Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
MAAMUZI YA KAMATI KUU YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA MPYA.


Kamati Kuu ya CHADEMA katika kikao chake maalum kilichofanyika siku ya Jumapili, tarehe 20 Novemba 2011 katika Ukumbi wa Hoteli ya Mbezi Garden, Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine, kimepokea na kujadili kwa kina taarifa ya majadiliano na kupitishwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011. Aidha, Kamati Kuu imejadili kwa kina hatua za kuchukua baada ya Serikali, kupitia wabunge wa CCM, kulazimisha kupitishwa bungeni kwa Sheria hiyo bila kuzingatia maoni ya Wananchi na wadau wengine mbalimbali. Baada ya kuyatafakari mambo haya kwa kina, Kamati Kuu imeazimia yafuatayo:
  1. Kamati Kuu imewapongeza wabunge wote wa CHADEMA kwa hatua thabiti na sahihi walizochukua, kwa niaba ya wananchi wa Tanzania, kupinga Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 kusomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa Bungeni bila ya wananchi kushirikishwa kwa ukamilifu kutoa maoni yao na muswada kuboreshwa kwa kuzingatia muafaka wa kitaifa. Kamati Kuu imewapongeza wabunge wa CHADEMA na wale NCCR Mageuzi kwa kususia vikao vya Bunge vilivyojadili na kupitisha Sheria hiyo kwani kushiriki kwao kungeipa uhalali wa kisiasa na kijamii Sheria ambayo haikuzingatia nia na haja ya dhati ya kuweka utaratibu wa kisheria utakaoiwezesha nchi yetu kupata Katiba Mpya yenye kuzingatia na kukidhi matakwa ya umma wa Watanzania;
  1. Kamati Kuu imezingatia kuwa Sheria iliyopitishwa na Bunge ina mapungufu mengi na ya kimsingi ambayo hayatajenga muafaka wa kitaifa juu ya Katiba Mpya na hayataleta mabadiliko yoyote ya kimsingi ya Katiba:
  1. Mchakato wa kuipitisha Sheria ndani ya Bunge ulikiuka Kanuni za Kudumu za Bunge kwani Muswada uliosomwa mara ya kwanza Bungeni sio ulioletwa Bungeni kusomwa mara ya pili na baadae kupitishwa; Kamati ilizuiliwa kukusanya maoni ya wananchi katika mikoa na maeneo mbali mbali; Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano aliingilia kazi na majukumu ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ikiwa ni pamoja na yeye mwenyewe na baadhi ya wajumbe wa CCM kukusanya maoni nje ya utaratibu wa Kamati na baadae kuingiza wajumbe wengine wa CCM na CUF kwa lengo la kupitisha matakwa ya CCM na Serikali ndani ya Kamati bila kuushirikisha wananchi kwa ukamilifu;
  1. Sheria inampa Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mamlaka makubwa ya kuunda Tume ya Katiba na Sekretarieti yake ambayo sio tu itakusanya maoni ya wananchi na kuandaa ripoti, bali pia ndiyo itakayoandaa na kuandika Rasimu ya Katiba Mpya na kusimamia mchakato wote wa wananchi kuijadili na kuipitisha katika Bunge la Katiba;
  1. Sheria inampa Rais na Mwenyekiti wa CCM mamlaka makubwa sio tu ya kupokea ripoti ya Tume ya Katiba bali pia ya kuifanyia mabadiliko ambayo yeye na Serikali yake wataona yanafaa kwa kutumia taratibu za kiserikali za kutunga sheria;
  1. Sheria inampa Rais na Mwenyekiti wa CCM mamlaka makubwa ya kuliitisha tena Bunge la Katiba kwa lengo la kufanya mabadiliko kwenye Katiba Mpya endapo litapitisha Katiba Mpya ambayo yeye Rais, au Serikali yake, au chama chake wataona hailindi maslahi yao;
  1. Sheria inaunda Bunge la Katiba ambalo litakuwa na Wajumbe hadi 400 wa CCM kati ya wajumbe 545 wa Bunge la Katiba. Idadi hii ya wajumbe itaiwezesha CCM kupata theluthi mbili ya wajumbe wanaohitajika chini ya Sheria hii ili kupitisha jambo lolote katika Bunge la Katiba na kwa hiyo Katiba Mpya itakuwa ni ile inayolingana na matakwa na maslahi ya CCM na itakuwa mpya kwa jina tu;
  1. Sheria inatoa nafasi kubwa kwa Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM na vyombo vya uwakilishi vya Zanzibar kushiriki kutunga Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano kinyume na Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 na Katiba ya sasa ambayo imevipa mamlaka ya kutunga Katiba ya Jamhuri ya Muungano vyombo vya Muungano kama Serikali na Bunge ambako Zanzibar ina uwakilishi wa kutosha;
  1. Sheria inahakikisha kwamba muundo wa sasa wa Muungano wa Serikali hautaguswa bali utadumishwa na kutiliwa nguvu licha ya madai ya miaka mingi ya wananchi na mapendekezo ya Tume za Kiserikali kwamba muundo wa Muungano uwe ni wa Serikali tatu;
  1. Sheria inaipa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyoteuliwa na Rais na Mwenyekiti wa CCM mamlaka ya kusimamia mchakato mzima wa kura ya maoni ya kuipa Katiba Mpya uhai wa kisheria. Tume ya Taifa ya Uchaguzi haina uhuru na imeshindwa mara nyingi kusimamia chaguzi huru na haki katika nchi yetu na haiwezi kusimamia kura ya maoni kwa uhuru unaohitajika;
  1. Kamati Kuu ya CHADEMA imesisitiza siku zote kwamba mchakato wa kupata Katiba Mpya unahitaji mwafaka wa kitaifa ambao utazingatia maoni mapana ya makundi mbalimbali ya kijamii. Kamati Kuu inasikitishwa na hatua za makusudi za kufifisha juhudi zote zilizofanyika na wadau mbalimbali katika kufikia mwafaka wa kitaifa juu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Aidha, Kamati Kuu imesikitishwa na upotoshaji wa makusudi wa hotuba ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni uliofanywa na wabunge wa CCM na CUF, wakiongozwa na Spika wa Bunge, Anna Makinda, kuhusu msimamo wa CHADEMA juu ya Muungano;
  2. Kamati Kuu inasisitiza kwamba njia pekee ya kuunusuru Muungano wetu ni kwa wananchi wa pande zote mbili kupiga kura ya maoni kuamua kwamba wanataka kuendelea na Muungano na kama jibu ni ndio, muundo gani wa Muungano huo wanaoutaka. Aidha, Kamati Kuu inarudia msimamo wa CHADEMA kwamba ili kuondoa kero na malalamiko ambayo yameuandama Muungano wetu tangu kuzaliwa kwake, muundo unaofaa ni wa Serikali tatu kama ilivyopendekezwa pia na Tume ya Nyalali mwaka 1991 na Tume ya Kisanga mwaka 1998;
  1. Kamati Kuu inaamini kuwa pamoja na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kupitishwa, bado kuna fursa za kisiasa na kijamii katika kujenga mwafaka wa kitaifa juu ya haja, nia, mchakato na misingi ya Katiba Mpya. Hata hivyo, Kamati Kuu imeshangazwa na kusikitishwa na uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete wa kutozitumia fursa hizo na badala yake kujiingiza katika jalala la taka za upotoshaji uliofanywa na Wabunge wa chama chake juu ya misingi na maudhui ya Sheria hiyo. Kamati Kuu inaamini kwamba badala ya kuwaunganisha Watanzania na kujenga muafaka unaohitajika katika mchakato wa Katiba Mpya, hotuba ya Rais Kikwete kwa wazee wa CCM wa Dar es Salaam imezidi kuwagawa Watanzania kwa misingi ya ushabiki wa vyama badala ya kuwaunganisha kwa misingi ya utaifa;
  1. Baada ya kutafakuri mambo yote haya, Kamati Kuu imeazimia yafuatayo:
  1. CHADEMA itaendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau wote juu ya ubovu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na juu ya haja ya kuwa na sheria itakayoweka utaratibu bora zaidi wa kuunda Tume Shirikishi ya Katiba kwa lengo la kukusanya maoni ya wananchi, kuandaa ripoti na Rasimu ya Katiba Mpya, Bunge Maalum la Katiba na usimamizi wa kura ya maoni itakayowezesha wananchi kufanya maamuzi kwa uhuru na kwa haki;
  1. Ushiriki wa CHADEMA katika mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya uliowekwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba utategemea utayari wa Serikali ya Rais Kikwete kufanya mabadiliko makubwa na ya kimsingi katika sheria hiyo kwa lengo la kujenga muafaka wa kitaifa juu ya mchakato huo;
  1. Kamati Kuu inawaagiza wabunge na viongozi wote wa chama katika ngazi zote kufanya mikutano ya ndani na ya hadhara yenye lengo la kuwaelimisha wananchi juu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na madhara yake kwa mchakato wa kupata Katiba Mpya na bora kwa nchi yetu kwa lengo la kuunganisha umma wa watanzania kuweza kufanya mabadiliko ya msingi;
  1. Kamati Kuu inaamini kwamba uamuzi wa Serikali ya CCM kulitumia Jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya hadhara na maandamano ya amani ya wananchi wanaopinga mchakato uliopitishwa kuwa Sheria sio tu ni kwenda kinyume na haki za kimsingi za kikatiba bali pia unahatarisha moja kwa moja amani, utulivu na umoja wa nchi yetu. Kamati Kuu inasikitishwa na msimamo huu wa Serikali ya CCM kwani unashindwa kutambua ukweli kuwa matumizi ya nguvu za dola hayajawahi kuokoa serikali za kidikteta kuondolewa madarakani na Katiba Mpya kupatikana katika nchi mbali mbali duniani na katika Bara la Afrika;
  1. Kamati Kuu inasisitiza kwamba CHADEMA itaendelea kutumia njia zote za amani, ikiwemo mikutano ya hadhara na maandamano kama ilivyoainishwa na Katiba na sheria husika za nchi yetu kuunganisha nguvu ya umma kupinga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na mchakato wake utakaopelekea Tanzania kutopata Katiba Mpya na bora;


Freeman A. Mbowe (MB)
MWENYEKITI WA TAIFA

Novemba 21, 2011

Wanabodi, baada ya taarifa hii, haswa hoja number 1

  1. Kamati Kuu imewapongeza wabunge wote wa CHADEMA kwa hatua thabiti na sahihi walizochukua, kwa niaba ya wananchi wa Tanzania, kupinga Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 kusomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa Bungeni bila ya wananchi kushirikishwa kwa ukamilifu kutoa maoni yao na muswada kuboreshwa kwa kuzingatia muafaka wa kitaifa. Kamati Kuu imewapongeza wabunge wa CHADEMA na wale NCCR Mageuzi kwa kususia vikao vya Bunge vilivyojadili na kupitisha Sheria hiyo kwani kushiriki kwao kungeipa uhalali wa kisiasa na kijamii Sheria ambayo haikuzingatia nia na haja ya dhati ya kuweka utaratibu wa kisheria utakaoiwezesha nchi yetu kupata Katiba Mpya yenye kuzingatia na kukidhi matakwa ya umma wa Watanzania
Kwa vile hoja kuu ya msingi ya mada yangu ni kuwa Chadema, haukuupinga muswada ule, taarifa ya M/Kiti anapongeza kwa kuupinga, nawaombeni kwa heshma na taadhima, sasa tusitishe huu mjadala kama heshima kwa viongozi wetu wa wakuu wa vyama.

Naomba sasa kukubali kuwa Chadema Waliupinga ili yaishe, walionielewa mmenielewa, msio nielewa samanini sana!.

Pasco
.
 
Mwana JFs Pasco, itakubidi umtafute Mh P Chana, Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Katiba..., ili akupe ufafanuzi jinsi kamati yake ilivyopitisha.., muswada ya ile sheria kabla ya kusomwa kwa mara ya pili..,
nadhani utakuwa ktk wakati mzuri wa kuizungumzia hoja yako hapa...!

Mjumbe wa hiyo kamati Mh Lissu aliwahi kulizungumzia ktk kipindi cha BBC jinsi Govt na CCM, kupitia Speaker Mlegevu wa Bunge letu alivyoingilia uhuru wa kamati ya Sheria na Katiba...!
CDM walikwisha liona hilo toka ndani ya Kamati ya Sheria na Katiba jinsi CCM na Govt walivyotumia kutumia ubabe wa kuiteka nyara na kuifanya watakavyo ktk hiyo sheria....,

Pasco nadhani hata ww utakumbuka sana Mh Chana, nadhani aliitwa DR... cyo chini ya mara 3, pale ktk ule mkutano wa wazee wa CCM Dar, alitajwa na kusifiwa kwa kazi yake iliyotukuka ktk ule mchakato wa muswada ya wa hiyo sheria....!

 
Mpatanishi, sio kweli napenda ligi, nimetoa hoja tatu za msingi, naona mnang'ang'ania moja. Nimesema Chadema walikosea, nikashauri kwanza wakubali makosa, kukubali makosa ni sawa na kuomba radhi, na mwisho nikashauri, wakubali yaishe, wawaambie wanachama na wapenzi wao wasonge mbele!.

Sheria imepitishwa, sasa kwa kususa, walichokipata ni kipi?, sheria ikishainiwa hii ni habari nyingine, hakuna tena chochote mnachoweza kufanya, sio Chadema, si wanaharakati!

Tatizo la baadhi ya manazi wa Chadema, wanaamini Chama chao ni chama kitakatifu na viongozi wake ni watakatifu hawawezi kufanya makosa!.

Mimi kama mwana jf nisiiegemea upande wowote, naelewa fika ukosoaji wa Chadema humu jamvini jinsi unavyoshukiwa.

Mimi naendelea kusimama na ukweli ninauamini, kama utaita ligi, ita tuu, watakaosema nimetumwa na waseme tuu, ila mwisha wa siku, wale wenye kuubali ukweli mchungu, mtanielewa baada ya 2015, tutakapo kuja tena humu humu tunalia lia!.

Pasco si kwamba nimeita ligi kwa unazi tu. Hapana. Mm nimesema baada ya kuona wewe bado hutaki kukubali baada ya kuwekwa mifano hai hapa kwa jinsi gani hicho kifungu 86 kisingeweza kuokoa.

Hivi ikiwa cuf tu wameukubali muswada je ulitegemea ccm waungane na cdm? Maana kifungu kingetumika ni wazi kura ingepigwa kuwa wangapi wanakubali na wangapi wanakataa na ni wazi hapo kwa wingi wa ccm muswada wao ungepita tu.

Najua tayari muswada umekua sheria na hata mimi na wale wote wenye mapenzi mema na nchi wanaumizwa kwa hilo lakini tambua uwepo wa sheria haiwi halali kama imekiuka haki za msingi bado watanzania kwa umoja wetu tunayo nafasi ya kusema NO.

Kuhusu 2015 cdm kulia hapo niseme tu kwamba bila kudai haki inayokandamizwa ccm haitatoka madarakani hata kama watashindwa uchaguzi na huu muswada wao utakaoleta katiba mbovu ni moja ya mkakati wa kufanikisha hilo hivyo ni msimamo wa cdm na sisi wananchi kwa ujumla ndio utaamua hiyo 2015.
 
Asante Politiki, nitamjibu Mzee Mwanakijiji yeye bado anajenga hoja kwenye presumpmtion ambayo ndio utopia politics, kama maandiko yanasema "tafuteni mtapata", " ombeni mtapewa" au " bisha hodi utafunguliwa!", kama msipotafuta, hampati!, msipoomba hampewi', na msipo bisha hodi, hamfunguliwi!. Kuna kitu Mhe. Tundu Lissu alipashwa kufanya, hakutimiza wajibu wake!, as a result Chadema lost the argument for good!, sasa huu utetezi wa Mzee Mwanakijiji eti hata kama wangeli ... wasingeli kubaliwa!, doesn't hold water!.
Miongoni mwa sheria ambazo mimi nimespecialize ni International Law na Private International Law ambazo zinasisitiza lazima u exohaust existing home remedies ndipo uingie kwenye international law, Mhe. Lissu had a chance hakuitumia!. There must be credible reasons ambazo ni justified kwa why not hizo sababu za Mzee Mwanakijiji ni scapegoat tuu na ni superficial tuu, hakuna sababu zozote za maana zaidi ya uzembe!.

Assumption yangu Chadema banked on Lissu talented gifted genious lawyer!. Ku addmit weakness au kukubali makosa, kwataka moyo!. This time Chadema was wrong!.

Nahisi kama umehamishia baraza la kumattach Lisu personally kutoka Bungeni kuja JF, tofauti yako na wabunge wa CCM na CUF
ni kwamba unamuattach kiakili zaidi. Na naona kama kinachokusukuma kufanya hivyo ni Lissu, Mwanasheria Mwenzako kusemwa
kwamba ni talented, gifted genious lawyer kama wewe mwenyewe unavyosema huku ukiumia.
 
FJM, nimeuliza swali, na nitaelea kuliuliza mpaka kesho na kesho kutwa, kwanini Chadema hawakuwasilisha pingamizi la muswada ule kwa mujibu wa kanuni?.

The rest ni immaterial, eti kwa vile spika atalihoji bunge, ndio sababu msiwasilishe pingamizi?. Pia nimeuliza sheria imepita, Chadema wamepata nini?, nothing!. Washabiki wenu humu wanataka kuwahamasisha muisusie na tume ya kukusanya maoni!, mtapata nini?. Ila pia nakubali ule msemo wa 'zimwi likujualo' labda mnaona inafaa katiba hii hii iendelee, mkisusia mchakato, ua mkipiga kura ya hapana, katiba iliyopo itaendelea!

Pasco, again, Spika would have none of that. Hakutaka hata kusikiliza Mnyika, Machali wanasema nini. And now we know why, maana kwa mchango wako huko nyuma huyu mama amewekwa kwenye hicho kiti kwa kazi maalum za wakubwa. Kwa CHADEMA kuendelea kubishana naye huyu mama kwa kutumia vifungu ambavyo 'mawani yake' inavifanya viwe giza ni kujichosha.

Kwenye red: Ni rahisi kusema CHADEMA hawajapata chochote, rahisi sana. But step back and reflect! Na hapa nataka nikukumbushe point yako kwenye hii hii thread pale uliposema kuwa CHADEMA walitukoka bungeni mwezi January kwa sababu hawakumtambua Rais. Nilidhani ililkuwa ni oversight toka kwako lakini nahisi ni kutokana na namna unavyonga'mua mambo.

1. Tuanze na mwezi January: CHADEMA hawakutoka kwa sababu hawamtambui rais, ila walitoka kwa sababu hawakuitambua 'PROCESS' iliyotumika kumpata rais. - Majumuisho ya kura yalikuwa upside down. Na unajua vema kuwa kwa katiba ya sasa rais akishatangazwa ni basi, huwezi kufanya chochote. Hivyo kama process ni mbovu na hakuna nguvu ya kuzia tutaendelea kupewa rais na sio kuchagua rais. Huu ndio msingi wa CHADEMA kutaka katiba mpya, katiba inayotoa haki, katiba inayotaka tume huru ya uchaguzi, katiba inayowapa wananchi nguvu ya kurekebisha mambo na hata matokeo ya uchaguzi yakiwa na utata basi kuwepo na option ya kwenda mahakaani.

2. Kama CHADEMA hawakutoka bungenni na kuendelea kupiga kelele (nje ya bunge) unaweza kusema kwa hakika kuwa leo tungekuwa tunaongea juu ya muswada wa katiba mpya? CCM hawakuwa na hiki kitu kwenye manifesto yao na hata pale CHADEMA walipoanza kusema mwanasheria mkuu na waziri wa sheria wote walisema NO. Matokeo ya kususia tunayaona.

3. CCM wanajua nini madhara ya katiba ya 'wananchi'. Wanajua itawaondelea (ccm) nguvu ya kumpata rais kupitia NEC. Na hapa ndio Makinda nahisi ameepewa maagizo maalum piga ua muswada upite. She is a shareholder (not a stakeholder) kwenye huu muswada.

4. Kutoka nje ya bunge kunawapa CHADEMA moral authority ya kusema 'hili' jambo ni haramu. Na kwa mazingira ya sasa kuna kila dalili kwamba wananchi wanasema (nikope msemo wa Gergo Bush Jr) 'You are either with us or against us'. CHADEMA kutoka nje wanaonekana kusema 'we are with you' na wale walio bakia ndani it does not matter walikuwa na maelfu ya kurasa ngapi za mapendezo, kwa wananchi ni kwamba wamesema 'we are agaisnt you'. Na kama una-doubt hii angalia shida waliyonayo CUF- Tanzania bara (sio Zanzibar) kwa sasa. Wanatumia muda mwingi hawa CUF kujibu hoja za serikali ya CCM na kueleza ilikuwaje wakabaki ndani. Ni vigumu mno kwa CUF huku bara kuaminisha watu kuwa ule muswada una kasoro maana walikuwa na opportunity to draw a line in the sand but they chose otherwise.

Na iko siku isiyo na jina CUF Tanzania bara wataachana kabisa na CUF Zanzibar kutokana na siasa za pande hizi mbili kuwa tofauti. Kule Zanzibar hawana shida maana walishaamua hakuna upinzani, ni siasa za kombolela tu ndio zinatumika lakini mwisho wa uchaguzi they all go through. Mshindi wa pili anakuwa makamo wa kwanza wa rais - daylight briebery but it is what it is na kwa maneno ya Mnyaa ni maamuzi ya wanzanzibar tunatakiwa tuyaheshimu.

5. Kutoka nje kwa CHADEMA kunafanya watu waanze kujadili huu muswada. Kikao cha bunge kimejadili mambo mengi na hata report ya Jairo imesomwa lakini discussion huku mtaani ni kuhusu huu muswada! Na mbaya sana watu wengi watausoma tofauti kama CHADEMA wangeamua kuchuana kwa kutumia vifungu, na watagundua madudu yote yaliyojificha. Nani anakumbuka muswada uliorihusu wakuu wa wilaaya/mikoa kusimamia nidhamu ya mahakama? Lissu alitumia vifungu lakini muswada ulipita.

Kwa kifupi, kuna wakati street politics zinakuwa more effective kuliko hizi za kukaaa kwenye viyoyozi.
 
Pingamizi alitaka kutoa Mnyika, Speaker akakataa, au kwako pingamizi mpaka atoe Lisu?

Nafikiri hili lilifafanuliwa na Spika. Kwani hoja au pingamizi alitakiwa Mnyika atoe taarifa kwa maneno au maandishi mapema kwa spika au ofisi ya spika kabla muswada kusomwa.

Mnyika alitaka kuweka pingamizi kabla kutoa notice kwa Spika na wakati muswada umeshaanza kusomwa. Hilo ni kinyume kwa kanuni za Bunge
lenu.
 
Pasco hajagundua Spika anaendeshaje bunge. Mambo ya kushika shilingi mara vifungi vya kuzuia hoja vyote vinaishia na kuhoji, mwisho ni wengi wape! Hatuna bunge!

Ngoja nikusaidie kidogo, ukienda kwenye "website" ya bunge, kuna sehemu unaweza kushusha "hansard" zote za Bungeni, sasa wewe ukieleza makosa ya bungeni hapa inabidi utuletee hiyo 'hansard", kama huwezi kufanya hivyo inakuwa huna mshiko wala cha maana bali ni kupinga kiushabiki na wala hujui unachokiandika.
 
Hatukubali yaishe mpaka hoja za msingi tulizopendekeza zijibiwe,wakati utaamua kama CHADEMA walikosea au la

Kwanza kwa sababu za kihistoria na zingine muswada unaweza kuendelea na kuwa sheria,lakini hiyo haimaanishi kwamba ni halali

Ustake ncheke, hebu tuwekee hapa hoja moja tuu ya maana mliyoitowa kuhusu mswaada uliopitishwa. Sijaiona.
 
Huna hoja? Unanchekesha.


Cheti za ndoa nje nje wanaume wanapombatiana ....Kameruni ametushika pabaya


GO9G4032.jpg
 
  • What i always don't understand viongozi wa ccm na mwenyekiti wao jk ambaye ametokea kuwa rais wa tz ni kwamba wanapopata madaraka wanajisahau kwamba ccm inatawala nchi ya tz yenye watu zaidi ya 40mil. Tujiulize je, ccm inawakilishaje mawazo ya watanzania wote wakati hata huyo rais mwenyewe alipigiwa kura na watu wasiozidi 5mil?????je wanachama wa ccm nchi nzima ni wangapi????je iweje leo wakatae kusikia maoni ya watu wengine walioko nje ya chama chao????????,hata kama chadema ndio wangekuwa wanaongoza nchi lazima nao wangepaswa kusikiliza maoni ya pande zote nje wanachama wao (hata ccm wakiwemo).Hili suala mbona limekuwa gumu kueleweka kwa hawa ccm walioko madarakani????katiba jamani si ya chama bali ya nchi.......
  • Tujiulize waliopiga kura kwenye uchaguzi uliopita ukiwaunganisha vyama vyote walikuwa kiasi gani??????nadhani hawakuzidi hata 10mil. Sasa leo iweje tuangalie matakwa ya chama kwenye mchakato wa kuunda katiba na tusahau kundi kubwa la wananchi walioko nje ya vyama (hata ukiweka vyote pamoja).
  • Rais anasema yeye ana mamlaka kikatiba kuunda tume.......je yeye hayo mamlaka kapewa na nani????
  • Rais anasema hawezi kuweka marafiki zake????nani atathibitisha hili wakati tayari matatizo mengi yanayolikabili taifa yanatokana na tatizo la teuzi zake za marafiki kweye nafasi za uongozi???
  • Kura za maoni zitaratibiwa na tume ya uchaguzi???hili silielewi.....moja ya sababu za kilio cha kutaka katiba mpya ni tatizo sugu la tume ya uchaguzi ambayo imekuwa inateuliwa na huyo huyo rais....na imekuwa ikisaiia upande wa chama tawala mara zote pale wanpoonekana kupoteza kura.......kwa maana ya kujali maslahi ya ccm....sasa leo iweje hawa wapewe kazi ile ile ambayo wananchi wanalia kuwa hawaifanyi kwa haki??????
  • Ninapotafakari haya mambo.....sipati majibu ya kwanini haya mambo rais hawezi kuyaepusha ili watu wasipoteze muda kumtakia mabaya ambayo kwa hakika yatatokea kama hawa ccm hawajirekebishi......
  • Nilitegemea rais angetumia nguvu kubwa aliyonayo kikatiba kushughulika kuwaadhibu wezi na wabadhirifu wa mali za umma kama kina jairo, na rostam.....na wezi epa n.k kuliko kusema eti atasaini mswada wa sheria ya katiba et tena haraka!!!!!! afanye basi pia haraka kuwashughulikia majambazi waliogundulika juzi kwenye wizi wizara ya nishati na madinii akina jairo na li mamvi luhanjo......
 
yaweza kuwa pasco ametumwa kukusanya maoni toka kambi ya upinzani. Na si ajabu huwa hafuatilii mijadala inayofanyika katika bunge letu la bi kiroboto, ambaye hafanyi lolote nje ya maelekezo aliyopewa na waliojuu yake na waliomtuma.
 
Huu mjadala nimejifunza mengi sana sana na naona ndiyo umefikia mwisho.

Pasco, ungelikuwa Mwalimu basi ungelikuwa unawasha Debate kali sana darasani hadi wanafunzi wanataka kupigana. Sijui enzi zako kama kulikuwa na mtu anakushinda mara mkianza kubishana/debate darasani au kijiweni.

Huu si mjadala wa kwanza kuuweka hapa. Kila mjadala huwa unazusha majadiliano makubwa sana na hapo vifungu vya kanuni, sheria na katiba humwagika kwa wingi. Sijui kama unafanya makusudi ili kutusaidia na sisi wavivu wa kusoma sheria au kwa kweli huwa unabisha, ila ukweli ni kwamba wengi sana tumefaidika na makala hii.

Nawalaani wote waliokuja na kuporomosha matusi kwako na kuanza kukuita majina ya ajabu ajabu. Wanasahau kuwa ni ubishi/udadisi wako/ugumu wako ndiyo umesababisha tumeona mistari mingi namna hiyo. Kwa bahati mbaya sana, kuna wengine wamedandia gari lako kama kawaida ili kuanzisha ligi na Chadema ila nimefurahi kuwa watu wamewadharau hata kuwajibu wameacha. Hii makala ukiacha wapuuzi fulani wachache kutoka Chadema/CCM, kweli imeenda shule na kwa wale watakaotaka kukielewa hicho kifungu cha 86 cha kanuni, basi nafikiri hii makala imeelezea kwa undani sana. Kwa hilo Pasco kwa mara nyingine tena kutoka thread mbili tofauti nasema ASANTE SANA.

Wakati makala ikiendelea, nilikuwa nabadilisha mawazo na uamuzi kwa kuona uko sawa na mara nasoma jibu na kugundua haupo sawa. Baada ya kusoma hadi mwisho, kuna point moja muhimu sana umeandika kuwa "kama wangeliweka pingamizi na baadaye kufafanua HUENDA baadhi ya wana CCM wangeliwaunga mkono".

Tatizo ni hilo neno HUENDA, na wewe umerudi kulekule kwa Chadema. Umeangalia nini kingelitokea mbeleni na kukitumia bila kujua hasa matokeo yangelikuwa vipi. Chadema wanasema "Wao walijua pingamizi lao litakataliwa kwa kuangalia uzoefu" na wewe unasema "achana na uzoefu na weka pingamizi maana HUENDA akina Deo Filikunjombe watawaunga mkono." Sasa hapa mtabishana sana maana wote mnaangalia nini kitatokea mbeleni na ndiyo mnaamua nini mkifanye sasa. Sasa kati yenu, nani ni Sheick Yahya mzuri? Inakuwa vigumu sana kujua ingawa kuna msemo wa Kiswahili unasema "Alishaumwa na nyoka, akiona unyasi anashtuka" na wewe unakuja na kusema "wee endelea tu na safari, maana hata kama kweli unyasi huo ni nyoka, basi HUENDA nyoka huyo hana Sumu."

Nawashukuru wote waliochangia kama the real GREAT THINKERS wa JF na bila ushabiki wa chama chochote cha Kisiasa Tanzania. Namshukuru tena Pasco kwa majadala mzuri kama huu na wote waliojaribu kumjibu kwa kutumia njia mbalimbali ili kumuonyesha Pasco kuwa ameelewa vibaya. Pasco, nasubiri kwa hamu sana mjadala mwingine (wengine wameita ligi) ambao nina uhakika nao utawasha moto hapa JF huku wale Washabiki wa vyama wakiachwa kando bila watu kujali sana wameandika au wamesema nini. Ningelikuwa Mods, nakuwa napita na kuzifuta makala zao ili kupisha mtitiriko mzuri. NOYAGA!!
 
Ngoja nikusaidie kidogo, ukienda kwenye "website" ya bunge, kuna sehemu unaweza kushusha "hansard" zote za Bungeni, sasa wewe ukieleza makosa ya bungeni hapa inabidi utuletee hiyo 'hansard", kama huwezi kufanya hivyo inakuwa huna mshiko wala cha maana bali ni kupinga kiushabiki na wala hujui unachokiandika.

FaizaFoxy, bila kujigeuza kuwa mfanyakazi wako naomba nikuhakikishie I know what I am talking about. Muswada wa kuruhusu wakuu wa wilaya/mikoa kusimamia nidhamu ya mahakama ilikuwa ni makosa. Huwezi kuruhusu mhimili mmoja kuingilia kazi za mhimili mwingine hili ni kinyume kabisa na dhana ya separation of powers. Na ndio ilikuwa chimbuka la Lissu kupingwa, Zitto akasaidi lakini mwisho wa siku Spika alihoji wabunge wengi wakasema ndio sheria ikapita.
 
Pingamizi alitaka kutoa Mnyika, Speaker akakataa, au kwako pingamizi mpaka atoe Lisu?
Sangarara, nakuomba urudi tena ikaisome kanuni muda wa kuwasilisha pingamizi ni muda gani, pia inaelekeza ni stage gani mbunge anaweza kuleta pingamizi na ni stage gani there is nothing anybody can do, walitakiwa wote wafanye kabla ya hotuba ya TL, ile hotuba ndio go ahead sasa mjadala na uanze!. Kanuni inamuamuru speaker asipokee hoja yoyote kuruhusu muongozo wowote!. Hata huyo speaker ningekuwa mimi, kama hakuna pingamizi lolote lililowasilishwa, then miongozo ya nini?. Kama walikuwa na hoja, kwanini hawakuwasilisha pingamizi on the first place?!.
 
Kumjibu huyu mama, una ROHO ya Paka kwelikweli kama siyo ya Lowassa aka J. Zuma.
FaizaFoxy, bila kujigeuza kuwa mfanyakazi wako naomba nikuhakikishie I know what I am talking about. Muswada wa kuruhusu wakuu wa wilaya/mikoa kusimamia nidhamu ya mahakama ilikuwa ni makosa. Huwezi kuruhusu mhimili mmoja kuingilia kazi za mhimili mwingine hili ni kinyume kabisa na dhana ya separation of powers. Na ndio ilikuwa chimbuka la Lissu kupingwa, Zitto akasaidi lakini mwisho wa siku Spika alihoji wabunge wengi wakasema ndio sheria ikapita.
 
Wanabodi,
Kanuni ya Kuu ya Kwanza kwa mwanahabari yoyote ni to tell nothing but the truth. Naomba kuitumia kanuni hii kuwaambia Chadema, they were wrong!, walikosea!, kwanza wakiri makosa, pili wakubali yaishe na mwisho wasonge mbele, 2015 sio mbali kihivyo!.

Mchelea mwana kulia, hulia yeye, japo binafsi sio mshabiki wa chama chochote cha siasa bali ni mkereketwa wa demokrasia ya kweli ndani ya bunge, hivyo wapenzi wote wa dhati wa demokrasia, lazima waikubali Chadema kama ndicho chama pekee cha upinzani Tanzania bara kilichoonyesha nuru ya matumaini ya uwezekano wa kupatikana kwa demokrasia ya kweli ndani ya bunge na labda hata ukombozi wa pili wa Mtanzania baada ya uhuru na miaka 50 ya utumwa wa chama kimoja kuhodhi madaraka yote ya dola.

Wengi wa wapenzi wa demokrasia wanaishabikia mno Chadema wakichelea kuiambia ukweli kuwa watalia, mimi nachelea mashabiki na wapenzi wao kulia mwaka 2015, hivyo nawaambia ukweli ili hata kama mtalia, lakini itakumbukwa mliambiwa!.

Suala la kususia jumla mchakato wa kuunda tume ya kukusanya maoni kuunda katiba mpya ni kosa kwa sababu Chadema kama kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ilikuwa na uwezo wa kuusimamisha na kuzuia uwasilishwaji kwa mara ya pili huo muswada kwa kutumia kanuni ya kifungu 86 hivyo kutoa fursa ya hoja ya kuzuia uwasilishwaji huo kusikilizwa, lakini Chadema haikufanya hivyo.

Hakuna ubishi kuhusu uwezo wa wabunge wa Chadema katika umakini, kitendo cha oversight ya opportunies provided by kifungu cha 86 cha kanuni za bunge kuuzuia huo muswada, sio tuu ni udhaifu mkubwa, but kosa kubwa ambalo Chadema lazima wakiri, waombe radhi na kusonga mbele.

Kanuni hiyo ya 86 inaeleza wazi hatua kwa hatua za kufuatwa ili kuuzuia muswada usisomwe kwa mara ya pili. Chadema ilipuuza na kuendelea kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani.

Kama Chadema ingezingatia kanuni hiyo, isinge wasilisha maoni ya kambi ya upinzani bali ingewasilisha pingamizi!.

Kitendo cha Mhe. Lissu kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani, yamemaanisha wameijibu hoja ya serikali hivyo kutoa go ahead majadiliano yaendelee. Uwasilishwaji wa hotuba hiyo ndio passport ya mjadala kuendelea, kama kambi ya upinzani wasingewasilisha maoni yao, muswada ungesitishwa kwanza na wao kusikilizwa. Hivyo iwasilishwaji wa hotuba ile ni kosa la pili, Chadema lazima wakiri kosa, waombe radhi na kusonga mbele!.

Kitendo cha kususia mjadala kwa siku ya kwanza na kutoka nje, was the right move kuonyesha protest dhidi ya unyanyasaji wa Mhe. Spika, lakini kuisusa hoja jumla, was a mistake hivyo sheria imetungwa bila imput yao, hivyo hili ni kosa la tatu, Chadema wakiri kosa, waombe radhi na kusonga mbele!.

Nimebahatika kuhudhuria mdahalo wa Star TV kuhusu Tanzania tuitakayo ambapo Mhe. Tindu Lissu ilikuwa ni mdahiliwa, na nilipata fursa ya kuuliza swali kuhusu kanuni ya 86 lililokuwa na vipengele a, b na c
(a) Kanini hawakitumia kanuni ya 86 kuuzuia muswada usisomwe?.
(b) Kwanini waliwasilisha hotuba ya maoni ya kambi ya upinzani yaliyotoa passport mjadala uendelee badala ya kuwasilisha pingamizi ambayo ingeusimamisha mjadala?.
(c) Chadema wamesusa sheria imepitishwa, jee wamefaidika na nini na kususa kwao?.

Mhe. Lissu amepiga chenga kutoa majibu ya kina kwa kujibu
(a). Amenisomea hitimisho la hotuba yake. Kanuni ya 86 ilimtaka Mhe. Lissu awasilishe pingamizi na sio hotuba!.
(b) Amepiga chenga kueleza ni kwanini amewasilisha hotuba badala ya pingamizi!.
(c) Wananchi wanaelewa ni nani mtetezi wao wa ukweli.

Kwa vile sheria imepitishwa na itasainiwa na rais kwa mbwembwe, lazima Chadema na wapenzi wao na mashabiki wao waukubali ukweli mchungu kuwa they lost the bettle hivyo watake wasitake, lazima wakubali matokeo. Hawawezi kuendelea kususa, lazima wajisibmit kwenye tume ya kuratibu maoni na kutoa maoni yao hata kama tume hiyo itaundwa bila imput yao na bila ridhaa yao!.

Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo (Tume ya kukusanya maoni) na yajayo (Katiba Mpya).

Namalizia kwa kusisitiza, kufanya kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa!. Chadema kwenye uundwaji tume mmefanya kosa!. Sheria imetungwa na sasa sio kosa tena, kosa ni kurudia kosa kama hamtoa maoni yenu kwenye tume!. Two wrongs don't make right, better late than never!.

2015 sio mbali kihivyo!.

Wasalaam
Pasco (wa jf).
Hivi unajua athari za huo muswada au unapiga miayo tu!!
"tugange yapi yajayo wakati yameishaghoshiwa"
Unaonyesha wewe ni mtu wa kukata tamaa kwenye haya mapambano! huu siyo ushauri bali umetumwa!! wewe mtumwa!!
 
Pasco na wengine kabla hamjaondoka moja kwa moja hapa, mie nina swali (Narudia swali).

Katika maelezo yako, umeandika kuwa "Mjadala hauwezi kuendelea, kabla kiongozi wa kamba ya upinzani hajatoa maoni."

Mwanakijiji alikuuliza hivi :
"... kama kiongozi wa upinzani akija na kusema, SISI HATUNA MAONI, je ina maana mjadala huo ndiyo itabidi usimame kwa sababu tu upinzani hauna maoni?"

Hivi alitangulia KUKU au YAI? Swali la kizushi.
 
Back
Top Bottom