Kwa maana hiyo basi Pasco ni mnafiki.
Pasco hajagundua Spika anaendeshaje bunge. Mambo ya kushika shilingi mara vifungi vya kuzuia hoja vyote vinaishia na kuhoji, mwisho ni wengi wape! Hatuna bunge!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa maana hiyo basi Pasco ni mnafiki.
mpotezeeni huyu pasco ni snitch tu,sanasana anataka umaarufu ili tumfahamu kwa kuwa ameuliza swali na ameonekana kwenye tv.
Mumwi, niko kwenye mobile hivyo sijaweza kuona status yako humu hivyo na presume wewe ni mgeni. Kumfananisha memba wa jf na yoyote ni kosa linaloitwa name calling na adhabu yake ni ban. Humu kwenye jujwaa la siasa tuna discuss issues na ideas hatujadili watu!.We ni Pasco Mayalla tu maana tulikuona ukiuliza hayo maswali.
Pasco umenena vyema.
Hawa jamaa wa magwanda hawana wakitakacho zaidi ya "shortcut".
Hata Kikwete afanye nini kwao ni kosa tu, tatizo lao ni Kikwete na si Serikali. Hilo lipo wazi kabisa, lakini ukweli ni kwamba Kikwete ndiye aliyefanya mema Tanzania hii zaidi ya Rais yeyote mwingine wa kabla yake na hilo halina utata wala ubishi. Wakae wafikiri.
huyu ni pascal mayala anajificha tumeshakujua babu
Mumwi, niko kwenye mobile hivyo sijaweza kuona status yako humu hivyo na presume wewe ni mgeni. Kumfananisha memba wa jf na yoyote ni kosa linaloitwa name calling na adhabu yake ni ban. Humu kwenye jujwaa la siasa tuna discuss issues na ideas hatujadili watu!.
Majukwaa ya kujadili watu pia yapo unaweza kuuliza na utajibiwa.
CDM wengi humu ni mbumbu wa sheria na watu wakufuata mkumbo tu. Wao wanamchukulia mh. Lisu kama Mungu na hakosei hata kidogo.
Mfano uliotoa kuhusu ushauri wake kwa mh Mbowe na kilichomtokea ni kielelezo cha imani ya kibubusa kwa mwanasheria huru kijana.
Utakachokipata humu ni matusi tu badala ya admission of mistakes.
Pasco, Lissu kashakujibu kwamba yeye ile baada ya kusoma spika alitakiwa aulize wanaounga mkono ni wangapi na wasiounga mkono ni wangapi lakini hakuuliza.halafu kama unakumbuka siku ile ya mswaada kuna Mbunge alisimama kuomba muongozo akanyamazishwa kwa kauli kwamba spika akiwa amesimama hamna muongozo akaongezea mswaada wenyewe ndo umeletwa sasa mwongozo wa kitu gani?kaa chini.akasema "tunaendelea, mh.Kilango malecela endelea".ndipo wabunge wakaanza kutoka nje.unajifanya huna chama sio kweli. Mia
Kwa maana hiyo basi Pasco ni mnafiki.
Pasco umenena vyema.
Hawa jamaa wa magwanda hawana wakitakacho zaidi ya "shortcut".
Hata Kikwete afanye nini kwao ni kosa tu, tatizo lao ni Kikwete na si Serikali. Hilo lipo wazi kabisa, lakini ukweli ni kwamba Kikwete ndiye aliyefanya mema Tanzania hii zaidi ya Rais yeyote mwingine wa kabla yake na hilo halina utata wala ubishi. Wakae wafikiri.
Huna cha kuchangia wewe subiri thread zko za kubishana si hii.Endeleeni kuumana tu!
Nitakuja kusoma conclusion. Thanx Pasco for useful post
Pasco, hivi wangetoa hoja kwa kutumia kanuni ya 86 mjadala ungesimamishwa automatically au Spika angeuliza Bunge na Bunge kuamua? Unafikiri Wabunge wa CCM wangekubali kusimamisha mjadala baada ya kuulizwa na Spika?
Sidhani kama wame lose; ukiangalia zaidi utaona kuwa wao wamegain kwa sababu mstari umechorwa kati ya wale wanaoamini Rais na wana CCM wanaweza kufanya yote wayatakayo na wale ambao wanaamini the CCM government is in contempt of the people. Tofauti hii ya maoni ni ya muhimu. Rais na CCM wameweza kulazimisha sheria waitakayo wao kupita - kama walivyofanya kwenye sheria ya gharama za uchaguzi - lakini mwisho wa siku watajikuta ni wao pekee ndio wanaandika hiyo Katiba mpya na wale wanaowaamini au kuwafuata. Je kwa vile sheria imepitishwa ina maana mchakato utakuwa halali kwa kuangaliai first principle? Ukweli ni kuwa CCM hawakuhitaji hoja za CDM au za mtu mwingine yeyote juu ya mswada huu, walikuwa na mawazo yao na wameyatekeleza bila kuzuiwa kwani hakukuwa na mtu yeyote ambaye angeweza kuwazuia.
Siyo lazima. Watanzania ambao hawaamini katika uhalali wa mchakato huu kwa sababu umevunja the First Principle wanaweza kuupinga, kukataa kushiriki na kuwahamaisha wengine wasishiriki kwa hoja ambazo zitaonesha kuwa mchakto mzima umekosewa toka mwanzo na haukuwa nafasi ya kufanikiwa kwa sababu ulikuwa ni wa kulazisha kwa kutumia tyranny of thte majority. Wananchi hawawezi kulazimishwa kuitii tume ambayo hawaamini ni halali. Tume kupitishwa na kuundwa hakuipi uhalali (legitimacy) kwani uhalali wa sheria hauji kwa kupitishwa tu bali pia kwa uhalali wa hoja zake na mantiki yake. Mwanadamu hawezi kulazimishwa kutii kitu ambacho ni kinyume na dhamira yake, ukweli na mantiki yake au kile ambacho kinaonekana kwa makusudi kimetengezwa ili kumkandamiza.
Wanaoamini kuwa sheria hii ni halali na kuwa mchakato ni halali wanayo haki ya kujitokeza kwa furaha kwenda kutoa maoni yao. Wale ambao wanaamini mchakato huu umesurp power ya wananchi na kuwa umelazimishwa wanayo haki ya kukaaa kushiriki na kuhamasishana kutoshiriki hadi hoja zao zisikilizwe vinginevyo wanalo jukumu la kuhakikisha kuwa itakapokuja kura ya maoni wataenda na kuhamasishana kupigia kura ya "hapana" hiyo referendum na kuzuia Katiba Mpya itakayopitishwa na wana CCM.
Wanaweza kukataa kusikiliza maoni juu ya mchakato na wanaweza kabisa kulazimisha watu waje kwenye tume yao lakini watakapoletwa swali hilo kwa wananchi hawana namna ya kuwazuia wale wasioshiriki mjadala kupiga kura ya hapana. Unless waseme watakaopiga kura ya maoni ni WALE TU walioshiriki kwenye kutoa maoni! Kitu ambacho hakimo kwenye mswada huu hadi waufanyie mabadiliko.
hapana ni kwamba ana maoni tofauti na kuwa anaamini maoni yake ni sahihi. Ni jukumu letu kuonesha kuwa maoni yake si sahihi. Mtu kuwa na maoni tofauti haina maana ni mnafiki.