Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Ahsante sana Nyanda kwa kipande hiki cha hotuba ya mh. Tundu Lisu. Bila shaka hakuna ubishi kwamba msemaji wa kambi ya upinzani alikitumia vizuri kifungu hicho isipokuwa spika ndiye alishindwa kutimiza wajibu wake.

Na ndio maana, Pasco alipomuuliza Lissu kwanini CHADEMA hakikupinga muswada, Lissu alimjibu aangalie hitimisho la hotuba yake.
 
Jee hivyo ndivyo kanuni inavyosema hivyo kuwa pingamizi litawasilishwa kwenye hotuba?.
Kwahiyo una maana Lissu hakufuata kanuni bali alitoa hotuba?

Binafsi nadhani hotuba yake ndiyo ilikuwa na maelezo kuwa ni kwanini hakufuata kanuni hizo za pingamizi.
 
Reactions: Nzi


Sasa angalau umekuja ambako tuliko sisi wengine.

a. Kuzuia mswada ule hakuhitaji wabunge wa upinzani.
b. Wabunge hao makini wa CCM kama kweli wako makini wangeanzisha wenyewe kuukataa huo mswada. Kwanini hawakufanya hivyo na badala yake kusubiri CDM waseme wakati kanuni ya 86:3b inaweza kutumiwa na mbunge yeyote? kwanini hawa wabunge 'makini, wa ukweli' wasifanye hili jambo wenyewe?
c. Kwa vile mswada umepitishwa uwepo wa hao wabunge wa CCM ambao unaamini wangeweza kukubaliana na hoja ya CDM hauna msingi kwa sababu kama kweli wangekuwepo na wanajali maslahi ya nchi wangepiga kura ya kuukataa. Siyo Filikunjombe wale wabunge 'alike' (whatever that means) waliosimama kuupinga mswada. Sasa kama walishindwa kufanya hivi wao wenyewe uliwategemea kweli watengenezewe jamvi la kukanyagia na CDM? Kama kweli wako makini kwanini hawakupinga mswada huo wao wenyewe. NI wazi waliweka maslahi ya CCM mbele.
d. Kama wengine walivyosema, hauna msingi wowote unaokufanya uamini kuwa ati baada ya spika kuuliza Bunge basi Bunge "lazima" lingekubali hoja ya CDM. Thats overtly presumptous.

Mhe. Lissu baada ya kufika kando ya mto na kuyatazama tuu yale maji, akaamua hapa hatuwezi kuvuka, na kuamua kurudi alikotoka, angepaswa kuingiza kwanza huo mguu na kuona kina cha maji.

Sumu haijalibiwi kwa kunywewa!

Mpaka sasa, hoja yangu ya msingi, haijajibiwa, kwanini Chadema hawakutoa pingamizi kwa muswada ule kwa mujibu wa kanuni?.

Hoja yako ya msingi imejibiwa ila hutaki kuamini kuwa ndilo jibu lenyewe. Hakukuwa na maslahi yoyote ya kuweka pingamizi ambalo unajua litakataliwa. Ni bora kuchagua njia ya kutoa maoni na kuondoka kuwaachia wenye kufanya cha kwao wafanye. Binafsi hoja yako ingekuwa nzuri sana kama baada ya CDM kuondoka wabunge makini wa CCM wangejitokeza kuupinga mswada na kuuzia. Hapo ungekuwa na hoja kwamba 'unaona hata CDM kuondoka wameondoka lakini wabunge wa CCM kwa kutumia 86:3b walizuia mswada." Unfortunately that did not happen; so your argument is negated.


Hivi nikisema kumbe waliotuangusha pale bungeni kwa kuruhusu muswada ule upite kiurahisi vile ndio wenzetu hawa hawa tuliowategemee kupinga kwa kutumia, wao wakapinga kwa kususa?.

Hapana waliotuangusha ni wabunge wa CCM ambao kwa kutokana na maslahi ya Chama chao walikubali kupitisha miongoni mwa miswada mibovu ya kisheria ili uwe sheria. Kuwalaumu CDM kwa kutofanya kitu ambacho unajua ilikuwa ni sawa na kusukuma lori mlimani ni kuwaonea. Lawama za kupitishwa kwa mswada huu zinawaangukia moja kwa moja na peke yao CCM na CCM tu. Wangetaka kuzuia wangeweza, wangetaka kufanya mabadiliko ya kweli wangeweza. Hawakufanya.


Nafasi hii ya 86:3b haiwahusu Chadema tu inawahusu CCM, CUF na NCCR kwanini hivyo vyama vingine havikusimama kuweka pingamizi? Au pingamizi lingekuwa pingamizi zuri endapo tu CDM wangeliweka?




Maneno yako ni ya kujaribu kukatisha tamaa watu. Wapo wanaoweza kukata tamaa kwa sababu umesima "there is nothing" that can be done. Bahati mbaya sana, ulimwengu umeundwa na watu ambao hawakubali kauli kama hizo. Kuna watu waliamini kabisa apartheid system isingeweza kuondolewa na kle Afrika ya Kusini wapo hata watu weusi ambao walikubali kuwa watumishi wa mfumo huo kwa sababu hawakuona dalili ya kuweza kuung'oa. Hata leo wapo watu wanaoamini kabisa vitu fulani haviwezi kufanyika kwa sababu hawaoni namna ya vitu hivyo kufanyika. Ukweli ni kuwa tuna historia ya kutosha tu katika bunge letu kuwa sheria ikipitishwa haina maana haiwezi kubadilishwa. Na kufanya kosa la kupinga ni uhalifu haitishi sana watu kwa sababu watawala mara zote hutumia sheria kukandamiza watu na wale wenye dhamira sahihi wanakuwa tayari kuvunja sheria hizo kwa sababu ni kinyume na haki, utu na usawa wa mwanadamu.

Tena kwa kufanya ni kosa la kihalifu wamethibitisha kuwa hawakuwa na hoja na sasa wana vioja!


Ndipo hapa ule ushauri wangu unaporudi tena, Chadema wakubali, makosa, sio lazima watubu hadharani, hata kimoyo moyo kama walivyosema hadharani hawamtambui rais, lakini kwa vile ana exist, umtambue usimtambue, yeye anabaki kuwa ni rais!.

Nadhani wenye kuhitaji kutuba kwa kugalagala na kujifunika magunia na kujipaka majivu kichwani ni CCM na wale wote ambao wanaamini kuwa CCM haina lawama katika kupitisha mswada huu mbovu wakati ndicho chama kilicho na wabunge wengi na ndichoa ambacho kimeshikilia Urais.
 
Nyandaigobeko, asante kwa hotuba hiyo, kwa vile Mhe. Lissu ndio amewasilisha pingamizi?. Mimi nasisitiza Mhe. Tundu Lissu hakuwasilisha pingamizi!. Mimi nasimama kwenye ukweli halisi kwa mujibu wa kanuni, hakuna pingamizi lolote lililowasilishwa!.

Wanabodi, pia naomba nikiri mimi ni mgumu wa kueleweka, nawasoma wengi humu wanaamini pingamizi limewasilishwa, lakini nashukuru kuna wachache humu, wanaelewa fika kuwa hakuna pingamizi lolote dhidi ya muswada huo lililowasilishwa, alichokifanya Mhe. Lissu ni hotuba ya maoni ya kambi ya upinzani, hata kama kwenye hotuba hiyo aliwasilisha matamshi ya pingamizi, someni kanuni jamani, pingamizi ni pingamizi na sio hotuba na hotuba ni hotuba tuu na sio pingamizi.

Jamani sipendi ubishi, wale ambao mnaamini pingamizi liliwasilishwa, endeleeni kuamini hivyo ili kuzipa raha dhamira zenu, wachache wanaonielewa, wanaelewa ukweli halisi wa 'nothing but the truth', HAKUNA PINGAMIZI LOLOTE LILILOWASILISHWA BUNGENI KUUPINGA MUSWADA HUO!.
 

kaka. ninasoma haya maandishi ya Pasco. ninachokiona ni kuwa ndugu Pasco anahoja ambayo ni "ideal" na hoja unazotoa wewe ni "real". siamini kusema eti ccm ina wabunge makini wangeunga mkono hoja ya CDM. sasa hajiulizi mpaka CDM wana toka bado hao wabunge makini hawakuweza kuibua hoja, kwa nini?. hivi ni nani asiyejua kuwa pale inapofika maslahi ya chama , CCM wanasahau maslahi ya nchi?.
ninaumia sana watu wanaposhindwa kufikilia mustakabali wa taifa, na kuendekeza itikadi ambazo zinawapatia chakula cha leo. ingependeza watanzania tungeache kuzaa. maana tunaowazaa hatuwatengenezei pa kuishi baadae.walio tangulia waliumia walijitahidi kwa nguvu zote wakatuachia taifa hli. lakini sisi tume jikita kuvuruga tu.
 
Kwahiyo una maana Lissu hakufuata kanuni bali alitoa hotuba?

Binafsi nadhani hotuba yake ndiyo ilikuwa na maelezo kuwa ni kwanini hakufuata kanuni hizo za pingamizi.
JMushi, Mhe. Lissu amewasilisha hotuba ya kambi ya upinzani kihalali kabisa tena kwa mujibu wa kanuni.

Ninachosema mimi, Mhe. Lissu hakupaswa kuwasilisha hotuba ile, alipaswa kuwasilisha pingamizi kwanza, kama angewasilisha pingamizi, Bunge lingesitisha majadiliano na kulisikiliza kwanza pingamizi, Hayo Mhe. Lissu aliyoyaeleza kwenye hotuba yake, alitakiwa ayaeleze kwenye pingamizi na sio kwenye hotuba. Bunge lingeshughulia kwanza pingamizi and you never know!.

Kwa vile hakukuwa na pingamizi rasmi, ile hotuba ya Mhe. TL ndio ilikuwa inahitimisha uwasilisha na kufungua mlango wa kuanza kwa majadiliano!.
 

Angalau umekaribia sasa .. 'you never know'. Mwanzoni ulisema kuwa kwa kuwasilisha pingamizi mswada ungesitishwa. Uliamini kuwa kwa kutoa pingamizi basi mswada usingeendelea na kurudishwa kwenye kamati. Bahati mbaya hutaki kukubali kuwa msimamo wako wa awali hauna msingi wa kanuni za Bunge. Unachosema sasa baada ya kurasa hizi zote ni kukubali kuwa CDM wangejaribu tu kuweka pingamizi lakini hatima yao ingeamuliwa na wabunge wa CCM. Hatujui kingetokea nini - and hence your 'you never know'.

a. Kubali kuwa kanuni ya 86:3b hailazimishi kuzuia mswada kusonga mbele, unatoa nafasi kwa pingamizi kutolewa na mbunge yeyote (siyo lazima wa CDM au wa upinzani; hata wa CCM angeweza kutoa na hawakutoa).

b. kubali kuwa kipengele cha 86:4 kinatoa nafasi kwa Bunge kuamua juu ya pingamizi lililowekwa kwa misingi ya 86:3b. Na kuwa spika atawahoji wabunge kutoa uamuzi kama kukubali pingamizi au la.

c. Kubali vile vile kuwa kutokana na wingi wa wabunge wa CCM ambao tayari walionesha ushabiki wa kutaka kupitisha mswada na kweli baadaye waliupitisha ilikuwa ni vigumu sana kwa CDM au chama kingine chochote kuzuia mswada ule.

d. Kubali kuwa jukumu la kuzuia mswada ule kwa maslahi ya taifa liliwaangukia wabunge wote na hasa wabunge wa CCM ambao ndio wengi Bungeni. Ni rahisi kwa CCM kuzuia mswada mbaya kuliko kwa CDM kushawishi CCM wazuie mswada ambao unaweza kunufaisha CCM zaidi.

je unakubali?
 

Mbona unamlazimisha kukubali? unapenda mashindano mkuu.duh!
 
Jamani nadhani ameshaliona kosa lake japokuwa hataki kukubali. Mimi huyu jamaa namjua sana kwa undani.. ni social climber mmoja wa hatari sana na ubishi na misifa ndio jadi yake...
 

Nimekuelewa MwanaK.
 
Anayependa mashindano ni Pasco, na ndio maana Tundu lisu alimuumbua siku ile ya mdahalo. Tundulisu akiendelea kujibu swali lake jamaa akawa ananyoosha mkono huku body language (akitikisa kichwa) ikionesha kukipinga kile Tundulisu alichokuwa anaekieleza, ndipo Tundulisu akaamua kumuuliza anayetakiwa kujibu swali ni nani ...mimi au wewe?
Mbona unamlazimisha kukubali? unapenda mashindano mkuu.duh!
 
Mzee Mwanakijiji, please lets cut the long story short naomba tuufunge huu mjadala kwa swali moja dogo, jee kuliwasilishwa pingamizi lolote?. Mimi nasisitiza hakuna pingamizi lolote lililo wasilishwa bungeni kupinga muswada huu!. Nakuomba sio unielimishe wala sihitaji maelezo marefu, jee muswada ule ulipingwa kwa mujibu wa kanuni?.
 

haukupingwa na CCM wala chama kingine chochote kwa kutumia kanuni. Vyama vingine havikuwa na namna ya kuuzia mswada. Lakini na wewe ujibu swali: Je unaamini kuwa wabunge makini CCM wangeweza kuzuia mswada ule kwa kutumia 86:3b lakini hawakufanya hivyo na hivyo walipitisha mswada ambao wangeweza kuuzuia?
 
Mzee Mwanakijiji, kwanza nakubali yote!.
Lakini nakuomba na wewe ukubali langu moja tuu, jee muswada ule ulipingwa au haukupingwa?. Nikimaanisha jee kulikuwa na pingamizi lolote kupinga muswada usiwasilishwe?.
 

sasa wewe una maoni gani kuhusu hiyo sheria? Je itasaidia watanzania kupata ya kiwango cha juu kama wengi wanavyotarajia? Au itakuwa tu ni yale yale ya miaka yote(rais ndiye mtu wa mwenye kuamua ni kitu gani cha kuweka kwenye katiba)
 
Kuna kitu najiuliza hapa; Hivi hawa waandishi mahiri na wenye uelewa mkubwa ktk hili watatumia kalamu zao bila uoga kuwaonyesha wananchi wa kawaida ubovu wa sheria hiyo na hasara ya kuitumia ktk mchakato wa kupata katiba, au watajitahidi kuwaonyesha makosa ya Chadema kuwa 'wangefanya hivi pengine ingekuwa hivi'...?? au watawashauri wasomaji wao kuwa kwa kuwa ccm wamelazimisha matakwa yao basi hakuna namna, kubalini tu yaishe... Kweli???
Sasa hivi tumechoka kiasi kuwa hata kuhoji kwa nini bunge limepokea muswada ambao waliouandaa wamekiuka hata maagizo ya bunge lenyewe tunashindwa, tumebaki kulaumu kuwa Chadema wangefanya hiki na kile... Hivi ni kweli mchakato wa katiba unawategemea Chadema na ccm na ndivyo inavyotakiwa kuwa?
 
Mzee Mwanakijiji, kwanza nakubali yote!.
Lakini nakuomba na wewe ukubali langu moja tuu, jee muswada ule ulipingwa au haukupingwa?. Nikimaanisha jee kulikuwa na pingamizi lolote kupinga muswada usiwasilishwe?.

Naam. Kama umekubali mjadala umeisha. Shukrani mkuu.
 
Asante kwa jibu lako nawaomba na wengine wote wajue kuwa muswada ule haukupingwa na yeyote!. This is a fact!. Kumbe harakati zote za kujidai kupinga zilikuwa ni ngonjera tuu!. Kama hakukuwa na pingamizi lolote hivyo kupelekea muswada kupita kiulaini! Kelele zote za kuupinga was nothing ni makelele tuu!, inatolewa fursa ya kupinga, hakuna anayepinga hizo kelele mnapigia nini?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…