jambo basi lirudishwe kwa kamati. Pasco hajatueleza kifungu kinacholazimisha hayo kutokea. Hadi atakapotokea mtu na kutupa kifungu kinachopingana na hoja ya mwanakijiji tutabaki kuamini kuwa suala la kurudisha mswada katika kamati kwa pingamizi la wapinzani halipo.

Kama Lissu angesoma Pingamizi bado kura ya 'ndiyo' ambayo ni ya wingi wa CCM na CUF ingeunga mkono mswada, na kinachofuatia ni kumuomba Lissu asome maoni ya kambi ya upinzani.

Hapo CDM wangekuwa na mambo mawili. Kwanza kuamua kutoka bila kutoa maoni na kuwafanya wananchi wasielewe nini wanapinga au (2) Kutoa maoni na kuhalalisha mpango mzima wakati wa kupiga kura ya kupitisha mswada.

Kwa kutambua hilo CDM walifanya kitu kinaitwa pre-emptive strategy kuwa wanaweka pingamizi na kutoa maoni yao na kutoka nje.
Yaani two in one, vinginevyo wangejikuta katika mambo mawili niliyoyasema hapo juu.
Nina uhakika waliangalia option nzuri na hiyo ndiyo ilikuwa open kwao kwa wakati ule.

Huu ni mtazamo wangu ambao si lazima uwe wa kisheria na nasimama kusahihishwa pale nitakapokuwa nimechanganya mtiririko wa taratibu za bunge ingawa haitabadilisha mantiki ya hoja yangu.
 
@Nguruvi3, nakubaliana na wewe kabisa kuwa CHADEMA wangetoka nje bila kusema waliyosema wananchi wasingeelewa wanapinga nini, na ingekuwa rahisi sana kwa CCM na CUF ku-spin mambo. Kwa kusoma hotuba CHADEMA wameweka kumbukumbu bungeni (bila kuchakachuliwa) na wananchi tumesikia kwa masikio yatu muswada ule una matatizo gani, na ni vipi taratibu zimekiukwa including Spika kuingilia shughuli za kamati ya katiba na sheria. CCM hawezi kupindisha mambo maana HANSARD ipo. Hili muhimu.

Pili kama unatumia dawa lakini haupati nafuu yoyote kwa nini uendelee kutumia hiyo dawa? Kama Spika amekuwa anatumia kifungu hicho hicho cha 86 (4) kuhakikisha mambo ya CCM hayaharibiki Pasco ana uthibitisho gani kuwa kungekuwa na exemption kwenye hili?
 
Shukran kwa maelezo FJM.
Ninachokiona mjadala umekwama mahali hapa, kwanza Pasco anasema kama kifungu hicho kingetumika basi uwezekano wa mswada kwenda mbele usingekuwepo. Ana maana Lissu aweke pingamizi halafu spika aombe wabunge wapige kura.
Mimi si mtaalamu wa sheria lakini nimesoma maoni ya 'sooth' aliyesema je Tanzania tunakifungu cha kulazimisha minority wasikilizwe kabla ya mswada kwenda mbele kama US?

Mwanakijiji anasema kwa njia yoyote bado suala hilo lisingezuilika kwasababu hakuna kifungu kinachosema wapinzani wakikataa jambo basi lirudishwe kwa kamati. Pasco hajatueleza kifungu kinacholazimisha hayo kutokea. Hadi atakapotokea mtu na kutupa kifungu kinachopingana na hoja ya mwanakijiji tutabaki kuamini kuwa suala la kurudisha mswada katika kamati kwa pingamizi la wapinzani halipo.

Kama Lissu angesoma Pingamizi bado kura ya 'ndiyo' ambayo ni ya wingi wa CCM na CUF ingeunga mkono mswada, na kinachofuatia ni kumuomba Lissu asome maoni ya kambi ya upinzani.

Hapo CDM wangekuwa na mambo mawili. Kwanza kuamua kutoka bila kutoa maoni na kuwafanya wananchi wasielewe nini wanapinga au (2) Kutoa maoni na kuhalalisha mpango mzima wakati wa kupiga kura ya kupitisha mswada.

Kwa kutambua hilo CDM walifanya kitu kinaitwa pre-emptive strategy kuwa wanaweka pingamizi na kutoa maoni yao na kutoka nje.
Yaani two in one, vinginevyo wangejikuta katika mambo mawili niliyoyasema hapo juu.
Nina uhakika waliangalia option nzuri na hiyo ndiyo ilikuwa open kwao kwa wakati ule.

Huu ni mtazamo wangu ambao si lazima uwe wa kisheria na nasimama kusahihishwa pale nitakapokuwa nimechanganya mtiririko wa taratibu za bunge ingawa haitabadilisha mantiki ya hoja yangu.
Msingi wa hoja ya mkuu Pasco ni CDM kutotumia fursa zote za kibunge zilizopo kupinga BILA KUJALI MATOKEO YAKE!! Sina tatizo na hoja yake ila nina tatizo na jinsi alivyokomaa na hili tangu juzi! Hicho anachoshauri kisingebadili matokeo lakini anavyosisitiza ni kama Matokeo yasingekuwa haya!! Pasco msimamo wako mkali sana juu ya hii hoja yako inanipa maswali mengi mkuu hasa ukiwa moja wa Ma great thinker wa JF mnaoheshimika!
 
Nguruvi angesema hivyo ndugu yangu wala isingekuwa shida kubwa yeye anasema definitively... kwamba mswada ungesitishwa.

Naam!
 
Msingi wa hoja ya mkuu Pasco ni CDM kutotumia fursa zote za kibunge zilizopo kupinga BILA KUJALI MATOKEO YAKE!! Sina tatizo na hoja yake ila nina tatizo na jinsi alivyokomaa na hili tangu juzi! Hicho anachoshauri kisingebadili matokeo lakini anavyosisitiza ni kama Matokeo yasingekuwa haya!! Pasco msimamo wako mkali sana juu ya hii hoja yako inanipa maswali mengi mkuu hasa ukiwa moja wa Ma great thinker wa JF mnaoheshimika!

Sidhani kama hiyo ndiyo hoja angeisema hivyo. Yeye anasema CDM walitakiwa kutumia njia ya 86:3 na kwa kufanya hivyo mjadala wa mswada usingeendelea kabisa. Hii hoja ndiyo tunaikataa kwamba hakuna chochote ambacho CDM ingetumia kuzuia mjadala ule.
 
Heshima kwako Pasco.

Mkuu wangu umesema kweli tatizo la wapenzi wengi wa CDM wanadhani viongozi wa CDM ni miungu hawakosei wako tayari kutetea ujinga wowote kwakuwa umetendwa na CDM.

Mkuu J. Mushi, tatizo members wengi humu sio tuu ni washabiki au wapenzi wa Chadema, bali ni ma fanatics wa Chadema wanawaona viongozi wa Chadema kama miungu watu hivyo wanajikuta wanawaabudu. Wanaamini viongozi wao hawawezi kufanya makosa!.

Amini nawaambieni hili la Chadema kushindwa kutumia kifingu cha 86 kuusimamisha muswada ule was a mistake.

Lissu ni mwanasheria makini, hilo halina ubishi, mimi si mwanasheria kwa sababu I don't practise ila nimetoa tongotongo za sheria za sheria kwa miaka minne full time pale UDSM, Mhe. Lissu hakupaswa kusoma hotuba, alipaswa kutoa pingamizi!. Baada ya pingamizi ndipo hotuba ya kambi ya upinzani ingefiatia.

Bila hotuba ya kambi ya upinzani, muswada wowote wa serikali hauwezi kusonga mbele!.

Nimemuuliza Mhe. Lissu, kwanini alisoma hotuba on the first place wakati alipaswa kuwasilisha pingamizi!.

Mhe. Lissu akanijibu kwa kusoma para ya pingamizi kwenye hotuba yake!. Jee kanuni hiyo ya 86 ndivyo ilivyoelekeza?!. Lissu alikosea pingamizi ni pingamizi tena amewekewa mpaka maneno ya kutamka na hivyo kusitisha process nzima!.

Mhe. Lissu aliposoma hotuba ya kambi ya upinzani, alimaanisha ameikubali hoja ya mtoa hoja, hivyo ku complete the process!.

Mimi ni miongoni mwa wakosoaji wakuu wa Spika Mhe. Mama Makinda tangu day 1. Niliripoti humu jinsi nilivyokutana na RA na kwa kinywa chake mwenyewe RA akanitambia na kusikia kwa masikio yangu mawili kuwa ni yeye RA aliyemuweka Spika SS tena kwa kulipia kura za Wanzanzibari baada ya wabara kumsuport Msekwa!.

RA akanihakikishia ni yeye aliyetoa SS na ni yeye aliyemuingiza Mama Makinda!. Kwenye Press Conference ya Kwanza ya Mama Makinda niliireport live humu na nilimuuliza kuhusu kuwekwa na RA, akajikanyaga kanyaga.

Nimewahi kuanzisha thread kadhaa juu ya madhaifu ya Mama Makinda lakini kwenye hili la kuzuia hoja yoyote baada ya kuwasilishwa hotuba ya kambi ya upinzani she was right!. Hivyo ndivyo kanuni inavyosema!.

Kwenye hili, naamini 100% kwa 100% Mhe. Lissu alichemsha!. Na kwa maoni yangu, JJ.Mnyika ni miongoni mwa hazina kubwa za Chadema, kama angeipitia hotuba ya Mhe. Lissu, isingekuwa vile ilivyo, tena nawaomba sana msiniprovoke nikaichambua hotuba ile, tutaishia kuvuana nguo hapa na kuachana uch..!

Lissu ni school mate wangu tangu Ilboru na ni kichwa cha ukweli, lakini kwenye hili amechemsha big time!.

Naombeni niwape angalizo all ma hopefulls kwamba there is something to be done!.

Please hear me loud and clear, baada ya rais kuusaini muswada huo kuwa sheria, there is nothing Chadema can do!. The only option ni kukubali matokeo, kama walivyojifanya hawamtambui rais Kikwete, japo ni kilaza wa tangu UDSM na GPA yake ya 2.0!, ( Facult wana uwezo wa kuongeza 2 points of grace ili ku salvage last year disco) yeye ndie rais. period.

Muswada ukishakuwa sheria inakuwa ni msumeno inakata nyuma na mbele kama upanga wa makali kuwili!. Chadema, Kibamba wala wanaharakati hakuna lolote wanaloweza kufanya!.

Msifikiri Watanzania ni kama Wamisri, Walibya au Wasyria, Watanzania ni kama kondoo!. Wanaomkumbuka mwanaharakati wa UDSM enzi zile, Bi Sikitiko Kapile alisema Watanzania tuna nidhamu ya ukondoo na hivyo ndivyo tulivyo. Kama Chadema ina bank on peoples powers!, wait for surprises, they are wrong again and again and again!.
 
Mojawapo ya sifa ya kiongozi bora ni kuwa na vision ama kuwa na uwezo wa kufikiri extra mile. Kuwa na upeo wa kuona mbali zaidi. CDM waliona mbali zaidi ya hapo Pasco unapopaona. Nimesoma kwa makini sana matundiko yote hapa kuna hoja moja ya msingi ambayo Mkuu Pasco unaipiga chenga, hujatueleza how possible hoja ile ingerudishwa kwenye kamati bila ya spika kuhoji uafikio ambao definately wengi wangeshinda. Kwa hakika hata wangefanya hivyo kama unavyosema ingekuwa ni kupoteza muda ilahali majibu wanayajua.

All in all hii debate ni muhimu kwa ajili ya kutoa elimu. Halafu Pasco nadhani nawe hukubaliani na muswada ule, kwa nini unafikiri CDM tu ndio wenye jukumu la kukomaa na kuona huo uozo peke yao? Nadhani hoja msingi ni hao ambao hata hiyo hoja ya ubovu wa muswada hawauoni.
 
Sasa swali halijibu swali. Kipengele hicho cha sita kina presume kipengele cha 4 kimeamuliwa kwa Bunge kukubali hoja ya kukataa kama itakavyokuwa imetolewa. Na ukumbuke kipengele cha 86.3b ambacho unakitumia hakimtaji kiongozi wa upinzani. Mbunge yeyote anaweza kukitumia kutoa maelezo yakukataa mswada. Sasa kama hoja ya 86:4 inatimizwa - kwamba baada ya Spika wa Bunge kuliuliza Bunge na Bunge linakubaliana na maelezo ya mbunge aliyetoa hoja chini ya kifungu kidogo cha 3b basi ndio ama kinafuata kifungu cha tano au cha sita. Nisahihishe kama uelewa wangu hauko sahihi. Kwamba kifungu cha sita na kile cha tano kinategea uamuzi unaofukiwa chini ya kifungu cha 4.

Sidhani kama unafanya sahihi. Hivi kwa mfano msemaji wa upinzani (lissu) angesimama na kusema kuwa "Kambi ya Upinzani haina maoni yoyote tunaomba mjadala uendelee" ina maana Spika angewalazimisha watoe maoni? Kifungu cha sita ndicho ambacho Lissu alikitumia kutoa maoni yake kwa niaba ya upinzani. Na alitumia kwa sababu hakukuwa na sababu ya kukataa mswada kwani hata wangekataa hawakuwa na kura ya kuzuia mswada usiendelee. Waliamua kusubiri muda wa kutoa maoni yao (chini ya hicho kifungu kidogo cha sita) na well.. WALITOA MAONI YAO!

Baada ya kutoa maoni yao wakijua kuwa hawana kura ya kuzuia mswada usiendelee waliamua kutoka Bungeni in protest. Yote hayo yakiwa ndani ya uwezo wao wa kidemokrasia. Hawakufanya kosa lolote.
Mzee Mwanakijiji, mtu anapotaka kuvuka mto, kina cha maji hakipimwi kwa macho, bali mtu huingiza mguu kidogo kidogo na akifika mahali maji yakamfikia magotini huku hata nusu ya safari hajafika, ndipo hurudi alipotoka kwa kuogopa akiendelea ataweza kuzama.

Mhe. Tundu Lissu hakupaswa kuisoma ile hotuba yake ya kambi ya upinzani, alipaswa kwanza atoe pingamizi, na mano ya kuyasema kwenye pingamizi hilo yameainishwa, baada ya kutoa pingamizi, hatua ya kwanza, muswada ungesitishwa, baada ya hapo Lissu angetakiwa sasa kutoa sababu zake ambazo zingekuwa seconded na wabunge wengine wowote.

Uamuzi wa kuendelea au kutoendelea ungetegemea Lissu ametoa hoja gani kwenye pingamizi hilo, naamini pamoja na uchache wa wabunge wa upinzani bungeni, wanapotoa hoja ya msingi kwa maslahi ya taifa, na hoja yenyewe ikawa na mashiko, wako wabunge makini wa CCM, kama kina Deo Filikunjombe and the like, lazima wangewaunga mkono upinzani, na kwa vile issue yenyewe ni ya kisheria, naamini wabunge wengi wa ukweli, wangewaunga mkono. Tena kwenye utoaji wa pingamizi hilo, wangebanana na kanuni tuu, Mama Spika angekuwa hana pa kotokea.

Mwisho wa siku, bunge zima sasa ndipo lingepiga kura kuunga mkono, hoja ya pingamizi au laa, kwenye kura sasa, ndipo kama hoja ya Chadema ingekataliwa, hapo sasa, ndipo palipostahili kuwasilishwa kwa hotuba ya kambi rasmi ya upinzani ikifuatiwa na honarable walkout!.

Mhe. Lissu baada ya kufika kando ya mto na kuyatazama tuu yale maji, akaamua hapa hatuwezi kuvuka, na kuamua kurudi alikotoka, angepaswa kuingiza kwanza huo mguu na kuona kina cha maji.

Mpaka sasa, hoja yangu ya msingi, haijajibiwa, kwanini Chadema hawakutoa pingamizi kwa muswada ule kwa mujibu wa kanuni?.

Kwanini badala ya kutoa pingamizi, wao ndio kwanza wakatoa go ahead ya majadiliano kuendelea kwa hotuba yao?.

Hivi nikisema kumbe waliotuangusha pale bungeni kwa kuruhusu muswada ule upite kiurahisi vile ndio wenzetu hawa hawa tuliowategemee kupinga kwa kutumia, wao wakapinga kwa kususa?.

Baada ya kusomwa kwa hotuba ya Mhe. Lissu, ndipo wabunge wanasimama kutaka miongozo?, miongozo ya nini tena wakati nafasi ya pingamizi walipewa na hawakuitumia?!. Hata kama spika ningekuwa ndio mimi, ningewazuia ili muswada usonge mbele, na ndicho alichokifanya madam speaker.

Kwa wale wote wanaomshutumu speaker kwa ubabe, hebu someni kanuni, kuna wakati kanuni inamuelekeza speaker asikubali kusikiliza hoja yoyote na anachofanya ni kufuata tuu kanuni.

Nadhani, tufike mahali, tukubaliane kutokubaliana, mimi nikisisitiza Chadema were wrong, they failed us na sasa sheria imeshapitishwa, ikishasainiwa, kuipinga ni criminal offence, na at this jancture, nakuhakikishia Mzee Mwanakijiji na wapenzi wote wa Chadema, there is nothing Chadema can do, wala hao wanaharakati!.

Ndipo hapa ule ushauri wangu unaporudi tena, Chadema wakubali, makosa, sio lazima watubu hadharani, hata kimoyo moyo kama walivyosema hadharani hawamtambui rais, lakini kwa vile ana exist, umtambue usimtambue, yeye anabaki kuwa ni rais!.
 
Mzee Mwanakijiji, mtu anapotaka kuvuka mto, kina cha maji hakipimwi kwa macho, bali mtu huingiza mguu kidogo kidogo na akifika mahali maji yakamfikia magotini huku hata nusu ya safari hajafika, ndipo hurudi alipotoka kwa kuogopa akiendelea ataweza kuzama.

Mhe. Tundu Lissu hakupaswa kuisoma ile hotuba yake ya kambi ya upinzani, alipaswa kwanza atoe pingamizi, na mano ya kuyasema kwenye pingamizi hilo yameainishwa, baada ya kutoa pingamizi, hatua ya kwanza, muswada ungesitishwa, baada ya hapo Lissu angetakiwa sasa kutoa sababu zake ambazo zingekuwa seconded na wabunge wengine wowote.

Uamuzi wa kuendelea au kutoendelea ungetegemea Lissu ametoa hoja gani kwenye pingamizi hilo, naamini pamoja na uchache wa wabunge wa upinzani bungeni, wanapotoa hoja ya msingi kwa maslahi ya taifa, na hoja yenyewe ikawa na mashiko, wako wabunge makini wa CCM, kama kina Deo Filikunjombe and the like, lazima wangewaunga mkono upinzani, na kwa vile issue yenyewe ni ya kisheria, naamini wabunge wengi wa ukweli, wangewaunga mkono. Tena kwenye utoaji wa pingamizi hilo, wangebanana na kanuni tuu, Mama Spika angekuwa hana pa kotokea.

Mwisho wa siku, bunge zima sasa ndipo lingepiga kura kuunga mkono, hoja ya pingamizi au laa, kwenye kura sasa, ndipo kama hoja ya Chadema ingekataliwa, hapo sasa, ndipo palipostahili kuwasilishwa kwa hotuba ya kambi rasmi ya upinzani ikifuatiwa na honarable walkout!.

Mhe. Lissu baada ya kufika kando ya mto na kuyatazama tuu yale maji, akaamua hapa hatuwezi kuvuka, na kuamua kurudi alikotoka, angepaswa kuingiza kwanza huo mguu na kuona kina cha maji.

Mpaka sasa, hoja yangu ya msingi, haijajibiwa, kwanini Chadema hawakutoa pingamizi kwa muswada ule kwa mujibu wa kanuni?.

Kwanini badala ya kutoa pingamizi, wao ndio kwanza wakatoa go ahead ya majadiliano kuendelea kwa hotuba yao?.

Hivi nikisema kumbe waliotuangusha pale bungeni kwa kuruhusu muswada ule upite kiurahisi vile ndio wenzetu hawa

@Pasco, kitu ambacho sielewi na wewe bado hujaeleza ni kwa vipi CHADEMA wangesimama na kutumia hicho kifungu cha 86 (kwa uzima) automatically mjadala ukasitishwa! Nauliza hiyo kwa sababy ili hii theory yako isimame unatakiwa ueleze with certaintity kwamba mbunge ansimama anasoma kifungu and the debate is shelved! Hilo tu!
 
mkuu PASCO!
kuna mahali uli'comment kuwa ulishawahi kuonana na RA na akakueleza wazi kuwa yeye ndo alimuweka SS na ndiye aliyemtoa na kumuweka Anna makinda kuwa spika, kwa mazingira hayo hayo sioni ni kwanini unaamini unaamini kifungu cha kanuni ya 86 kingefuatwa kihalali (nasema kihalali maana inawezekana kikafuatwa isivyo kihalali) na hivyo mswada kutosomwa mara ya pili, iweje leo mtu aliyewekwa kwenye uspika na fisadi aache kufuata kanuni na masharti ya fisadi huyo? (note: RA na CCM ndo mafisadi)
 
Back
Top Bottom