Pasco,
Suala la katiba lilianza siku nyingi lakini likapata msukumo wa nguvu pale CDM walipolipeleka mahakama ya wananchi. Kosa ni pale walipokubali kuwa rais Kikwete bila ridhaa ya serikali au chama chake alipoamua kulisamimia na CDM wakatulia na kuamini hivyo. Technically hapa ndipo kosa la CDM lilipoanzia.
Kama bunge letu lingekuwa na 'fair play' yote uliyoeleza ndiyo yalipaswa kutokea na lawama dhidi ya CDM zingekuwa haki, kwa bahati mbaya bunge halifanyi kazi kwa kuzingatia sheria au kanuni hasa zinapokinzana na masilahi ya rais na spika ni mjumbe wa CC ya CCM. Anatumwa kutekeleza yale ya chama ni si ya wananchi.
Mswada uliporudishwa baada ya maoni kuleta mushkeli CDM waliuliza je umeondolewa au umefutwa? Nakumbuka PM Pinda alisema umerejeshwa kwenye kamati. Alipobanwa hakuwa na jibu clear na pengine wapinzani wakjua hoja imekufa. Hili nalo lilikuwa kosa kwasababu ilipaswa CDM wapate majibu yasiyo na njia panda.
Kutoka nje ya bunge baada ya kuwasilisha maoni ni jambo la kiungwana kwasababu leo tunajua kwanini walitoka nje, vinginevyo tungebaki kujiuliza wametimka tu je wanajua kwanini wametimka.Kutimka kwao ndiko kumeishtua jamii kuwa lipo jambo, jamii kama ya kwetu ambayo wengi hawana ufahamu mpaka kitakapotokea kishindo ambacho CDM wamekifanya.
Nadhani suala la katiba ni letu sote, CDM wanajaribu kutuwakilisha kwa kadri wanavyoweza wakiwa katika 'stress' ya hali ya juu sana.
Kwa vile katiba ni yetu sasa tujadili tunaiokoaje katiba yetu kwa kushirikiana na CDM ili isipokwe na wanyang'anyi!
Kama ilivyokuwa Nkrumah hall, Karmjee na Zanzibar sisi wenye katiba tusimame na kuwaambia hata kama wamepitisha sheria, sheria hiyo si ile tunayoitaka na tusme No! Tunauwezo wa kuwalazimisha watusikilize, tunasababu tunachokosa kwa sasa ni uthubutu.
Badala ya kuwalaumu CDM tufikirie tutajengaje uthubutu kwa raia wetu ambao wapo tayari