Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Kanuni ya Kuu ya Kwanza kwa mwanahabari yoyote ni to tell nothing but the truth. Naomba kuitumia kanuni hii kuwaambia Chadema, they were wrong!, walikosea!. Ukikosoa makosa yoyote, toa na mapendekezo ya kurekebisha makosa hayo. Hivyo Chedema kwanza wakiri makosa, pili wakubali yaishe na mwisho, wakubali kusonga mbele, 2015 sio mbali kihivyo!.
Mchelea mwana kulia, hulia yeye, japo binafsi ni kada wa chama cha siasa, bali pia ni mkereketwa wa demokrasia ya kweli ya vyama vingi ndani ya bunge, hivyo wapenzi wote wa dhati wa demokrasia, lazima waikubali Chadema kama ndicho chama pekee cha upinzani Tanzania bara kilichoonyesha nuru ya matumaini ya uwezekano wa kupatikana kwa demokrasia ya kweli ndani ya bunge na labda hata ukombozi wa pili wa Mtanzania baada ya uhuru na miaka 50 ya utumwa wa chama kimoja kuhodhi madaraka yote ya dola.
Wengi wa wapenzi wa demokrasia wanaishabikia mno Chadema wakichelea kuiambia ukweli kuwa watalia, mimi nachelea mashabiki na wapenzi wao kulia mwaka 2015, hivyo nawaambia ukweli ili hata kama mtalia, lakini itakumbukwa mliambiwa!.
Suala la kususia jumla mchakato wa kuunda tume ya kukusanya maoni kuunda katiba mpya ni kosa kwa sababu Chadema kama kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ilikuwa na uwezo wa kuusimamisha na kuzuia uwasilishwaji kwa mara ya pili huo muswada kwa kutumia kanuni ya kifungu 86 hivyo kutoa fursa ya hoja ya kuzuia uwasilishwaji huo kusikilizwa, lakini Chadema haikufanya hivyo.
Hakuna ubishi kuhusu uwezo wa wabunge wa Chadema katika umakini, kitendo cha oversight ya opportunies provided by kifungu cha 86 cha kanuni za bunge kuuzuia huo muswada, sio tuu ni udhaifu mkubwa, but kosa kubwa ambalo Chadema lazima wakiri, waombe radhi na kusonga mbele.
Kanuni hiyo ya 86 inaeleza wazi hatua kwa hatua za kufuatwa ili kuuzuia muswada usisomwe kwa mara ya pili. Chadema ilipuuza na kuendelea kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani.
Kama Chadema ingezingatia kanuni hiyo, isinge wasilisha maoni ya kambi ya upinzani bali ingewasilisha pingamizi!.
Kitendo cha Mhe. Lissu kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani, yamemaanisha wameijibu hoja ya serikali hivyo kutoa go ahead majadiliano yaendelee. Uwasilishwaji wa hotuba hiyo ndio passport ya mjadala kuendelea, kama kambi ya upinzani wasingewasilisha maoni yao, muswada ungesitishwa kwanza na wao kusikilizwa. Hivyo iwasilishwaji wa hotuba ile ni kosa la pili, Chadema lazima wakiri kosa, waombe radhi na kusonga mbele!.
Kitendo cha kususia mjadala kwa siku ya kwanza na kutoka nje, was the right move kuonyesha protest dhidi ya unyanyasaji wa Mhe. Spika, lakini kuisusa hoja jumla, was a mistake hivyo sheria imetungwa bila imput yao, hivyo hili ni kosa la tatu, Chadema wakiri kosa, waombe radhi na kusonga mbele!.
Nimebahatika kuhudhuria mdahalo wa Star TV kuhusu Tanzania tuitakayo ambapo Mhe. Tindu Lissu ilikuwa ni mdahiliwa, na nilipata fursa ya kuuliza swali kuhusu kanuni ya 86 lililokuwa na vipengele a, b na c
(a) Kanini hawakitumia kanuni ya 86 kuuzuia muswada usisomwe?.
(b) Kwanini waliwasilisha hotuba ya maoni ya kambi ya upinzani yaliyotoa passport mjadala uendelee badala ya kuwasilisha pingamizi ambayo ingeusimamisha mjadala?.
(c) Chadema wamesusa sheria imepitishwa, jee wamefaidika na nini na kususa kwao?.
Mhe. Lissu amepiga chenga kutoa majibu ya kina kwa kujibu
(a). Amenisomea hitimisho la hotuba yake. Kanuni ya 86 ilimtaka Mhe. Lissu awasilishe pingamizi na sio hotuba!.
(b) Amepiga chenga kueleza ni kwanini amewasilisha hotuba badala ya pingamizi!.
(c) Wananchi wanaelewa ni nani mtetezi wao wa ukweli.
Kwa vile sheria imepitishwa na itasainiwa na rais kwa mbwembwe, lazima Chadema na wapenzi wao na mashabiki wao waukubali ukweli mchungu kuwa they lost the battle hivyo watake wasitake, lazima wakubali matokeo. Hawawezi kuendelea kususa, lazima wajisibmit kwenye tume ya kuratibu maoni na kutoa maoni yao hata kama tume hiyo itaundwa bila imput yao na bila ridhaa yao!.
Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo (Tume ya kukusanya maoni) na yajayo (Katiba Mpya).
Namalizia kwa kusisitiza, kufanya kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa!. Chadema kwenye uundwaji tume mmefanya kosa!. Sheria imetungwa na sasa sio kosa tena, kosa ni kurudia kosa kama hamtoa maoni yenu kwenye tume!. Two wrongs don't make right, better late than never!.
2015 sio mbali kihivyo!.
Wasalaam
Paskali
Update 1.
Update-2.
Pasco was right on CHADEMA

Wanabodi, baada ya taarifa hii, haswa hoja number 1
Kwa vile hoja kuu ya msingi ya mada yangu ni kuwa Chadema, hawakuupinga muswada ule, taarifa ya M/Kiti Chadema anapongeza kwa kuupinga, nawaombeni kwa heshma na taadhima, sasa tusitishe huu mjadala kama heshima kwa viongozi wakuu wa Chadema.
- Kamati Kuu imewapongeza wabunge wote wa CHADEMA kwa hatua thabiti na sahihi walizochukua, kwa niaba ya wananchi wa Tanzania, kupinga Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 kusomwa kwa mara ya pili
Naomba sasa kukubali kuwa Chadema waliupinga huo muswada ili yaishe, walionielewa mmenielewa, msio nielewa samahanini sana tutakuja kuelewana mbele ya safari.
Paskali
Update-2.
Update-3.kweli yaishe kwa sababu wewe uliwategemea CDM badala ya kuwategemea CCM ambao ndio walikuwa na uwezo wa kuzuia mswada huu na hawakufanya hivyo. Angalau tunafarijika kujua kuwa CDM walitoa msimamo wao kuonesha mapungufu ya mswada na wakaukataa kwa vitendo livyo dhahiri - kwa kutoka nje. CCM waliobakia ndani wangeweza kubadilisha au kuukataa hawakufanya lolote wakabakia kupigiana makofi. Hawa ndio wa kuwasikitikia. Bahati mbaya huoni tatizo kwa CCM kupitisha mswada mbovu wakati wale unaowaita ni "wabunge makini' waliposhindwa kutumia kanuni ile ile ya 86:3b. Hata mimi nakubali yaishe maana kama CCM waliopitisha mswada kwa mbwembwe walitarajiwa waunge mkono CDM basi inatosha siku kuwa vituko.
Update-4Mkuu Mkandara, huu mjadala tulishaufunga kwa closing points za Mzee Mwanakijiji nami niliafiki tuufunge. Lakini kwa vile lengo ni kuelimishana, naomba niweke hapa majibu yangu in points form, huenda na wengine wasio nielewa wakanielewa hivyo hii itakuwa ni closing nyingine.
1. Uwasilishaji wa miswada bungeni is a process ambayo huanzia hatua ya kwanza mpaka hatua ya mwisho. Hatua hizo zimeainishwa katika kanuni za kudumu za bunge, tolea la mwaka 2007.
2. Katika process hiyo, kanuni zinatoa muongozo, ni wakati gani mbunge anaweza kufanya jambo gani na wanakuwekea mpaka maneno ya kutumia.
3. Pia kanuni hizo zinatoa muongozo kwa spika, ni wakati gani ataruhusu hoja, pingamizi au miongozo, na kumueleke muswada ukishafikia stage fulani on the process, kunakuwa hakuna tena kuhoji, maswali wala kupokea hoja yoyote ili kuikamilisha process nzima.
4. Muswada huu ulipoletwa kwa mara ya kwanza, ile mwezi April, uliwasilishwa na kupokelewa rasmi na bunge, ambalo lilitoa maelekezo kuwa muswada urudishwe serikali, ufanyiwe a,b,c, na d, halafu uletwe tena kwenye kamati.
5. Kamati ilipewa majukumu ya kukusanya maoni zaidi ya wananchi na kujumuisha maoni hayo.
6. Kilichofanyika, ni serikali iliuchukua huo muswada na kuufanyia marekebisho bila kuihusisha kamati ya bunge!. Ikumbukwe, muswada wa serikali, ukishawasilishwa kwa mara ya kwanza bungeni, ownership ya muswada husika inachange hands toka kwa serikali kwenda kwa bunge, hivyo sasa wanaoumiliki ni bunge, serikali inapokeo maelekezo ya bunge nini kifanyike hivyo hoja ya Mhe. TL ni valid kuwa serikali imefanya mabadiliko katika ule muswada wa kwanza ambao ndio ulitakiwa kuletwa na kusomwa kwa mara ya pili, lakini kilicholetwa sasa sio ule ule muswada wa awali, bali serikali imeleta muswada mpya ambao ulipaswa kuwasilishwa kwa mara ya kwanza na sio mara ya pili, na hapa ndipo jukwaa la katiba na wanaharakati walichotaka.
7.Kuanzia hapa sasa Mkuu Mkandara, naomba sasa ndio nikulete kwenye kanuni 86 kifungu cha 3.
(3) Haitakuwa halali katika hatua hii kuleta hoja ya kufanya
mabadiliko katika hoja isipokuwa tu kwamba:- ( Kanuni inatamka wazi kuweka zuio kwa spika kuruhusu hoja yoyote, hivyo alikuwa right kumzuia Mnyika, Kafulila au yoyote, unless otherwise hii inayofuatia,
(a) mabadiliko bila kutoa sababu yanaweza kutolewa
kwa kusema:
"Kwamba, Muswada huu usisomwe mara ya Pili
sasa na badala yake usomwe baada ya &[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];..
kuanzia &[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];..", na hapo muda ambao Muswada
huo unaokusudiwa kusomwa utatajwa.
Hapa ndipo ulipopotea Mkuu Mkandara, hapa hapano hoja kwangu kwa vile hili ni pingamizi tuu la kuomba bunge liusiupokee muswada husika siku hiyo na badala yake kuomba liupokee siku nyingine, kwa case yetu, this is immaterial.
(b) mabadiliko yenye kutoa sababu yanaweza
kutolewa kwa kusema:
"Kwamba, Bunge hili likatae Muswada huu
Kusomwa
Mara ya Pili kwa sababu zifuatazo &[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];.", na hapo
sababu za kupinga Muswada Kusomwa Mara ya
Pili zitatajwa kwa ukamilifu.
Hapa ndipo mimi niliposimamia kwenye hoja yangu mwanzo mwisho!. Maneno hayo ndio Mhe. Tundu Lissu alitakiwa ayaseme ili kuweka pingamizi kwa muswada huo, usisonge mbele. Hli ndilo pingamizi rasmi kwa mujibu wa kanuni. Baada ya kuweka pingamizi hili, Spika lazima alisikilize na kuzikiliza sababu za pingamizi hili, na hapa ndipo Mhe. Lissu alitakiwa kutoa sababu ni kwa nini wanapinga.
Nilieleza kuwa kama ni kweli, Lissu aonyesha contrast kati ya ule muswada wa awali na huu mpya, na kuwafungua macho wabunge kuwa huu ni muswada mpya kabisa, wabunge wangeelewa na wangewaunga mkono.
Mimi ni mhudhuriaji mzuri wa bunge, mule bungeni kuna wabunge makini ambao ni vichwa vya ukweli, wangedhibitishiwa huo upuuzi wa serikali, wangewaunga mkono Chadema, ingawa pia lazima nikiri, bunge hili pia limeshehenezwa wabunge kibao ambao ni vichwa maji, vichwani ni watupu kabisa lakini ni mahodari sana kupiga kele kama lilivyo debe tupu. Ili hoja za kipuuzi puuzi kupitishwa, serikali kupitia vikao vya wabunge wa vyama, party causes, hukaa na wabunge wao kuwaambia lazima waunge mkono hoja za serikali, na huwategemea sana hawa madebe matupu kuzipigia tarumbeta.
Nilimuhakikishia Mzee Mwanakijiji, kuwa suala la katiba ni suala la kitaifa, hivyo kama hoja za TL zilikuwa na mashiko kwa maslahi ya taifa, wabunge vichwa wa CCM, wangewaunga mkono wapinzani. Mbona kuna baadhi ya miswada ya serikali iliwahi kupigwa chini, ukiwemo ule wa baraza la usalama la taifa na serikali kujikuta imelazimika ku withdraw
Mkuu Mkandara, hapa ndipo niliposimamia kuwa hakuna pingamizi lolote lililowasilishwa, kama TL au mbunge yeyote angewasilisha hilo pingamizi, then hiki ndicho kingefuatia
(4) Iwapo hoja itatolewa chini ya fasili ya 3(a) na (b) ya Kanuni hii,
Spika atalihoji Bunge ili kufikia uamuzi.
8. Kwa kuwa hakuwa na pingamizi lolote rasmi kuhusu muswada huu, process iliendelea kwa
(5) Mwenyekiti wa Kamati iliyopelekewa Muswada wa Sheria au
Mjumbe mwingine wa Kamati aliyeteuliwa kwa ajili hiyo, atatoa
maoni ya Kamati kuhusu Muswada husika.
Hapa ndipo mwenyekiti wa kamati ya Lissu (Sheria na Katiba) Mhe. Pindi Chana (pia ni kichwa!), aliwasilisha maoni yake
Ikumbukwe, baada ya kukosekana pingamizi rasmi, ile kanu bado inamlazimisha spika kutoruhusu hoja yoyote, pingamizi lolote wala muongozo wowote!
9. Baada ya hapo ndipo ikafuatia
(6) Ikiwa Muswada wa Sheria unaohusika ni Muswada wa Serikali,
basi Msemaji wa Kambi ya Upinzani atatoa maoni yake juu ya
Muswada husika na endapo ni Muswada Binafsi au Muswada wa
Kamati, basi msemaji wa Serikali atatoa maoni yake.
Hapa ndipo Mhe. TL aliposoma hotuba yake, nawaombeni sana tuwe waangalifu zaidi, muda wa pingamizi ulishapita sasa ni maoni, hivyo anachokisema Mhe. Lissu ni maoni tuu, hata kama katika maoni hayo, atatamka matamshi ya kupinga, maoni ni maoni (opinion) hayasitishi kitu, hayasimamishi kitu, hayazuii kitu, ndio maana mimi nililalamika kwanini hawakuupinga rasmi muswada huu?.
Hoja kubwa ya Mwanakijiji kutetea kutowasilisha pingamizi, ni eti wangepinga wangeshindwa kwenye kura za kulihoji bunge, hivyo wakaamua bora waendelee, mimi nikasisitiza that was a mistake!
Ikumbukwe lile zuio linalomtaka spika kutoruhusu hoja zozote, swali lolote wala muongozo wowote, bado lipo.
10. Kama mtakumbuka, hapo mwanzo nilisema hii ni process na inakamilishwa kwa hotuba ya kambi ya upinzani. Kanuni inasema ili muswada wa serikali upite, lazima upate maoni ya kambi ya upinzani ku complete the process. Nikauliza, kama Chadema, ambacho ni chama makini cha upinzani, kinaupinga muswada huu, kwanini hakikuwasilisha pingamizi?, watetezi wake wakajenga hoja za utetezi. Nikauliza Tena na hili ndilo swali langu la pili kwa Lissu, Kama ni kweli mnapingwa kuwasilishwa kwa muswada huo, kwa nini mmetoa maoni ambayo ndio yanahitimisha process, nilisema Lissu alipiga chenga, nikawaambia hotuba ile ndio the missing link to complete the process.
Ingawa kanuni haitamki wazi nini kingefanyika iwapo kambi ya upinzani itasita kutoa maoni yake, kwa vile hii ni process, nikasema bila maoni hayo, muswada huo usingeweza kujadiliwa kwa sababu maoni ya kambi ya upinzani ni pre-requisite kwa muswada wa serikali kusonga mbele!.
Baada ya Hotuba ya TL, wakina Nyika na Kafulila etc wanasimama kuomba muongozo wa spika!, wanaomba muongozo wa nini at this stage wakati kifungu kinamlazimisha spika kutoruhu chochote!.
Hitimisho.
Mkuu Mkandara, kwa maoni yangu, kutowasilisha pingamizi was a mistake, kusoma hotuba ya TL was another mistake na at the end of the day sheria imetungwa we've lost!
Kwenye hoja yangu ya msingi nimesema, baada ya sheria kusainiwa, no one can do anything, sio Chadema wala wanaharakati.
Nashukuru taarifa ya M/k wa Chadema jana kuwa sasa wanakubali yaishe, wanamtafuta JK kuongea nao ili serikali iwasikilize. Naomba niwadokolee kitakachofuata. Waungwana watamshauri JK kukutana na Chadema kuwasikiliza, rais JK japo ni mtu wa smilling face, in reality ni very arrogant!. Mimi nilizishuhudia his true colors siku ile alipohutubia Wazee wa Dar es Salaam kuzua mgomo wa wafanyakazi!. Hivyo JK, kamwe hatakubali kuwaona Chadema mpaka baada yakusaini muswada ule kuwa sheria, kuwaona kabla ni ku bow down, something he will never do!, nilimuona akibow down wakati wa kuomba kura tuu, never again on anything else, labda akiwa kwenye zile trips za kutembeza bakuli!, but not to Chadema!.
Naomba tusiendelee kulijadili hili, mjadala huu umeshafungwa, ila tuendelee kuelimisha tuu, sio kubishana!.
Paskali
Update-5.Huu mjadala nimejifunza mengi sana sana na naona ndiyo umefikia mwisho.
Pasco, ungelikuwa Mwalimu basi ungelikuwa unawasha Debate kali sana darasani hadi wanafunzi wanataka kupigana. Sijui enzi zako kama kulikuwa na mtu anakushinda mara mkianza kubishana/debate darasani au kijiweni.
Huu si mjadala wa kwanza kuuweka hapa. Kila mjadala huwa unazusha majadiliano makubwa sana na hapo vifungu vya kanuni, sheria na katiba humwagika kwa wingi. Sijui kama unafanya makusudi ili kutusaidia na sisi wavivu wa kusoma sheria au kwa kweli huwa unabisha, ila ukweli ni kwamba wengi sana tumefaidika na makala hii.
Nawalaani wote waliokuja na kuporomosha matusi kwako na kuanza kukuita majina ya ajabu ajabu. Wanasahau kuwa ni ubishi/udadisi wako/ugumu wako ndiyo umesababisha tumeona mistari mingi namna hiyo. Kwa bahati mbaya sana, kuna wengine wamedandia gari lako kama kawaida ili kuanzisha ligi na Chadema ila nimefurahi kuwa watu wamewadharau hata kuwajibu wameacha. Hii makala ukiacha wapuuzi fulani wachache kutoka Chadema/CCM, kweli imeenda shule na kwa wale watakaotaka kukielewa hicho kifungu cha 86 cha kanuni, basi nafikiri hii makala imeelezea kwa undani sana. Kwa hilo Pasco kwa mara nyingine tena kutoka thread mbili tofauti nasema ASANTE SANA.
Nawashukuru wote waliochangia kama the real GREAT THINKERS wa JF na bila ushabiki wa chama chochote cha Kisiasa Tanzania. Namshukuru tena Pasco kwa majadala mzuri kama huu na wote waliojaribu kumjibu kwa kutumia njia mbalimbali ili kumuonyesha Pasco kuwa ameelewa vibaya. Pasco, nasubiri kwa hamu sana mjadala mwingine (wengine wameita ligi) ambao nina uhakika nao utawasha moto hapa JF huku wale Washabiki wa vyama wakiachwa kando bila watu kujali sana wameandika au wamesema nini. Ningelikuwa Mods, nakuwa napita na kuzifuta makala zao ili kupisha mtitiriko mzuri. NOYAGA!!
Pasco was right on CHADEMA
Kwasababu madai ya Pasco yalikuwa ni kwanini CDM hawaku exhaust ile procedure ya kupinga muswada kwa kutumia kifungu cha 86,nimeona kama madai yake kuhusu hiyo mistake ya CDM ni ya ukweli kwakuwa wapenzi na wanachama wa CDM walipingana naye kwa kusema mwishowe Speaker ndiye mwamuzi kwani anaweza kuitisha upigaji kura miongoni mwa wabunge,na kwasababu wabunge wa CCM ni wengi zaidi,basi waka assume kuwa hawatafika mahali...Pia kuna waliosema ni jambo ambalo lilishawahi kutokea huko nyuma.
Swali linakuja,je hakuna nyakati ambazo upinzani umefanya kikao na rais?CUF walishawahi kuwa na viao vya aina hiyo pia wakati wa Mkapa...
Kwa upande mwingine,CDM wameomba kuonana na Mh Rais,je hilo lina tofauti gani na situation iliyopita ya kujaribu kuupinga muswada bungeni pale walipokuwa na opportunity hiyo bila kujali kama watafanikiwa ama la?Given ukweli wa wazi kabisa kuwa JK hawezi kula matapishi yake?
Je kama ni kweli kuna wapenzi wa CDM humu wanadai kuwa hata akikataa basi CDM itatumia nafasi hiyo kuwaambia wananchi kuwa tulimwambia ila "akaweka pamba masikioni"
Je kwanini hawakutumia standards hizo hizo wakati walipokuwa bungeni ili waje kuwaambia wananchi kuwa tulimwambia spika na bunge lakini "wakaweka pamba" masikioni?
Mimi siendi all the wa kuwaambia kwamba mkubali yaishe kama Pasco alivyosema, kwamba muwaachie CCM waandae utaratibu wa kupata katiba mpya,however nakubaliana na Pasco kwamba that was a mistake.
Kama nikizichukulia hizi issue within the same standards,then ni kweli CDM walikosea.
So Pasco was definetly right...
Kama walijuwa hoja yao haitashinda bungeni, ni nini kinawafanya wadhani kuwa itapita kwa Rais?
Ni vigezo gani?Binafsi siamini kabisa kuwa Rais atabadili mawazo kwenye kikao hicho,just kama vile ambavyo wao hawakuamini kwamba hoja yao itafanikiwa bungeni, kwani whats the diference?