Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!


Wanabodi, baada ya taarifa hii, haswa hoja number 1

  1. Kamati Kuu imewapongeza wabunge wote wa CHADEMA kwa hatua thabiti na sahihi walizochukua, kwa niaba ya wananchi wa Tanzania, kupinga Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 kusomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa Bungeni bila ya wananchi kushirikishwa kwa ukamilifu kutoa maoni yao na muswada kuboreshwa kwa kuzingatia muafaka wa kitaifa. Kamati Kuu imewapongeza wabunge wa CHADEMA na wale NCCR Mageuzi kwa kususia vikao vya Bunge vilivyojadili na kupitisha Sheria hiyo kwani kushiriki kwao kungeipa uhalali wa kisiasa na kijamii Sheria ambayo haikuzingatia nia na haja ya dhati ya kuweka utaratibu wa kisheria utakaoiwezesha nchi yetu kupata Katiba Mpya yenye kuzingatia na kukidhi matakwa ya umma wa Watanzania
Kwa vile hoja kuu ya msingi ya mada yangu ni kuwa Chadema, haukuupinga muswada ule, taarifa ya M/Kiti anapongeza kwa kuupinga, nawaombeni kwa heshma na taadhima, sasa tusitishe huu mjadala kama heshima kwa viongozi wetu wa wakuu wa vyama.

Naomba sasa kukubali kuwa Chadema Waliupinga ili yaishe, walionielewa mmenielewa, msio nielewa samanini sana!.

Pasco
.
 
Mwana JFs Pasco, itakubidi umtafute Mh P Chana, Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Katiba..., ili akupe ufafanuzi jinsi kamati yake ilivyopitisha.., muswada ya ile sheria kabla ya kusomwa kwa mara ya pili..,
nadhani utakuwa ktk wakati mzuri wa kuizungumzia hoja yako hapa...!

Mjumbe wa hiyo kamati Mh Lissu aliwahi kulizungumzia ktk kipindi cha BBC jinsi Govt na CCM, kupitia Speaker Mlegevu wa Bunge letu alivyoingilia uhuru wa kamati ya Sheria na Katiba...!
CDM walikwisha liona hilo toka ndani ya Kamati ya Sheria na Katiba jinsi CCM na Govt walivyotumia kutumia ubabe wa kuiteka nyara na kuifanya watakavyo ktk hiyo sheria....,

Pasco nadhani hata ww utakumbuka sana Mh Chana, nadhani aliitwa DR... cyo chini ya mara 3, pale ktk ule mkutano wa wazee wa CCM Dar, alitajwa na kusifiwa kwa kazi yake iliyotukuka ktk ule mchakato wa muswada ya wa hiyo sheria....!

 

Pasco si kwamba nimeita ligi kwa unazi tu. Hapana. Mm nimesema baada ya kuona wewe bado hutaki kukubali baada ya kuwekwa mifano hai hapa kwa jinsi gani hicho kifungu 86 kisingeweza kuokoa.

Hivi ikiwa cuf tu wameukubali muswada je ulitegemea ccm waungane na cdm? Maana kifungu kingetumika ni wazi kura ingepigwa kuwa wangapi wanakubali na wangapi wanakataa na ni wazi hapo kwa wingi wa ccm muswada wao ungepita tu.

Najua tayari muswada umekua sheria na hata mimi na wale wote wenye mapenzi mema na nchi wanaumizwa kwa hilo lakini tambua uwepo wa sheria haiwi halali kama imekiuka haki za msingi bado watanzania kwa umoja wetu tunayo nafasi ya kusema NO.

Kuhusu 2015 cdm kulia hapo niseme tu kwamba bila kudai haki inayokandamizwa ccm haitatoka madarakani hata kama watashindwa uchaguzi na huu muswada wao utakaoleta katiba mbovu ni moja ya mkakati wa kufanikisha hilo hivyo ni msimamo wa cdm na sisi wananchi kwa ujumla ndio utaamua hiyo 2015.
 

Nahisi kama umehamishia baraza la kumattach Lisu personally kutoka Bungeni kuja JF, tofauti yako na wabunge wa CCM na CUF
ni kwamba unamuattach kiakili zaidi. Na naona kama kinachokusukuma kufanya hivyo ni Lissu, Mwanasheria Mwenzako kusemwa
kwamba ni talented, gifted genious lawyer kama wewe mwenyewe unavyosema huku ukiumia.
 

Pasco, again, Spika would have none of that. Hakutaka hata kusikiliza Mnyika, Machali wanasema nini. And now we know why, maana kwa mchango wako huko nyuma huyu mama amewekwa kwenye hicho kiti kwa kazi maalum za wakubwa. Kwa CHADEMA kuendelea kubishana naye huyu mama kwa kutumia vifungu ambavyo 'mawani yake' inavifanya viwe giza ni kujichosha.

Kwenye red: Ni rahisi kusema CHADEMA hawajapata chochote, rahisi sana. But step back and reflect! Na hapa nataka nikukumbushe point yako kwenye hii hii thread pale uliposema kuwa CHADEMA walitukoka bungeni mwezi January kwa sababu hawakumtambua Rais. Nilidhani ililkuwa ni oversight toka kwako lakini nahisi ni kutokana na namna unavyonga'mua mambo.

1. Tuanze na mwezi January: CHADEMA hawakutoka kwa sababu hawamtambui rais, ila walitoka kwa sababu hawakuitambua 'PROCESS' iliyotumika kumpata rais. - Majumuisho ya kura yalikuwa upside down. Na unajua vema kuwa kwa katiba ya sasa rais akishatangazwa ni basi, huwezi kufanya chochote. Hivyo kama process ni mbovu na hakuna nguvu ya kuzia tutaendelea kupewa rais na sio kuchagua rais. Huu ndio msingi wa CHADEMA kutaka katiba mpya, katiba inayotoa haki, katiba inayotaka tume huru ya uchaguzi, katiba inayowapa wananchi nguvu ya kurekebisha mambo na hata matokeo ya uchaguzi yakiwa na utata basi kuwepo na option ya kwenda mahakaani.

2. Kama CHADEMA hawakutoka bungenni na kuendelea kupiga kelele (nje ya bunge) unaweza kusema kwa hakika kuwa leo tungekuwa tunaongea juu ya muswada wa katiba mpya? CCM hawakuwa na hiki kitu kwenye manifesto yao na hata pale CHADEMA walipoanza kusema mwanasheria mkuu na waziri wa sheria wote walisema NO. Matokeo ya kususia tunayaona.

3. CCM wanajua nini madhara ya katiba ya 'wananchi'. Wanajua itawaondelea (ccm) nguvu ya kumpata rais kupitia NEC. Na hapa ndio Makinda nahisi ameepewa maagizo maalum piga ua muswada upite. She is a shareholder (not a stakeholder) kwenye huu muswada.

4. Kutoka nje ya bunge kunawapa CHADEMA moral authority ya kusema 'hili' jambo ni haramu. Na kwa mazingira ya sasa kuna kila dalili kwamba wananchi wanasema (nikope msemo wa Gergo Bush Jr) 'You are either with us or against us'. CHADEMA kutoka nje wanaonekana kusema 'we are with you' na wale walio bakia ndani it does not matter walikuwa na maelfu ya kurasa ngapi za mapendezo, kwa wananchi ni kwamba wamesema 'we are agaisnt you'. Na kama una-doubt hii angalia shida waliyonayo CUF- Tanzania bara (sio Zanzibar) kwa sasa. Wanatumia muda mwingi hawa CUF kujibu hoja za serikali ya CCM na kueleza ilikuwaje wakabaki ndani. Ni vigumu mno kwa CUF huku bara kuaminisha watu kuwa ule muswada una kasoro maana walikuwa na opportunity to draw a line in the sand but they chose otherwise.

Na iko siku isiyo na jina CUF Tanzania bara wataachana kabisa na CUF Zanzibar kutokana na siasa za pande hizi mbili kuwa tofauti. Kule Zanzibar hawana shida maana walishaamua hakuna upinzani, ni siasa za kombolela tu ndio zinatumika lakini mwisho wa uchaguzi they all go through. Mshindi wa pili anakuwa makamo wa kwanza wa rais - daylight briebery but it is what it is na kwa maneno ya Mnyaa ni maamuzi ya wanzanzibar tunatakiwa tuyaheshimu.

5. Kutoka nje kwa CHADEMA kunafanya watu waanze kujadili huu muswada. Kikao cha bunge kimejadili mambo mengi na hata report ya Jairo imesomwa lakini discussion huku mtaani ni kuhusu huu muswada! Na mbaya sana watu wengi watausoma tofauti kama CHADEMA wangeamua kuchuana kwa kutumia vifungu, na watagundua madudu yote yaliyojificha. Nani anakumbuka muswada uliorihusu wakuu wa wilaaya/mikoa kusimamia nidhamu ya mahakama? Lissu alitumia vifungu lakini muswada ulipita.

Kwa kifupi, kuna wakati street politics zinakuwa more effective kuliko hizi za kukaaa kwenye viyoyozi.
 
Pingamizi alitaka kutoa Mnyika, Speaker akakataa, au kwako pingamizi mpaka atoe Lisu?

Nafikiri hili lilifafanuliwa na Spika. Kwani hoja au pingamizi alitakiwa Mnyika atoe taarifa kwa maneno au maandishi mapema kwa spika au ofisi ya spika kabla muswada kusomwa.

Mnyika alitaka kuweka pingamizi kabla kutoa notice kwa Spika na wakati muswada umeshaanza kusomwa. Hilo ni kinyume kwa kanuni za Bunge
lenu.
 
Pasco hajagundua Spika anaendeshaje bunge. Mambo ya kushika shilingi mara vifungi vya kuzuia hoja vyote vinaishia na kuhoji, mwisho ni wengi wape! Hatuna bunge!

Ngoja nikusaidie kidogo, ukienda kwenye "website" ya bunge, kuna sehemu unaweza kushusha "hansard" zote za Bungeni, sasa wewe ukieleza makosa ya bungeni hapa inabidi utuletee hiyo 'hansard", kama huwezi kufanya hivyo inakuwa huna mshiko wala cha maana bali ni kupinga kiushabiki na wala hujui unachokiandika.
 
Hatukubali yaishe mpaka hoja za msingi tulizopendekeza zijibiwe,wakati utaamua kama CHADEMA walikosea au la

Kwanza kwa sababu za kihistoria na zingine muswada unaweza kuendelea na kuwa sheria,lakini hiyo haimaanishi kwamba ni halali

Ustake ncheke, hebu tuwekee hapa hoja moja tuu ya maana mliyoitowa kuhusu mswaada uliopitishwa. Sijaiona.
 
  • What i always don't understand viongozi wa ccm na mwenyekiti wao jk ambaye ametokea kuwa rais wa tz ni kwamba wanapopata madaraka wanajisahau kwamba ccm inatawala nchi ya tz yenye watu zaidi ya 40mil. Tujiulize je, ccm inawakilishaje mawazo ya watanzania wote wakati hata huyo rais mwenyewe alipigiwa kura na watu wasiozidi 5mil?????je wanachama wa ccm nchi nzima ni wangapi????je iweje leo wakatae kusikia maoni ya watu wengine walioko nje ya chama chao????????,hata kama chadema ndio wangekuwa wanaongoza nchi lazima nao wangepaswa kusikiliza maoni ya pande zote nje wanachama wao (hata ccm wakiwemo).Hili suala mbona limekuwa gumu kueleweka kwa hawa ccm walioko madarakani????katiba jamani si ya chama bali ya nchi.......
  • Tujiulize waliopiga kura kwenye uchaguzi uliopita ukiwaunganisha vyama vyote walikuwa kiasi gani??????nadhani hawakuzidi hata 10mil. Sasa leo iweje tuangalie matakwa ya chama kwenye mchakato wa kuunda katiba na tusahau kundi kubwa la wananchi walioko nje ya vyama (hata ukiweka vyote pamoja).
  • Rais anasema yeye ana mamlaka kikatiba kuunda tume.......je yeye hayo mamlaka kapewa na nani????
  • Rais anasema hawezi kuweka marafiki zake????nani atathibitisha hili wakati tayari matatizo mengi yanayolikabili taifa yanatokana na tatizo la teuzi zake za marafiki kweye nafasi za uongozi???
  • Kura za maoni zitaratibiwa na tume ya uchaguzi???hili silielewi.....moja ya sababu za kilio cha kutaka katiba mpya ni tatizo sugu la tume ya uchaguzi ambayo imekuwa inateuliwa na huyo huyo rais....na imekuwa ikisaiia upande wa chama tawala mara zote pale wanpoonekana kupoteza kura.......kwa maana ya kujali maslahi ya ccm....sasa leo iweje hawa wapewe kazi ile ile ambayo wananchi wanalia kuwa hawaifanyi kwa haki??????
  • Ninapotafakari haya mambo.....sipati majibu ya kwanini haya mambo rais hawezi kuyaepusha ili watu wasipoteze muda kumtakia mabaya ambayo kwa hakika yatatokea kama hawa ccm hawajirekebishi......
  • Nilitegemea rais angetumia nguvu kubwa aliyonayo kikatiba kushughulika kuwaadhibu wezi na wabadhirifu wa mali za umma kama kina jairo, na rostam.....na wezi epa n.k kuliko kusema eti atasaini mswada wa sheria ya katiba et tena haraka!!!!!! afanye basi pia haraka kuwashughulikia majambazi waliogundulika juzi kwenye wizi wizara ya nishati na madinii akina jairo na li mamvi luhanjo......
 
yaweza kuwa pasco ametumwa kukusanya maoni toka kambi ya upinzani. Na si ajabu huwa hafuatilii mijadala inayofanyika katika bunge letu la bi kiroboto, ambaye hafanyi lolote nje ya maelekezo aliyopewa na waliojuu yake na waliomtuma.
 
Huu mjadala nimejifunza mengi sana sana na naona ndiyo umefikia mwisho.

Pasco, ungelikuwa Mwalimu basi ungelikuwa unawasha Debate kali sana darasani hadi wanafunzi wanataka kupigana. Sijui enzi zako kama kulikuwa na mtu anakushinda mara mkianza kubishana/debate darasani au kijiweni.

Huu si mjadala wa kwanza kuuweka hapa. Kila mjadala huwa unazusha majadiliano makubwa sana na hapo vifungu vya kanuni, sheria na katiba humwagika kwa wingi. Sijui kama unafanya makusudi ili kutusaidia na sisi wavivu wa kusoma sheria au kwa kweli huwa unabisha, ila ukweli ni kwamba wengi sana tumefaidika na makala hii.

Nawalaani wote waliokuja na kuporomosha matusi kwako na kuanza kukuita majina ya ajabu ajabu. Wanasahau kuwa ni ubishi/udadisi wako/ugumu wako ndiyo umesababisha tumeona mistari mingi namna hiyo. Kwa bahati mbaya sana, kuna wengine wamedandia gari lako kama kawaida ili kuanzisha ligi na Chadema ila nimefurahi kuwa watu wamewadharau hata kuwajibu wameacha. Hii makala ukiacha wapuuzi fulani wachache kutoka Chadema/CCM, kweli imeenda shule na kwa wale watakaotaka kukielewa hicho kifungu cha 86 cha kanuni, basi nafikiri hii makala imeelezea kwa undani sana. Kwa hilo Pasco kwa mara nyingine tena kutoka thread mbili tofauti nasema ASANTE SANA.

Wakati makala ikiendelea, nilikuwa nabadilisha mawazo na uamuzi kwa kuona uko sawa na mara nasoma jibu na kugundua haupo sawa. Baada ya kusoma hadi mwisho, kuna point moja muhimu sana umeandika kuwa "kama wangeliweka pingamizi na baadaye kufafanua HUENDA baadhi ya wana CCM wangeliwaunga mkono".

Tatizo ni hilo neno HUENDA, na wewe umerudi kulekule kwa Chadema. Umeangalia nini kingelitokea mbeleni na kukitumia bila kujua hasa matokeo yangelikuwa vipi. Chadema wanasema "Wao walijua pingamizi lao litakataliwa kwa kuangalia uzoefu" na wewe unasema "achana na uzoefu na weka pingamizi maana HUENDA akina Deo Filikunjombe watawaunga mkono." Sasa hapa mtabishana sana maana wote mnaangalia nini kitatokea mbeleni na ndiyo mnaamua nini mkifanye sasa. Sasa kati yenu, nani ni Sheick Yahya mzuri? Inakuwa vigumu sana kujua ingawa kuna msemo wa Kiswahili unasema "Alishaumwa na nyoka, akiona unyasi anashtuka" na wewe unakuja na kusema "wee endelea tu na safari, maana hata kama kweli unyasi huo ni nyoka, basi HUENDA nyoka huyo hana Sumu."

Nawashukuru wote waliochangia kama the real GREAT THINKERS wa JF na bila ushabiki wa chama chochote cha Kisiasa Tanzania. Namshukuru tena Pasco kwa majadala mzuri kama huu na wote waliojaribu kumjibu kwa kutumia njia mbalimbali ili kumuonyesha Pasco kuwa ameelewa vibaya. Pasco, nasubiri kwa hamu sana mjadala mwingine (wengine wameita ligi) ambao nina uhakika nao utawasha moto hapa JF huku wale Washabiki wa vyama wakiachwa kando bila watu kujali sana wameandika au wamesema nini. Ningelikuwa Mods, nakuwa napita na kuzifuta makala zao ili kupisha mtitiriko mzuri. NOYAGA!!
 

FaizaFoxy, bila kujigeuza kuwa mfanyakazi wako naomba nikuhakikishie I know what I am talking about. Muswada wa kuruhusu wakuu wa wilaya/mikoa kusimamia nidhamu ya mahakama ilikuwa ni makosa. Huwezi kuruhusu mhimili mmoja kuingilia kazi za mhimili mwingine hili ni kinyume kabisa na dhana ya separation of powers. Na ndio ilikuwa chimbuka la Lissu kupingwa, Zitto akasaidi lakini mwisho wa siku Spika alihoji wabunge wengi wakasema ndio sheria ikapita.
 
Pingamizi alitaka kutoa Mnyika, Speaker akakataa, au kwako pingamizi mpaka atoe Lisu?
Sangarara, nakuomba urudi tena ikaisome kanuni muda wa kuwasilisha pingamizi ni muda gani, pia inaelekeza ni stage gani mbunge anaweza kuleta pingamizi na ni stage gani there is nothing anybody can do, walitakiwa wote wafanye kabla ya hotuba ya TL, ile hotuba ndio go ahead sasa mjadala na uanze!. Kanuni inamuamuru speaker asipokee hoja yoyote kuruhusu muongozo wowote!. Hata huyo speaker ningekuwa mimi, kama hakuna pingamizi lolote lililowasilishwa, then miongozo ya nini?. Kama walikuwa na hoja, kwanini hawakuwasilisha pingamizi on the first place?!.
 
Kumjibu huyu mama, una ROHO ya Paka kwelikweli kama siyo ya Lowassa aka J. Zuma.
 
Hivi unajua athari za huo muswada au unapiga miayo tu!!
"tugange yapi yajayo wakati yameishaghoshiwa"
Unaonyesha wewe ni mtu wa kukata tamaa kwenye haya mapambano! huu siyo ushauri bali umetumwa!! wewe mtumwa!!
 
Pasco na wengine kabla hamjaondoka moja kwa moja hapa, mie nina swali (Narudia swali).

Katika maelezo yako, umeandika kuwa "Mjadala hauwezi kuendelea, kabla kiongozi wa kamba ya upinzani hajatoa maoni."

Mwanakijiji alikuuliza hivi :
"... kama kiongozi wa upinzani akija na kusema, SISI HATUNA MAONI, je ina maana mjadala huo ndiyo itabidi usimame kwa sababu tu upinzani hauna maoni?"

Hivi alitangulia KUKU au YAI? Swali la kizushi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…