Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

pasco si leo wewe ulikuwa movenpick na ukauliza swali hili?? n ulijibiwa tena vizuri...na unajulikana umeegemea upande gani...
 
tka juzi kakomalia kanuni hii ya 86...leo kaenda movenpick kwenye mdahalo akauliza sawali hili..akajibiwa vizuri sana lakini kwa kuwa toka juzi amekomaa bado hakubali....halafu anasema mimi sina chama wakati tunakujua vizuri mlengo wako...halafu hiyo kanuni unayoikomalia haitoi mwanya wa kuzuia hoja kutojadiliwa....mbona vitu viko wazi mkuu!!!
 
Pasco usijidanganye hata kidogo. CCM walikuwa waipitishe tu hata ingekuwaje! Walikuwa na mkakati wa kufanya hivyo kijanja janja kama kawaida yao. Na wanachoamini ni kuwa wananchi wengi wala hawajui maana ya katiba, wanajua fika kuwa wasomi wengi, na haswa walioelimika wako kinume kabisa na hii staili yao ya kuchaguana na kundesha nchi.
Kwa maoni yangu ni afadhali ikabakia kwenye historia kwamba ni CCM peke yake ndiyo walipitisha huo mswada. Period!
 


Wananchi wakiamua wanaweza kusimamisha huu mchakato wote na hata kumuondoa rais ili asiusaaini mswada kuwa sheria. Wewe ni mnafiki mkubwa sana, na unafiki ni dhambi. ukweli ni kuwa wanachi walio wengi hawajafurahishwa na ubabe wa wabunge wa ccm na wake zao cuf na wanatafakari wafanye nini kuonyesha hasira yao ila muda utatupa majibu ya kilicho jaa ndani ya mioyo ya waTZ hasa Watanganyika.
 
Pasco,pia ni muhimu kutenganisha mambo ya katiba mpya na chadema kwasababu ukisema hivyo unawachanganya wananchi especially wene uelewa mdogo.

Issue kwa wengi wetu si katiba mpya ya chadema,ni katiba mpya ya wananchi.

Kama imetokea kuwa chadema iko upande wa wananchi kwenye upatikanaji wa katiba mpya,basi haina maana kuwa katiba hiyo ni ya chadema.

Katiba ya nchi yenye multiparty ni lazima iwe na katiba yenye kuakisi hilo.

Na katiba hiyo itapatikana kwa kutokana na wadau wote wa jamii kama inavyoeleweka kiutaratibu kwenye taifa linalofuata utawala wa kidemokrasia.

Kwahiyo kudhani kwamba hata wao chadema ndiyo wenye kubeba mustakabali wa katiba ya nchi kama vile ni katiba yenye kukidhi mahitaji ya chama fulani pekee,basi ni kutaka kuleta upotofu.

Kumbuka kuna kada za wananchi mbali mbali na hata wasio na vyama vya siasa lakini wenye uchungu na taifa lao.

Hao umewaweka wapi?Tuweni makini sana kwenye issue hii ya katiba kama ni kweli tunataka kupata katiba mpya.
 
Hata kama ni yeye Mayalla.cha msingi tujikite kuangalia hoja yake na kuijibu kama ambavyo MMKJ kashaanza na wengine.
 

Ahsante sana Mkuu. Watu wanasahau nguvu ya umma wanadhania chama ambacho wanachama wake hawafikii hata 2% ya population yetu wanaweza kuiburuza 98% ya idadi ya Wananchi bila kujali matakwa yao kwenye swala muhimu kama hili la katiba ya nchi.
 
Alishaibiwa na Lissu
Lissu aligusia hicho kifungu cha 86?Lissu inaoneana alizungumzia hotuba...Labda muweke na hilo hitimisho haa ili na sisi tujuwe kama lilijibiwa.

Kwa mujibu wa Pasco,Lissu alijubu hivi...

 
eti tundu lissu amepinga chenga..hahaah...watu wameona amekujibu tena vizuri tu ...au ulitka kumtia maneno mdomoni ili akupe majibu unayotaka kwa herufi na sentensi unazotaka?......lissu siku hiyo bungeni alitoa maoni ya kambi ya upinzani na alipinga moja kwa moja huo mswaada kusomwa kwa mara ya pili..na alieleza sababu lukuki....leo kwenye mdahalo ameeleza tena tena vizuri tu...
 
Ni kweli mbumbu na wafuata upepo.Hawaamini kama viongozi wao hukosea.wakubali kwamba wamechemka na wasonge mbele
 
@Pasco, napingana na hoja ya kwamba CHADEMA wamekosea:
1. Kama umesoma huu muswada na kuuelewa vizuri (nasisitiza kama umeuelewa huu muswada between the lines) utagundua CCM wameshaamua katiba iweje na hofu yao ya kuupeleka kwa wananchi ni kwa sababu watu wangefumua kila kitu!. hilo moja

2. Kama umemsikiliza Lissu, mambo aliyosema bungeni kwa niaba ya kambi ya upinzani ndiyo hayo hayo anayesema sasa. Na leo hii kasema pia alitoa hoja zote hizo kwenye kamati ya bunge ambayo yeye ni mjumbe. Lakini tunajuwa mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa kamati hii ya katiba na sheria ni wabunge wa ccm wa VITI MAALAM na wako pale kwa kazi MAALUM = kusimamia katiba ya CCM na sio katiba ya watanzania wengine!

3. Baada ya hotuba ya Mh Lissu mwakilishi wa kambi ya upinzani, Mnyika alisimama kutoa hoja ya kutaka kusitisha mjadala ili hili swala lirudi kwa wananchi lakini Spika wa CCM (wanamuita spika wa bunge) wazi wazi akakataa kusikiliza. Na kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa mambo huko Dodoma CCM walishaamua huu muswada utasomwa kwa mara ya pili.

4. Kwa mtindo wa uendeshaji wa bunge chini ya spika Makinda ni vigumu sana tena sana kwa CHADEMA kushinda hoja ambayo imeshaamuliwa na CCM. Nadhani unajua mtindo wa 'sasa nitawahoji' na wengi wape. Statistically wabunge wengi ni CCM na sasa wameungana na CUF hivyo kwa vyoyote vile wawili hawa wakishakubaliana kupitisha hoja CHADEMA wanashindwa kwa sababu ya uchache wao. Tuliona wakati wa hoja ya Lissu ya kutoruhus mhimili mmoja (serikili/wakuu wa wilaya/mkoa) kusimamia nidhamu ya mhimili mwingine (mahakama). Pamoja na kwamba ni kinyume cha mgawanyo wa madaraka nchi hii CCM walipitisha hii hoja. Hivyo kusema kuwa Lissu na wenzake toka CHADEMA wangeweza kusitisha muswada huu bungeni kwa kutumia kifungu ni ndoto za mchana. Mtindo wa sasa ni wabunge wanahojiwa na wengi wape. ZIPPED!

5. Kususia kwa CHADEMA- watu wanaweza kubeza na kuona kuwa ni kazi bure! Nahisi unasema haya kwa sababu ulikuwa Dodoma lakini ungekuwa huku mtaani utagundua CHADEMA wanafanya 'people's politics'. Wanaonekana kugusa hisia za wananchi wa kawaida.Wanasoma alama za nyakati. Chama chochote cha kisiasa kinaposhindwa kujua hisia za wananchi ziko vipi kinajitafutia balaa. CCM wanaendeleza siasa za 'kuwaamulia wananchi' lakini wasilo tambua wananchi wa sasa (ambao wengi ni vijana) wanataka waamue hatma ya maisha yao wenyewe baada ya kuchoshwa na mfumo butu unaowanufaisha wachache.

6. Huu muswada umejaa makengeza na CHADEMA wanajua exactly makengeza yote yako wapi, na wana uwezo wa kueleza (articulate) kwa wananchi. Hadi sasa CCM hawajadili huu muswada wameamua ku-advertise Lissu pamoja na kuanika uwezo wao wa kutukana! Na hii itawapa wananchi hamu ya kusikia CHADEMA wakichambua muswada maana wabunge wa ccm wamepoteza hiyo opportunity (siku 4 ya mipasho).

6. Kwa nini wananchi wanawasikiliza zaidi viongozi wa CHADEMA? Wamepatwa na wazimu?

7. Lakini swali muhimu kabisa ambalo CCM wanatakiwa wajiulize ni hili: CHADEMA ni nani? Ni Lissu? Ni Dr. Slaa? Ni wabunge wa CHADEMA kwa ujumla wao? Who is CHADEMA?

Kwa maoni yangu, kitendo cha wabunge wa CHADEMA kutoka nje kimeufanya huu muswada uwe haramu kuliko mbele ya wananchi. Safari ndio imeanza na bila haya ya kuwa na nguvu za Sheikh Yahya CCM wana kazi nzito kama sio kaburi na huu muswada.
 
Lissu aligusia hicho kifungu cha 86?Lissu inaoneana alizungumzia hotuba...Labda muweke na hilo hitimisho haa ili na sisi tujuwe kama lilijibiwa.

Kwa mujibu wa Pasco,Lissu alijubu hivi...


huyu bwana kajibiwa vizuri na hakuna sehemu lissu amepiga chenga kumjibu.....huyu pasco anajulikana ni mzee wa ligi.....
 
Kwa maana hiyo basi Pasco ni mnafiki.
 
huyu bwana kajibiwa vizuri na hakuna sehemu lissu amepiga chenga kumjibu.....huyu pasco anajulikana ni mzee wa ligi.....
@Pasco,kwanini hiyo sehemu ya hotuba yake aliyoitumia kuijibu usingetuwekea hapa tuamuwe wenyewe?

Wewe ume summersize na inaonekana wengine wameridhika na jibu ulilopewa.

Je unapindisha habari kwa maslahi yako binafasi?
 


kaka umemaliza kila kitu....pasco umeelewa?
 
mpotezeeni huyu pasco ni snitch tu,sanasana anataka umaarufu ili tumfahamu kwa kuwa ameuliza swali na ameonekana kwenye tv.
 
Pasco umenena vyema.

Hawa jamaa wa magwanda hawana wakitakacho zaidi ya "shortcut".

Hata Kikwete afanye nini kwao ni kosa tu, tatizo lao ni Kikwete na si Serikali. Hilo lipo wazi kabisa, lakini ukweli ni kwamba Kikwete ndiye aliyefanya mema Tanzania hii zaidi ya Rais yeyote mwingine wa kabla yake na hilo halina utata wala ubishi. Wakae wafikiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…