FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Dada yangu Faiza Fox, wewe kama mama wa familia una majukumu yako kwa mumeo, familia, na jamii. Katika kutimiza majukumu hayo, unadhani unafanya favour?. Mfano kumvisha mwanao, kumsomesha etc, au kumpikia mumeo na kumpa vile 'vyakula' vyote is it favour?.
Hayo yote JK aliyoyafanya ni within majukumu yake, anatimiza wajibu wake, tumpongeze rais wetu kutimiza wajibu wake?.
Nakushauri anzisha thread ya " MEMA YA JK', au "MAZURI YA JK", tutachangia!.Humu tunajadili jinsi watu tuliowategemea kuupinga ule muswada, walivyoshindwa kuwasilisha pingamizi ambalo mimi naona ni kosa, na sio kujadili mazuri ya JK.
Wiki ijayo, atausaini huu muswada kwa mbwembwe zote, tumpongexze pia kwa kusaini maana atakuwa amewafanyia watanzani favour kubwa kuwaanzishia safari ya kuelekea katiba mpya!.
Kufanya jema si kufanya favour. Favour ni kitu kingine kabisa havihusiani na wema, umenena vyema kasoro:
Hapo nilipokuwekea nyekundu, kumbuka mimi ni Mwanamke wa Kiislaam, nna wajib wangu kwa mume wangu, watoto, jamii na kadhalika, hilo la kumpikia mume wangu si katika majukumu yangu, Waislaam wanaume hufundishwa "kumlisha na kumvisha mkeo", sasa tazama hiyo kauli halafu uniambie. Kupika ili anilishe ni jukumu lake kama hawezi kupika aniwekee mpishi, ikiwa mimi ntaingia kumpikia na kumlisha basi mawili, amma nnamfanyia "favour" kwa kupenda kwangu amma nipatane nae awe ananilipa ujira wa kazi yangu hiyo ya kumpikia.
Wengi wana dhanna kuwa kupika na kumfulia mume ni kazi za mwanamke, la hasha si wa Kiislaam, wafanyao hufanya kimila zilizo nje ya Uislaam amma hufanya kama "favour" si jukumu lao hata kidogo. Saa ngapi nijipambe kwa ma oud (udi) na ma liwa, saa ngapi nipike saa ngapi nifuwe saa ngapi nioshe vyombo? khaaa! hata hiyo mikono si itakuwa kama fundi mekanika halafu nije kumshikashika mume wangu si ntamchubuwa? Unanchekesha, mke nyumbani ni pambo babu na si "house girl".
Kuhusu hili la Kikwete hata kama ni majukumu yake basi bado ni jema, kwani hao wa mwanzo hawakuwa na jukumu hilo? mbona walikuwa wanatuwacha twende Kenya kwanza kabla ya kufika Mwanza. Hilo ni moja kati ya Mema ya Kikwete wala halina ubishi.