Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!


Kufanya jema si kufanya favour. Favour ni kitu kingine kabisa havihusiani na wema, umenena vyema kasoro:

Hapo nilipokuwekea nyekundu, kumbuka mimi ni Mwanamke wa Kiislaam, nna wajib wangu kwa mume wangu, watoto, jamii na kadhalika, hilo la kumpikia mume wangu si katika majukumu yangu, Waislaam wanaume hufundishwa "kumlisha na kumvisha mkeo", sasa tazama hiyo kauli halafu uniambie. Kupika ili anilishe ni jukumu lake kama hawezi kupika aniwekee mpishi, ikiwa mimi ntaingia kumpikia na kumlisha basi mawili, amma nnamfanyia "favour" kwa kupenda kwangu amma nipatane nae awe ananilipa ujira wa kazi yangu hiyo ya kumpikia.

Wengi wana dhanna kuwa kupika na kumfulia mume ni kazi za mwanamke, la hasha si wa Kiislaam, wafanyao hufanya kimila zilizo nje ya Uislaam amma hufanya kama "favour" si jukumu lao hata kidogo. Saa ngapi nijipambe kwa ma oud (udi) na ma liwa, saa ngapi nipike saa ngapi nifuwe saa ngapi nioshe vyombo? khaaa! hata hiyo mikono si itakuwa kama fundi mekanika halafu nije kumshikashika mume wangu si ntamchubuwa? Unanchekesha, mke nyumbani ni pambo babu na si "house girl".

Kuhusu hili la Kikwete hata kama ni majukumu yake basi bado ni jema, kwani hao wa mwanzo hawakuwa na jukumu hilo? mbona walikuwa wanatuwacha twende Kenya kwanza kabla ya kufika Mwanza. Hilo ni moja kati ya Mema ya Kikwete wala halina ubishi.
 
Duh nawakubali CDM wanakaba mpaka penalty ahaaa aaaa.

Sio suala la kukaba hadi penalty; kama mtoa mada ameshakiri kwamba wabunge CHADEMA hawakufanya kosa peke yao, bali wabunge wote walikosea katika kuupitisha huo muswada bila kuupinga, ni halali na haki kichwa cha uzi kibadilishwe ili uzi huu ubaki kama uwanja wa kuelimishana na kushauri namna ya kusonga mbele!!
 

Wewe kweli u mzito kuelewa kwa hiyo na hizo 5000 zingine zikisha zitakuwa zaidi ya KM 14,000 ahsante kwa kunirekebisha, hapo umeniongezea hesabu yangu.

Hata hizo 5000 uzisemazo wewe kwa miaka 6 bado ni nyingi kuliko marais wote wa kabla yake pamoja na mkoloni. Upo hapo ulipo?
 

Kuna mawili, aidha hukusoma ama hujui kabisa hesabu ama la ulisoma na ukapata zero.

Kama tuna barabara za lami zinazofikia urefu wa km 5,000 na kuna wakandarasi wanajiandaa kuanza ujenzi ili tufikishe barabara zenye urefu wa km 10,000 hapo ni kusema takribani barabara za urefu wa km 5,000 ndio ziko kwenye maandalizi ya kujengwa, sasa sijui hiyo km 14, 000 umeitoa wapi!

Nimesema kwa mujibu wa waziri magufuli, hadi sasa tuna barabara za lami zinazofikia km 5,000. Hapo kwenye km 5,000 unazungumzia barabara zote alizojenga Nyerere, Mwinyi, Mkapa na alizomalizia Kikwete kutoka kwa mkapa. Na ni ukweli uliodhahiri kwamba Mkapa ndiye kajenga barabara nyingi za lami unazomsifia kikwete. Kama unataka kumsifia kikwte kwamba ndiye kajenga, subiri 2015 atakapokuwa ameondoka madarakani, na kama hizo ambazo ziko kwenye mobilization stage zitakuwa zimekamilika, kwakuwa tumewazoea mnapeleka wakandarasi site bila kuwalipa kwa ajili ya kujitafutia sifa za kijinga na umaarufu wa bei chee, lakini mwisho wa siku wanaishia kuondoka na barabara kubaki na mahandaki kama kawaida.

Narudia kusema kwenye barabara kikwete hawezi kuchukua credit yoyote hadi hapo atakapokamilisha miradi aliyoianzisha mwenyewe! wala usimtafutie kusifiwa kwa kazi nzuri ya Ben Mkapa.
 
Hayo yote hayahitaji kusifiwa mkuu kwavile ndio majukumu ya serikali na ilipoomba kura, iliahidi kutekeleza hayo majukumu. Mimi sioni kipi cha kusifia wakati inatekeleza/itakua inatekeleza majukumu yake iliyopewa na wananchi.

Mkuu naomba nikukumbushe kwamba miaka mingi yu iliyopita, serikali ilikuwa imependekeza na kuamuliwa ujengwe uwanja mpya wa kimataifa huko mkuranga na kulikuwa na mpango wa kuiboresha bandari ya mtwara na Tanga ili ziweze kukidhi mahitaji ya mizigo inayoingia na kutoka nchini.

Lakini all over sudden baada ya JK kuingia madarakani serikali imeanza kubadili mawazo na kutaka kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa bagamoyo badala ya mkuranga. Serikali hiyo hiyo imeanza kupanga kujenga bandari kubwa na ya kisasa bagamoyo na kuziacha bandari za tanga na mtwara.

Hapo sasa mimi ndo nikasema asubiri tumsifu kwa hilo! nadhani anataka kuigeuza bagamoyo kuwa kama yamousokrou ya ivory coast, nadhani hadi hapo utakuwa umenisoma.
 

Hakika kwa hili atahitaji kupewa sifa maana he will accomplish the extraordinary!! Nimekusoma kamanda.
 
Ila Pasco wewe ni kiboko. All in all sijatoka mtupu hapa kuna elimu kubwa sana nimeipata hapa nadhani wengi watakiri hivyo.
 
Pasco,

..nadhani waliopaswa kusimamisha mswada wa katiba ndani ya bunge kupitia kifungu ulichokitaja ni wabunge wa CCM na siyo Chadema.

..nasema hivyo kwasababu CCM ndiyo wenye wabunge wengi mle bungeni na wanachoamua wao ndicho kinachopita.

..mabadiliko kupitia bunge la nchi hii kwa kweli yanategemea zaidi CCM kuliko chama chochote kile kinachowakilishwa ktk bunge la jamhuri.

..bila CCM kutanguliza maslahi ya taifa ndani ya bunge basi kwa kweli wananchi tuandike maumivu tu.

..mtawapigia kelele CDM lakini kwa mtizamo wangu they did what they could ktk mazingira magumu sana.
 
JokaKuu,

Nadhani waliopaswa kusimamisha mswada wa katiba ni wabunge toka chama chochote ambao walibaini kasoro za mswada.



 
Mkuu sawa nimekuelewa vizuri sana lakini nachotaka kuelewa zaidi ni wakati gani PINGAMIZI hututolewa na mbunge? tuseme kuna mbunge wa CCM, NCCR, ama chama kingine ametaka kutoa PINGAMIZI utaratibu wake unakuaje?
 
Hapana mkuu wangu nimemwelewa vizuri Pasco... anachosema yeye ni kwamba mshtakiwa alitakiwa kusema maneno haya:- GUILTY ama NOT GUILTY kisha utaambiwa kaa chini na kesi itaahirishwa hadi baadaye mtakapo itwa tena, na sii kutoa maelezo ya kujitetea..

Hivyo, kulingana na utaratibu wa Bunge Mama Kilango alitakiwa kuisoma hotuba ya TL mapema na kukuta makosa yamefanyika hivyo kusema hili ni PINGAMIZI hivyo yachukuliwe maneno ya mwisho tu..Ndivyo ilivyo mahakamani mtu ukikosea na kuanza kujieleza wakati unatakiwa kusema guilty or not guilty jaji hutoa mwongozo. Hawezi kutoa hukumu kwa kufuata makosa ya kanuni wakati mtuhumiwa anatakiwa kukiri amekubaliana na amepinga..

Kwa maana hii Spika aliyaona makosa ya kanuni toka kambi ya Upinzani ktk kujibu wanakubaliana ama wanapinga lakini akayaachia yaingie bungeni kwake makusidi ili pingamizi litakapo somwa litaonekana ni maoni ya kambi ya Upinzani kisheria..na ndio maana alikataa kutoa hata mwongozo makusudi.
 

As far as I remember, baada ya Waziri wa Katiba na Sheria Kombani kuwasilisha muswada bungeni kwa mara ya pili, alisikika mbunge akiomba mwongozo wa Spika kuahirisha bunge. Spika hakutoa nafasi ya kusikiliza mwongozo unasema nini na akasema hakuna mwongozo. Kisha akamwita msemaji wa Kambi Rasmi ya Ushindani (siyo Upinzani) bungeni. Tundu Lissu akashusha nondo zake na alipomaliza wanabunge wa Chadema na NCCR-Mageuzi wakatoka nje. Sioni kama Chadema wali'miss' any opportunity bali walijua maoni yao hayatasikilizwa. After all, kwenye hotuba ya Kombani zile sehemu zote muhimu ambazo zilihitaji marekebisho ya msingi alisema: "Serikali haikukubaliana na marekibisho hayo na hivyo serikali imeona ibaki kama ilivyo." Kwa maneno mengine, kubaki kwa Chadema bungeni kusingesaidia chochote badala yake kungetumiwa na serikali kwamba wamepitisha muswada pamoja na ili ilionekane kuwa hawakuunga mkono huo ujanja wa CCM ilibidi wapenda mabadiliko watoe msimamo wao.
 
Inasikitisha sana ndugu yangu. Huko nyuma nimeuliza kuwa hawa 'waandishi mahiri' watatumia kalamu zao kuwaonyesha wananchi ubaya wa sheria hiyo au kile ambacho Chadema hawakufanya??!!
punainem-red, japo zamani niliwahi kuwa mwandishi wa habari, bahati mbaya sikuwahi kufikia kiwango cha 'mwandishi mahiri'.
Anayetembea akajikwaa na kuanguka, akiinuka na kuangalia pale alipoangukia, next time atajikwaa tena pale pale na alipojikwaa mwanzo.

Yule anayetembea na akajikwaa na kuanguka, anapoinuka na kutazama pale alipojikwaa na sio alipoangukia, huyo next time, hatajikwaa tena pale pale!.

Naamini kwa kuonyesha tuliowaaminia, wamejikwaa wapi, next time hawatajikwaa tena pale pale!
 
Mkuu hicho kipande nilicho ki highlight unaweza kuthibitisha mbunge huyo ni nani ama tunaweza kupata hotuba nzima ya bunge siku hiyo...
 
Joka Kuu, hii ni kweli ndio maana nikaikubali hoja ya Mzee Mwanakijiji iliyofunga mjadala, na nikasema wazi, tuusiitwishe mzigo huu Chadema.
 
Ngongo said:
Nadhani waliopaswa kusimamisha mswada wa katiba ni wabunge toka chama chochote ambao

Ngongo,
..nakubaliana na wewe 100%...nilichomaanisha mimi ni kwamba CCM, kwa kuzingatia kwamba ndiyo wengi ktk bunge, had a better chance ya kufanikiwa kusitisha mswada huo kwa ku-invoke kifungu anachokitaja Pasco.

..tunawalaumu CDM bure, quite frankly they can only do so much ndani ya bunge lililosheheni wana CCM walioweka mbele maslahi binafsi na ya chama chao.

..binafsi nilipoona mswada mbovu kiasi kile umeshafika bungeni tayari niliandika "maumivu." there was no party other than CCM ambao wangeweza kuuzuia mswada ule usipite.

..lawama zangu nazielekeza kwa Raisi, Mwanasheria Mkuu, na Waziri wa Sheria, na wabunge wa CCM. hao ndiyo waliokuwa na UWEZO wa kutupatia mswada mzuri unaozingatia maslahi ya taifa.
 
Mkuu sawa nimekuelewa vizuri sana lakini nachotaka kuelewa zaidi ni wakati gani PINGAMIZI hututolewa na mbunge? tuseme kuna mbunge wa CCM, NCCR, ama chama kingine ametaka kutoa PINGAMIZI utaratibu wake unakuaje?
Naomba ipitie ile update 3 kwenye maandishi mekundu.

Baada ya hotuba ya mtoa hoja, serikali, mbunge yoyote atasimama na spika atakampa nafasi, atatangulia kusema yale maneno kwenye red. Spika atasimamisha kila kitu na kusikiliza hilo pingamizi na sababu za pingamizi hilo.
 
Mkandala, hakukuwa na makosa kwenye hotuba ya TL, kwani yale ndio maoni ya kambi ya upinzani, tatizo, kwenye maoni hayo, ndio akaweka na kipengele cha pingamizi ambalo spika makinda, alilikataa. Enzi za Sitta, wangetengua kanuni, kile kipengele cha pingamizi kirudishwe kwenye pingamizi na lingesikilizwa, na Sitta ni miongoni wa wana CCM bold sana ambaye asingekubali upuuuzi upuuzi wowote wa serikali. Nakumbula alipobishana na Jaji Mkuu kuhusu ulegevu wa mahakama, na ile siku JK analihutubia lile bunge jingine, Sitta alimshutumu kuwa amezidi upole, pale alipowasamehe wezi wa EPA!.

Tumuombee Mama Makinda nae apate busara kama za Sulemani, vinginevyo, tumekwisha!.
 
Magobe T, hili la kushindwa kuchukua hatua kwa kuogopa defeat, kwangu ni udhaifu!, wangechukua hatua, washindwe na Watanzania katika umoja wetu tungesimama nao!.
 
Pasco said:
Joka Kuu, hii ni kweli ndio maana nikaikubali hoja ya Mzee Mwanakijiji iliyofunga mjadala, na nikasema wazi, tuusiitwishe mzigo huu Chadema.

Pasco,

..u have very good points.

..lakini nadhani huenda uliweka matumaini makubwa mno wa CDM, tena ktk mambo ambayo hawana uwezo nayo.

..hivi umejiuliza kwanini imefika mahali KANUNI ndiyo zitumike kuupinga mswada wa katiba na siyo HOJA zenye uzito?

..binafsi nadhani njia nzuri ya kuboresha mswada wowote ule ni kupitia HOJA na MAPENDEKEZO mbadala na siyo kanuni.

..kanuni can only buy u sometime, lakini at the end of the day, mswada unaboreshwa kupitia maoni, na zaidi unapitishwa kwa kura za wabunge.

NB:

..nasisitiza kwamba hoja zako ni nzuri ktk kutoa "somo" kuhusu masuala ya kanuni za bunge. wasiwasi wangu ni kwamba "somo" hili unalojaribu kutoa kwa CDM peke yao linaweza kutumika vibaya na kuwa upenyo wa kutokea kwa wale ambao hawakufanya kazi kwa maslahi ya taifa hili, yaani Raisi, Mwanasheria Mkuu,na Waziri wa Sheria.

..ukitaka kujua kwamba Raisi hana nia njema ni pale alipoamua kuwadanya wazee wa DSM, watu wazima wanaoweza kumzaa, kwamba CDM walisema wataandika katiba mpya ndani ya siku 100.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…