Hapa ndugu Pasco labda utusaidie maanake ushahidi huu unamweka Spika mahala pabaya zaidi kulingana na jinsi Pasco alivyotujuza huko nyuma..Maanake kila ulichoandika hapa kinaonyesha wazi juhudi za kuvunja majadiliano ya muswada huo yalifanyika kulingana na kanuni za bunge lakini Spika alipuuza..
Mkuu Mkandara, Mjadala huu tumeshaufunga kilichobaki ni kuendelea tuu kuelimishana kuhusu kanuni.
1. Mijadala ya bunge inaendeshwa kwa kanuni.
2. Hoja zote rasmi zinawasilishwa kwanza kwa spika kwa maandishi ndipo zinakuja kusomwa. Hata yale maswali yalishawasilishwa kwanza ofisi ya spika kwa maandishi. Na yale majibu pia yako kwa maandishi.
3. Mbunge yoyote mwenye hoja, ataiwasilisha kwa spika kwa maandishi.
4. Mpaka ninapoandika hapa, hakuna hoja yoyote ya kuhusu pingamizi iliyowasilishwa kwa maandishi kwa spika!.
5. Kanuni ya 86 inamuamuru spika asipokee hoja yoyote swali lolote wala kutoa muongozo wowote isipokuwa 86.3. Hakuna pingamizi lolote lililowasilishwa hivyo alikuwa right kukataa kila aliyetaka kuzungumza.
6. Hotuba ya TL aliiwasilisha kwa mujibu wa 86.6 ambayo ni maoni ya kambi ya upinzani. Kwenye maoni hayo ndipo akaweka na pingamizi mumo kwa mumo.
7. Maoni ni maoni, na pingamizi ni pingamizi!. Kanuni inasema pingamizi ikiwasilishwa kwa mujibu wa 86.3, Bunge litasitisha mchakato, kusikiliza pingamizi na bunge kupiga kura kuhusu kupitisha pingamizi hilo au kutopitisha.
8. Kwa vile ofisi ya spika ilishapewa hotuba ya TL in advance, na ikaona kuwa imechanganya maoni na pingamizi, ingekuwa ni enzi za SS wangetengua kanuni na kusikiliza pingamizi lililowasilishwa kama sehemu ya maoni. Hapa lazima tumkumbuke yule mzee wa kasi na viwango, Speed & Standards, SS.
9. Kanuni inaelekeza baada ya TL kuwasilisha maoni, majadiliano huanza bila kupokea hoja nyingine yoyote, swali au muongozo wowote!.
10. Namalizia kwa msisitizo, HAKUNA PINGAMIZI LOLOTE, LILILO WASILISHWA NA YEYOTE KUUPINGA MUSWADA HUO!. Alichowasilisha TL ni maoni na sio pingamizi!.