Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Kilichofanyika na Tundu Lissu kimezaa matunda ya mbegu zile zilizopandwaBaada ya hotuba ya TL, mjadala uliendelea. Safi kabisa. Lakini walichofanya wabunge waliobaki kujadili kilionyesha ni kwa kiasi gani TL alifanikiwa na kambi yake ya upinzani. Hawakuweza kujadili mswada badala yake walijadili hotuba ya TL. Umeona. Hizo ni Mbinu za wanyama wenye akili wanavyojielekezea fikra ili wanyama wengine wakali wasiwaumize watoto wao.Wananchi wameona jinsi gani wabunge wa ccm na tanzu zao walivyo na uwezo mdogo. Hii haina tofauti na kichaa anapofukuzwa na mzima, wazima wengine watamchukulia mzima kuwa kama kichaa. Kwa maana nyingine waliunga mkono hotuba ya Lissu na sio mswada.
 
MM na FJM heshima sana kweni. Absolutely brilliant contributions with exceptional insight and analysis.

Mijadala kama hii ina faida sana. You're the peak of the bunch!
 
MMM na FJM heshima sana. Your contributions with exceptional insight and analysis really made my day
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
MAAMUZI YA KAMATI KUU YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA MPYA.


Kamati Kuu ya CHADEMA katika kikao chake maalum kilichofanyika siku ya Jumapili, tarehe 20 Novemba 2011 katika Ukumbi wa Hoteli ya Mbezi Garden, Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine, kimepokea na kujadili kwa kina taarifa ya majadiliano na kupitishwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011. Aidha, Kamati Kuu imejadili kwa kina hatua za kuchukua baada ya Serikali, kupitia wabunge wa CCM, kulazimisha kupitishwa bungeni kwa Sheria hiyo bila kuzingatia maoni ya Wananchi na wadau wengine mbalimbali. Baada ya kuyatafakari mambo haya kwa kina, Kamati Kuu imeazimia yafuatayo:

  1. Kamati Kuu imewapongeza wabunge wote wa CHADEMA kwa hatua thabiti na sahihi walizochukua, kwa niaba ya wananchi wa Tanzania, kupinga Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 kusomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa Bungeni bila ya wananchi kushirikishwa kwa ukamilifu kutoa maoni yao na muswada kuboreshwa kwa kuzingatia muafaka wa kitaifa. Kamati Kuu imewapongeza wabunge wa CHADEMA na wale NCCR Mageuzi kwa kususia vikao vya Bunge vilivyojadili na kupitisha Sheria hiyo kwani kushiriki kwao kungeipa uhalali wa kisiasa na kijamii Sheria ambayo haikuzingatia nia na haja ya dhati ya kuweka utaratibu wa kisheria utakaoiwezesha nchi yetu kupata Katiba Mpya yenye kuzingatia na kukidhi matakwa ya umma wa Watanzania;

  1. Kamati Kuu imezingatia kuwa Sheria iliyopitishwa na Bunge ina mapungufu mengi na ya kimsingi ambayo hayatajenga muafaka wa kitaifa juu ya Katiba Mpya na hayataleta mabadiliko yoyote ya kimsingi ya Katiba:

  1. Mchakato wa kuipitisha Sheria ndani ya Bunge ulikiuka Kanuni za Kudumu za Bunge kwani Muswada uliosomwa mara ya kwanza Bungeni sio ulioletwa Bungeni kusomwa mara ya pili na baadae kupitishwa; Kamati ilizuiliwa kukusanya maoni ya wananchi katika mikoa na maeneo mbali mbali; Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano aliingilia kazi na majukumu ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ikiwa ni pamoja na yeye mwenyewe na baadhi ya wajumbe wa CCM kukusanya maoni nje ya utaratibu wa Kamati na baadae kuingiza wajumbe wengine wa CCM na CUF kwa lengo la kupitisha matakwa ya CCM na Serikali ndani ya Kamati bila kuushirikisha wananchi kwa ukamilifu;

  1. Sheria inampa Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mamlaka makubwa ya kuunda Tume ya Katiba na Sekretarieti yake ambayo sio tu itakusanya maoni ya wananchi na kuandaa ripoti, bali pia ndiyo itakayoandaa na kuandika Rasimu ya Katiba Mpya na kusimamia mchakato wote wa wananchi kuijadili na kuipitisha katika Bunge la Katiba;

  1. Sheria inampa Rais na Mwenyekiti wa CCM mamlaka makubwa sio tu ya kupokea ripoti ya Tume ya Katiba bali pia ya kuifanyia mabadiliko ambayo yeye na Serikali yake wataona yanafaa kwa kutumia taratibu za kiserikali za kutunga sheria;

  1. Sheria inampa Rais na Mwenyekiti wa CCM mamlaka makubwa ya kuliitisha tena Bunge la Katiba kwa lengo la kufanya mabadiliko kwenye Katiba Mpya endapo litapitisha Katiba Mpya ambayo yeye Rais, au Serikali yake, au chama chake wataona hailindi maslahi yao;

  1. Sheria inaunda Bunge la Katiba ambalo litakuwa na Wajumbe hadi 400 wa CCM kati ya wajumbe 545 wa Bunge la Katiba. Idadi hii ya wajumbe itaiwezesha CCM kupata theluthi mbili ya wajumbe wanaohitajika chini ya Sheria hii ili kupitisha jambo lolote katika Bunge la Katiba na kwa hiyo Katiba Mpya itakuwa ni ile inayolingana na matakwa na maslahi ya CCM na itakuwa mpya kwa jina tu;

  1. Sheria inatoa nafasi kubwa kwa Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM na vyombo vya uwakilishi vya Zanzibar kushiriki kutunga Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano kinyume na Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 na Katiba ya sasa ambayo imevipa mamlaka ya kutunga Katiba ya Jamhuri ya Muungano vyombo vya Muungano kama Serikali na Bunge ambako Zanzibar ina uwakilishi wa kutosha;

  1. Sheria inahakikisha kwamba muundo wa sasa wa Muungano wa Serikali hautaguswa bali utadumishwa na kutiliwa nguvu licha ya madai ya miaka mingi ya wananchi na mapendekezo ya Tume za Kiserikali kwamba muundo wa Muungano uwe ni wa Serikali tatu;

  1. Sheria inaipa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyoteuliwa na Rais na Mwenyekiti wa CCM mamlaka ya kusimamia mchakato mzima wa kura ya maoni ya kuipa Katiba Mpya uhai wa kisheria. Tume ya Taifa ya Uchaguzi haina uhuru na imeshindwa mara nyingi kusimamia chaguzi huru na haki katika nchi yetu na haiwezi kusimamia kura ya maoni kwa uhuru unaohitajika;

  1. Kamati Kuu ya CHADEMA imesisitiza siku zote kwamba mchakato wa kupata Katiba Mpya unahitaji mwafaka wa kitaifa ambao utazingatia maoni mapana ya makundi mbalimbali ya kijamii. Kamati Kuu inasikitishwa na hatua za makusudi za kufifisha juhudi zote zilizofanyika na wadau mbalimbali katika kufikia mwafaka wa kitaifa juu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Aidha, Kamati Kuu imesikitishwa na upotoshaji wa makusudi wa hotuba ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni uliofanywa na wabunge wa CCM na CUF, wakiongozwa na Spika wa Bunge, Anna Makinda, kuhusu msimamo wa CHADEMA juu ya Muungano;
  2. Kamati Kuu inasisitiza kwamba njia pekee ya kuunusuru Muungano wetu ni kwa wananchi wa pande zote mbili kupiga kura ya maoni kuamua kwamba wanataka kuendelea na Muungano na kama jibu ni ndio, muundo gani wa Muungano huo wanaoutaka. Aidha, Kamati Kuu inarudia msimamo wa CHADEMA kwamba ili kuondoa kero na malalamiko ambayo yameuandama Muungano wetu tangu kuzaliwa kwake, muundo unaofaa ni wa Serikali tatu kama ilivyopendekezwa pia na Tume ya Nyalali mwaka 1991 na Tume ya Kisanga mwaka 1998;

  1. Kamati Kuu inaamini kuwa pamoja na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kupitishwa, bado kuna fursa za kisiasa na kijamii katika kujenga mwafaka wa kitaifa juu ya haja, nia, mchakato na misingi ya Katiba Mpya. Hata hivyo, Kamati Kuu imeshangazwa na kusikitishwa na uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete wa kutozitumia fursa hizo na badala yake kujiingiza katika jalala la taka za upotoshaji uliofanywa na Wabunge wa chama chake juu ya misingi na maudhui ya Sheria hiyo. Kamati Kuu inaamini kwamba badala ya kuwaunganisha Watanzania na kujenga muafaka unaohitajika katika mchakato wa Katiba Mpya, hotuba ya Rais Kikwete kwa wazee wa CCM wa Dar es Salaam imezidi kuwagawa Watanzania kwa misingi ya ushabiki wa vyama badala ya kuwaunganisha kwa misingi ya utaifa;

  1. Baada ya kutafakuri mambo yote haya, Kamati Kuu imeazimia yafuatayo:

  1. CHADEMA itaendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau wote juu ya ubovu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na juu ya haja ya kuwa na sheria itakayoweka utaratibu bora zaidi wa kuunda Tume Shirikishi ya Katiba kwa lengo la kukusanya maoni ya wananchi, kuandaa ripoti na Rasimu ya Katiba Mpya, Bunge Maalum la Katiba na usimamizi wa kura ya maoni itakayowezesha wananchi kufanya maamuzi kwa uhuru na kwa haki;

  1. Ushiriki wa CHADEMA katika mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya uliowekwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba utategemea utayari wa Serikali ya Rais Kikwete kufanya mabadiliko makubwa na ya kimsingi katika sheria hiyo kwa lengo la kujenga muafaka wa kitaifa juu ya mchakato huo;

  1. Kamati Kuu inawaagiza wabunge na viongozi wote wa chama katika ngazi zote kufanya mikutano ya ndani na ya hadhara yenye lengo la kuwaelimisha wananchi juu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na madhara yake kwa mchakato wa kupata Katiba Mpya na bora kwa nchi yetu kwa lengo la kuunganisha umma wa watanzania kuweza kufanya mabadiliko ya msingi;

  1. Kamati Kuu inaamini kwamba uamuzi wa Serikali ya CCM kulitumia Jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya hadhara na maandamano ya amani ya wananchi wanaopinga mchakato uliopitishwa kuwa Sheria sio tu ni kwenda kinyume na haki za kimsingi za kikatiba bali pia unahatarisha moja kwa moja amani, utulivu na umoja wa nchi yetu. Kamati Kuu inasikitishwa na msimamo huu wa Serikali ya CCM kwani unashindwa kutambua ukweli kuwa matumizi ya nguvu za dola hayajawahi kuokoa serikali za kidikteta kuondolewa madarakani na Katiba Mpya kupatikana katika nchi mbali mbali duniani na katika Bara la Afrika;

  1. Kamati Kuu inasisitiza kwamba CHADEMA itaendelea kutumia njia zote za amani, ikiwemo mikutano ya hadhara na maandamano kama ilivyoainishwa na Katiba na sheria husika za nchi yetu kuunganisha nguvu ya umma kupinga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na mchakato wake utakaopelekea Tanzania kutopata Katiba Mpya na bora;


Freeman A. Mbowe (MB)
MWENYEKITI WA TAIFA

Novemba 21, 2011
Mimi nawapongeza chadema kwa kazi nzuri wanayofanya kwani bila kuhoji baadhi ya Mambo tungekuwa bado gizani!!!
Kwa mtanzamo wangu najua hata wabunge wa CCM hawana imani na utendendaji wa Rais Kikwete na ndiyo maana wanataka kumuondoa katika nafasi ya Uenyekiti Taifa!!!

Naomba wananchi kokote mliko ondoeni uoga tuseme kweli!!!
Hapa sio madaraka makubwa aliyopewa Rais Kikwete lakini ni uadilifu wa JAKAYA MRISHO KIKWETE sio Mzuri kabisa!!

Je ,Kwenye sakata hili la katiba , angepewa madaraka hayo SLAA wananchi wangelalamika ???
Je , angepewa Mwakyembe ,au Mangufuli, au Shivji wananchi Wange lalamika??
Angalia mawazo ya SALIMU ,KITINE, WARIOBA je, Kunatatizo???

Angekuwa Nyerere Kuna tatizo ???

Hapa Kikwete kama kikwete anapaswa kujua kuwa Wananchi hawamtaki kutokea ndani ya CCM ,serikali hadi upinzani !!!

Hata hao CUF nao hawamtaki Kikwete angalia tayari ndani ya CUF kumetokea mpasuko wa Kutaka kumutoa SEIF issue kubwa ni Ndoa ya Mkeka!!!

Nataka Watanzani wote tujadili mambo ya maana kuwa , Kikwete hawezi kusimamia mchakato wa Katiba mpya bali atafutwe mtu mwingine!!!

Jambo hili linajulikana hata ndani ya CCM!!!

Hofu iliyopo ndani ya CCM ni Mchakato wa kumupata mgombea Urais Mwaka 2015, wanajua Kikwete hawezi kusimamia sasa kama hawezi kusimamia Mchakato wa Kumupata mgombea ndani ya CCM anaweza kusimamia mchakato wa Katiba mpya unao husisha vyama vyote???

Tafakari !!! uwe mkweli!!! Ogopa MUNGU!!!! Usijilimbikizie Mali!!! kumbuka kunasafari ya kwenda India!!!

 
Mwalimu, sio Chadema tuu, ni mbunge yoyote, kwa vile CUF wana ndoa yao na CCM, usitegemee lolote kutoka kwao!.

Mrema wa TLP na Cheyo wa UDP wote hawa ni spent force, hivyo hope ikabaki kwa Chadema na NCCR-Mageuzi, wale vijana wali bank on Chadema kwa sababu ndio kambi rasmi ya upinzani!.

Kama usemayo ni kweli kuwa vyama vyote vya upinzani ni hopeless isipokuwa chadema na nccr huoni kuwa hapa walikuwa wanapambana na nguvu isiyo ya kawaida? Manake ni CHADEMA VS CCM+CUF+UDP+TLP!! Endapo wangefanya kile unachoshauri unadhani probability ya kufanikiwa ungewapa asilimia ngapi? Kama ni karibu na sifuri basi they were right haikuwa na maana kuhangaika kubaki mle ndani!
 
@Nguruvi3, nakubaliana na wewe kabisa kuwa CHADEMA wangetoka nje bila kusema waliyosema wananchi wasingeelewa wanapinga nini, na ingekuwa rahisi sana kwa CCM na CUF ku-spin mambo. Kwa kusoma hotuba CHADEMA wameweka kumbukumbu bungeni (bila kuchakachuliwa) na wananchi tumesikia kwa masikio yatu muswada ule una matatizo gani, na ni vipi taratibu zimekiukwa including Spika kuingilia shughuli za kamati ya katiba na sheria. CCM hawezi kupindisha mambo maana HANSARD ipo. Hili muhimu.

Pili kama unatumia dawa lakini haupati nafuu yoyote kwa nini uendelee kutumia hiyo dawa? Kama Spika amekuwa anatumia kifungu hicho hicho cha 86 (4) kuhakikisha mambo ya CCM hayaharibiki Pasco ana uthibitisho gani kuwa kungekuwa na exemption kwenye hili?

.....kwa neema nadhani. lol
 
Wanabodi,
Kanuni ya Kuu ya Kwanza kwa mwanahabari yoyote ni to tell nothing but the truth. Naomba kuitumia kanuni hii kuwaambia Chadema, they were wrong!, walikosea!, kwanza wakiri makosa, pili wakubali yaishe na mwisho wasonge mbele, 2015 sio mbali kihivyo!.

Mchelea mwana kulia, hulia yeye, japo binafsi sio mshabiki wa chama chochote cha siasa bali ni mkereketwa wa demokrasia ya kweli ndani ya bunge, hivyo wapenzi wote wa dhati wa demokrasia, lazima waikubali Chadema kama ndicho chama pekee cha upinzani Tanzania bara kilichoonyesha nuru ya matumaini ya uwezekano wa kupatikana kwa demokrasia ya kweli ndani ya bunge na labda hata ukombozi wa pili wa Mtanzania baada ya uhuru na miaka 50 ya utumwa wa chama kimoja kuhodhi madaraka yote ya dola.

Wengi wa wapenzi wa demokrasia wanaishabikia mno Chadema wakichelea kuiambia ukweli kuwa watalia, mimi nachelea mashabiki na wapenzi wao kulia mwaka 2015, hivyo nawaambia ukweli ili hata kama mtalia, lakini itakumbukwa mliambiwa!.

Suala la kususia jumla mchakato wa kuunda tume ya kukusanya maoni kuunda katiba mpya ni kosa kwa sababu Chadema kama kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ilikuwa na uwezo wa kuusimamisha na kuzuia uwasilishwaji kwa mara ya pili huo muswada kwa kutumia kanuni ya kifungu 86 hivyo kutoa fursa ya hoja ya kuzuia uwasilishwaji huo kusikilizwa, lakini Chadema haikufanya hivyo.

Hakuna ubishi kuhusu uwezo wa wabunge wa Chadema katika umakini, kitendo cha oversight ya opportunies provided by kifungu cha 86 cha kanuni za bunge kuuzuia huo muswada, sio tuu ni udhaifu mkubwa, but kosa kubwa ambalo Chadema lazima wakiri, waombe radhi na kusonga mbele.

Kanuni hiyo ya 86 inaeleza wazi hatua kwa hatua za kufuatwa ili kuuzuia muswada usisomwe kwa mara ya pili. Chadema ilipuuza na kuendelea kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani.

Kama Chadema ingezingatia kanuni hiyo, isinge wasilisha maoni ya kambi ya upinzani bali ingewasilisha pingamizi!.

Kitendo cha Mhe. Lissu kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani, yamemaanisha wameijibu hoja ya serikali hivyo kutoa go ahead majadiliano yaendelee. Uwasilishwaji wa hotuba hiyo ndio passport ya mjadala kuendelea, kama kambi ya upinzani wasingewasilisha maoni yao, muswada ungesitishwa kwanza na wao kusikilizwa. Hivyo iwasilishwaji wa hotuba ile ni kosa la pili, Chadema lazima wakiri kosa, waombe radhi na kusonga mbele!.

Kitendo cha kususia mjadala kwa siku ya kwanza na kutoka nje, was the right move kuonyesha protest dhidi ya unyanyasaji wa Mhe. Spika, lakini kuisusa hoja jumla, was a mistake hivyo sheria imetungwa bila imput yao, hivyo hili ni kosa la tatu, Chadema wakiri kosa, waombe radhi na kusonga mbele!.

Nimebahatika kuhudhuria mdahalo wa Star TV kuhusu Tanzania tuitakayo ambapo Mhe. Tindu Lissu ilikuwa ni mdahiliwa, na nilipata fursa ya kuuliza swali kuhusu kanuni ya 86 lililokuwa na vipengele a, b na c
(a) Kanini hawakitumia kanuni ya 86 kuuzuia muswada usisomwe?.
(b) Kwanini waliwasilisha hotuba ya maoni ya kambi ya upinzani yaliyotoa passport mjadala uendelee badala ya kuwasilisha pingamizi ambayo ingeusimamisha mjadala?.
(c) Chadema wamesusa sheria imepitishwa, jee wamefaidika na nini na kususa kwao?.

Mhe. Lissu amepiga chenga kutoa majibu ya kina kwa kujibu
(a). Amenisomea hitimisho la hotuba yake. Kanuni ya 86 ilimtaka Mhe. Lissu awasilishe pingamizi na sio hotuba!.
(b) Amepiga chenga kueleza ni kwanini amewasilisha hotuba badala ya pingamizi!.
(c) Wananchi wanaelewa ni nani mtetezi wao wa ukweli.

Kwa vile sheria imepitishwa na itasainiwa na rais kwa mbwembwe, lazima Chadema na wapenzi wao na mashabiki wao waukubali ukweli mchungu kuwa they lost the bettle hivyo watake wasitake, lazima wakubali matokeo. Hawawezi kuendelea kususa, lazima wajisibmit kwenye tume ya kuratibu maoni na kutoa maoni yao hata kama tume hiyo itaundwa bila imput yao na bila ridhaa yao!.

Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo (Tume ya kukusanya maoni) na yajayo (Katiba Mpya).

Namalizia kwa kusisitiza, kufanya kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa!. Chadema kwenye uundwaji tume mmefanya kosa!. Sheria imetungwa na sasa sio kosa tena, kosa ni kurudia kosa kama hamtoa maoni yenu kwenye tume!. Two wrongs don't make right, better late than never!.

2015 sio mbali kihivyo!.

Wasalaam
Pasco (wa jf).

Bwana pasco mi nadhani umekosa kitu kinaitwa spirit of revolution, na kama unayo ni ya kishabiki. Wabunge wa ccm ni weng i mara tano zaidi ya wabunge wa chadema, ukiongeza ccm B ya cuf ndo usiseme! Hawa watu kwa hali ya democrasia ya wengi wape bila hoja, wanaweza kupitisha sheria yoyote na wakati wowote. The time has come now to show them that some of the things wanatufanyia wananchi sio, kama kujichotea rasilimali na mambo mengine bila kujali umasikini wetu. Ilikuwa ni sahihi na mapambano hayajaisha. Unaposema wakubali yaishe tusonge mbele, twende wapi? Ndugu yangu njia sio safi na ina miba lazima isafishwe kwanza!
 
Pasco, unakubali kuwa kwa kutumia kanuni ya 86:3b Lissu angepewa nafasi ya kuelezea sababu za kwanini mswada ule ukataliwe na Spika angempa nafasi hiyo?
Argument ya Pasco ni kwamba hatuwezi kujuwa unless angefanya hivyo.

Sasa sijui kwanini hataki ku accept past experience one of the factor.

Ni kweli ana argument,na mjadala huu utawaacha watu kwenye mawazo waliokuwa nayo awali kila mmoja kwa upande wake anavyoona ie CDM was wrong vs whthere they were right, unless kama kuna hayo ya nguvu ya umma ku take place.
 
Miradibubu, inapotokea hoja ya msingi inamakosa, kanuni zinatamka kwanza unatoa pingamizi, hoja yangu inabaki na inasimama pale pale, Kwanini Chadema hawakutoa pingamizi?. Kanuni inasema kwanza toa pingamizi, ukishatoa pingamizi, toa sababu, kitendo cha kutoa hotuba ni kumwambia spika hatuna pingamizi, maoni yetu ni haya ... endeleeni, regardless ya content ya maoni hayo, kutungwa kwa sheria ni mchakato, yaani process, unaanzia hapa unapita hapa na hapa na hapa mpaka unafika mwisho, kwanini hawakupinga?.

Mkuu, nimefuatilia huu uzi pamoja na posts za wadau; mdau mmoja kwa jina la FJM alisema kwamba kutokana na mwenendo wa bunge hili chini ya Makinda, CHADEMA wameshawahi kupinga baadhi ya mambo hapo bungeni, lakini kutokana na wingi wa wabunge wa upande mwingine, siku zote hawakufanikiwa. Sasa kwanini katika hilo la muswada wa marekebisho ya katiba wapinge wakati hawajawahi kufanikiwa katika kupinga?

Pia Mzee Mwanakijiji, aliweka hadi hiyo kanuni ya 86 unayoizungumzia; nayo ametoa maelezo ya kutosha ya kwamba kupinga tu hakutoshi, bali kunakamilika kwa spika kuhoji bunge zima kama linaafiki upingaji huo! Hapa tunarudi kwenye historia iliyotolewa na FJM; mambo yangekua yale yale. Wakati mwingine assumptions uwa hazikwepi. Katika hilo assumptions hazikwepi pia; kwani hata theories zote uzijuazo zimetengenezwa kwa assumptions!

Sitaki kuamini kwamba wewe ulitaka CHADEMA wapinge tu kwa kufuata protocol za upingaji ilihali wenyewe walielewa fika kwamba upingaji wao husingekua na manufaa yoyote kutokana na aina ya bunge lililopo!

Pia suala la kukihoji CHADEMA juu ya muswada huo halijakaa vyema; wadau humu wamekuuliza ya kwamba, kwani huo muswada ni mali ya CHADEMA?

Wewe kama mpenda mabadiliko/mageuzi (or whatever you may name it) unahisi hili suala lilistahili kupingwa? Kama ndio hakuna taratibu ambazo zinakuruhusu wewe kama mpenda mabadiliko/mageuzi kwenda kufungua kesi mahakamani ili kupinga? Maana hapa unavyojionyesha ni as if CHADEMA has to be blamed for this!!

Naomba majibu!
 
Pasco,
Mkuu wangu nadhani ku face reality ndio muhimu zaidi inapotokea hoja kama hii. Mimi nadhani Chadema wamefanikiwa sana kuonyesha vitu kabla hata havitatokea ni kama vile utabiri wao umejionyesha wazi pale CCM na NCCR walopotoka kisha CCM wakaupitisha muswada bila pingamizi. Kwa hali yoyote ile muswada huu ungepita na yaonyesha wazi Spika asingesimama na CDM/ NCCR bila support kutoka upande wa CCM hata baada ya wao kuondoka bungeni hapakuwa na pingamizi..

Kuuputisha muswada bila pingamizi toka upande wa pili kumeonyesha wazi kwamba mawazo nje ya yale ya wanaCCM hayawezi kupewa nafasi na mfumo wetu ni wengi wape usisahau hilo...Na binafsi yangu, sio tu tunahitaji katiba mpya bali ku re define - Articals of Union ambazo zinawapa baraza la Mapinduzi nguvu kubwa ya ku oversee maswala yote yasiyoihusiana na Muungano kuhusu Zanzibar. Maadam sasa tuna mfumo wa vyama vingi sidhani kama ni haki Baraza la Mapinduzi ambalo wajumbe wake wote ni wanachama wa ASP ambacho leo ni CCM na hawa ndio walokuwa sababu kubwa ya Salim. A. Salim kuondolewa haki yake ya kugombea Urais.
 
Hii issue ni sawa na mtu ambaye anataka kufa lakini dawa ya kumwokoa iko kwenye himaya ya simba wenye njaa...

Je mtu huyo asubiri afe kwasababu anajuwa kwamba akienda kwenye himaya ya Simba wakali wenye njaa hawatamwacha na hivyo matokeo kuwa yale yale yani kifo?

Ni uamuzi unaoweza kuchukuliwa kwa utofauti na watu wa tofauti.

Ndo jinsi hii issue ilivyokaa.
 
Pasco,
Mkuu wangu nadhani ku face reality ndio muhimu zaidi inapotokea hoja kama hii. Mimi nadhani Chadema wamefanikiwa sana kuonyesha vitu kabla hata havitatokea ni kama vile utabiri wao umejionyesha wazi pale CCM na NCCR walopotoka kisha CCM wakaupitisha muswada bila pingamizi. Kwa hali yoyote ile muswada huu ungepita na yaonyesha wazi Spika asingesimama na CDM/ NCCR bila support kutoka upande wa CCM hata baada ya wao kuondoka bungeni hapakuwa na pingamizi..

Kuuputisha muswada bila pingamizi toka upande wa pili kumeonyesha wazi kwamba mawazo nje ya yale ya wanaCCM hayawezi kupewa nafasi na mfumo wetu ni wengi wape usisahau hilo...Na binafsi yangu, sio tu tunahitaji katiba mpya bali ku re define - Articals of Union ambazo zinawapa baraza la Mapinduzi nguvu kubwa ya ku oversee maswala yote yasiyoihusiana na Muungano kuhusu Zanzibar. Maadam sasa tuna mfumo wa vyama vingi sidhani kama ni haki Baraza la Mapinduzi ambalo wajumbe wake wote ni wanachama wa ASP ambacho leo ni CCM na hawa ndio walokuwa sababu kubwa ya Salim. A. Salim kuondolewa haki yake ya kugombea Urais.
Mkuu Mkandara,

Naona Pasco anapingana zaidi na Lissu kuhusiana na maadili ya kisheria kama nimwelewa, kwamba the process should have been exhausted.

Sasa sijui kama ni right kumu hold to those standards given the fact kuwa sidhani kama procedure ilikuwa ya kisheria ama ni taratibu za bunge.

Ama kama taratibu za bunge ie kwenye issue ya muswada hii zina angukia kwenye "sheria"

Nadhani mwishowe tutaelewana tu.
 
MM wewe ni miongoni mwa wapenzi wa CDM walio tayari kuburuzwa na hoja dhaifu pasipo kuhoji na kibaya zaidi unataka kuwafunga mdomo wanahoji kwa nia njema.Mkuu Pasco kaleta hoja nzuri akitegemea atapata majibu ya uhakika ninachokiona hapa ni aina ya majibu yanayokwepa swali la msingi !.

Ngongo,
Kwanza nataka kukukumbusha kwamba sio tu mimi ni mpenzi wa chadema, bali mimi ni mwanachama hai na ni Kiongozi ngazi ya Jimbo.
Wala usijidanganye bure ndugu yangu, mimi siburuzwi hata siku moja. Katika hili la muswada wa katiba mpya ninawaunga mkono viongozi wangu mia kwa mia. Siwaungi mkono kwa sababu tu ni viongozi wangu/wabunge wa chama changu, bali ni kwakuwa nimejitahidi kuusoma muswada pamoja na kufuatilia kwa karibu hoja mbalimbali zinazotolewa na makundi mbalimbali ya watanzania, kuanzia kwa wanaharakati, majaji wastaafu na hata wazee wastaafu wa ccm na serikali. Wote hao wamekuwa na mtazamo sawa na wa chadema, sasa usije ukaniambia kwamba jukwaa la katiba, majaji wastaafu na wazee wastaafu wa ccm na serikali nao wanaburuzwa na hoja dhaifu.
Hoja hii ukiita dhaifu, bila shaka wewe ndiye utakuwa dhaifu kwakuwa utakuwa umeshindwa kuona uzito wa hoja ambao umemlazimu mwenyekiti wa ccm taifa kuizungumzia kwa marefu na mapana yake katika kujitetea, sasa hapo wewe unaiona ni hoja dhaifu? utakuwa na matatizo ya kupima hoja mkuu si bure.

Sijamfunga mdomo mtu yeyote anayewahoji viongozi wangu/wabunge wangu, bali ninahoji hoja yake kama anavyohoji wabunge wangu. TL alitoa hoja bungeni kwa mujibu wa kifungu hicho anachokitaja lakini spika hakumuelewa. Kama tutakubaliana kwamba Mnyika na Machali hawakutoa taarifa mapema kwa spika ili watoe hoja yake lakini nitakukumbusha kwamba kwenye hotuba ya Lisu alitoa hoja ya kusitisha huo mjadala wa muswada kwa kifungu hicho lakini spika akapindisha makusudi ili kuinusuru serikali kwa kuwa wlaishakuwa na kikao chao mapema na kukubaliana kuendelea hivyo hivyo bila kusikiliza wadau wengine.
 
......
  • pia tuwe na tahadhari kwani, kuna theories zingine huwa zinashindwa kufanya kazi kwenye practical ....
  • na wakati mwingine sound logic huwa zinakuwa zaidi ya moja ...
Hivyo Pasco anaweza kuwa right ama wrong pia. Lakini possibility ya Pasco kuwa wright inakuwa affected na determination ya CCM waliyoonesha ndani ya Bunge. Hivyo Mwanakijiji anaonekana kuwa na possibility kubwa ya kuwa sahihi zaidi.

Mimi ni mwana CCM lakini nina simanzi kubwa na kinachoendelea katika nchi na ndani ya CCM. Natamani katiba ijadiliwe kwa uwazi na muungano pia. Lazima tukubali kuwa sasa ya mabadiliko imefika na itakuwa vigumu sana kuyasimamisha (to stop the wind of change is rather impossible..). Si Libya tu, mabadiliko yametikisa hadi Ulaya na Asia, na mwangwi wake umefika hadi Amerika. Sisi wa-Tz na Kikwete wetu hatuwezi kushindana na upepo huo, haiitawezekana.

Mimi naamini kabisa kuwa, tukikaa chini na kujadiliana ni amani, na tukifanya siasa na kushindana kwa haki na kubadilishana katika uongozi kwa taratibu zetu, itakuwa amani zaidi. Tatizo ni ubinafsi na hofu ya watawala kuumbuliwa madhambi yao ya ufisadi... Hicho ndiyo kitaangamiza Tanzania na Tanganyika yake...
 
Mkuu Mkandara,

Naona Pasco anapingana zaidi na Lissu kuhusiana na maadili ya kisheria kama nimwelewa, kwamba the process should have been exhausted.

Sasa sijui kama ni right kumu hold to those standards given the fact kuwa sidhani kama procedure ilikuwa ya kisheria ama ni taratibu za bunge.

Ama kama taratibu za bunge ie kwenye issue ya muswada hii zina angukia kwenye "sheria"

Nadhani mwishowe tutaelewana tu.
Sawa lakini nachojua mimi inategemea TL ameyazungumza haya katika hatua gani ya bunge..Kama nilimwelewa vizuri JK ktk hotuba yake inaonyesha wazi CDM na NCCR wamepinga muswada huu ktk hatua za mwanzo kabisa za kanuni ya 70 kujia 72... sasa huwezi mtu kuzungumzia kanuni ya 86 nje ya kamati ya bunge wakati muswada umekwamishwa ktk hatua ya 70 kwa kutumia vifungu vya kanuni ya 71...
 
"Kwa sababu hizi zote, Mheshimiwa Spika,naomba kutoa hoja chini ya kanuni ya 86(3)(b) ya Kanuni za Kudumu za Bunge hili tukufu kwamba Bunge hili likatae Muswada huu Kusomwa Mara ya Pili kwa sababu Serikali imeleta Muswada Mpya na wenye mabadiliko makubwa na ya msingi bila kufuata masharti ya kanuni ya 84(3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge; na pia kwa sababu Serikali haijatekeleza maagizo ya Bunge hili tukufu kuhusu kutoa muda zaidi kwa Kamati na wananchi kuufikiria, kuuelewa na kuutolea maoni Muswada huu kinyume na matakwa ya ibara ya 18(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano juu ya uhuru wa wananchi kutoa maoni yao; ibara ya 21(1) na (2) juu ya haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wan chi, na haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayowahusu wananchi, maisha yao au yanayolihusu Taifa".


Hayo ni maneno yaliyomo kweye hotuba ya kambi ya upinzani (Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria). Sasa sielewi Pasco anachokitaka.

Nakumbuka baada ya kumaliza kuongea Tundu Lissu alisema "Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha". Nilivyomuelewa na kumsikia Spika siku ile ni kwamba Tundu Lissu alipaswa kusema "Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja" ili suala ilo liweze kuhojiwa; lakini kwavile alikosea ndio maana Spika alikataa.

Lakini ukweli unabaki kwamba, licha ya Lissu kukosea, Spika angekua yupo pale kwa maslahi ya taifa (angekua hasie wa kuegemea upande wowote) angeweza kumpa nafasi Lissu ya kusema kwa usahihi; lakini kwavile nia yake ni kukomoa upinzani hakufanya hivyo. Mara ngapi tumeona mawaziri na hata wenyeviti wa kamati wanakosea katika namna ya kumalizia hotuba zao, lakini spika anawasahihisha na kuwapa nafasi ya kusema kwa usahihi?

Hivyo ndugu Pasco, labda kama una dhumuni jingine, lakini katika hili sidhani kama utakua na substance ​tena.
 
pasco, move ya chadema ilikuwa ni anticipation of the inevitable.
anticipation signifies brilliance and maturity in a person.
 
"Kwa sababu hizi zote, Mheshimiwa Spika,naomba kutoa hoja chini ya kanuni ya 86(3)(b) ya Kanuni za Kudumu za Bunge hili tukufu kwamba Bunge hili likatae Muswada huu Kusomwa Mara ya Pili kwa sababu Serikali imeleta Muswada Mpya na wenye mabadiliko makubwa na ya msingi bila kufuata masharti ya kanuni ya 84(3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge; na pia kwa sababu Serikali haijatekeleza maagizo ya Bunge hili tukufu kuhusu kutoa muda zaidi kwa Kamati na wananchi kuufikiria, kuuelewa na kuutolea maoni Muswada huu kinyume na matakwa ya ibara ya 18(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano juu ya uhuru wa wananchi kutoa maoni yao; ibara ya 21(1) na (2) juu ya haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wan chi, na haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayowahusu wananchi, maisha yao au yanayolihusu Taifa".


Hayo ni maneno yaliyomo kweye hotuba ya kambi ya upinzani (Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria). Sasa sielewi Pasco anachokitaka.

Nakumbuka baada ya kumaliza kuongea Tundu Lissu alisema "Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha". Nilivyomuelewa na kumsikia Spika siku ile ni kwamba Tundu Lissu alipaswa kusema "Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja" ili suala ilo liweze kuhojiwa; lakini kwavile alikosea ndio maana Spika alikataa.

Lakini ukweli unabaki kwamba, licha ya Lissu kukosea, Spika angekua yupo pale kwa maslahi ya taifa (angekua hasie wa kuegemea upande wowote) angeweza kumpa nafasi Lissu ya kusema kwa usahihi; lakini kwavile nia yake ni kukomoa upinzani hakufanya hivyo. Mara ngapi tumeona mawaziri na hata wenyeviti wa kamati wanakosea katika namna ya kumalizia hotuba zao, lakini spika anawasahihisha na kuwapa nafasi ya kusema kwa usahihi?

Hivyo ndugu Pasco, labda kama una dhumuni jingine, lakini katika hili sidhani kama utakua na substance ​tena.
Mkuu wangu shukuran sana..Ndio uzuri wa JF ni darasa wakati wote..Kwa hiyo, nimejifunza kuwa mbunge anaweza tumia kifungu cha 86 (3) baada ya muswada kutoka kamati ya bunge na kuwasilishwa...
 
Mkuu Ngongo, niliwahi kuchangia mahali kuhusu watumizi ya misuso haswa kwa jamii za kiasiri za kiafrika, mnajua tabia za mususo ni za kina nani, na siku zote huwa sikubaliani na baadhi ya misuso yao, na kwa vile niko very frank, huwa nawaeleza, na kinachofuatiwa ni kushukiwa kwa nguvu zote.

Pasco,

Unapokuwa unasoma sheria ama kanuni usiishie kuitazama katika makaratasi tu, ni muhimu sana kuitazama practically na usisahau katika huu uwanja wa siasa za ushindani wa vyama vingi ni muhimu sana kukumbuka historia. Wanabodi wengi wamegusia hili, kwamba ni chadema wametazama nyuma wakaona historia inasema kwamba ccm wamekuwa wakitumia wingi wao vibaya bungeni kupitisha sheria zisizokuwa na manufaa ama maslahi kwa umma wa watanzania.

Wewe unaweza kuja hapa ukasema kwa kususa chadema wamepata nini, lakini ukumbuke kwamba si suala la chadema kupata nini at first hand, bali wananchi wa Tanzania wamejifunza nini na wananufaikaje na huo utaratibu wa msuso wa chadema. Tangu chadema waje na hizi strategy kali na mpya kabisa katika siasa za Tanzania, kila mara baadhi ya watu wamekuwa wakisema chadema imekosea na kuwatabiria wananchi kuwatupa mkono, na wewe ni mmoja wao. Lakini ukweli ni kwamba tumekuwa tukishuhudia ushawishi wa chadema ukiongezeka kila kukicha. Sasahivi huku mtaani(nilipo mimi) agenda imekuwa ni katiba mpya, kila mtu anazungumza katiba mpya. Kwahiyo utaona kuna athari za moja kwa moja wazopata wananchi kutokana na matendo ya chadema.

Wananchi sasahivi wanapata fursa ya kuelimishwa na kujielimisha mapungufu ya muswada uliopitishwa ili kutaka kujua sababu ya chadema kuususia. Kama wangeendelea kuujadili, sasahivi tungekuwa tunaongea habari ya jairo na luhanjo lakini svyo, habari sasahivi kila kona ya nchi ni katiba mpya!!
 
"Kwa sababu hizi zote, Mheshimiwa Spika,naomba kutoa hoja chini ya kanuni ya 86(3)(b) ya Kanuni za Kudumu za Bunge hili tukufu kwamba Bunge hili likatae Muswada huu Kusomwa Mara ya Pili kwa sababu Serikali imeleta Muswada Mpya na wenye mabadiliko makubwa na ya msingi bila kufuata masharti ya kanuni ya 84(3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge; na pia kwa sababu Serikali haijatekeleza maagizo ya Bunge hili tukufu kuhusu kutoa muda zaidi kwa Kamati na wananchi kuufikiria, kuuelewa na kuutolea maoni Muswada huu kinyume na matakwa ya ibara ya 18(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano juu ya uhuru wa wananchi kutoa maoni yao; ibara ya 21(1) na (2) juu ya haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wan chi, na haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayowahusu wananchi, maisha yao au yanayolihusu Taifa".


Hayo ni maneno yaliyomo kweye hotuba ya kambi ya upinzani (Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria). Sasa sielewi Pasco anachokitaka.

Nakumbuka baada ya kumaliza kuongea Tundu Lissu alisema "Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha". Nilivyomuelewa na kumsikia Spika siku ile ni kwamba Tundu Lissu alipaswa kusema "Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja" ili suala ilo liweze kuhojiwa; lakini kwavile alikosea ndio maana Spika alikataa.

Lakini ukweli unabaki kwamba, licha ya Lissu kukosea, Spika angekua yupo pale kwa maslahi ya taifa (angekua hasie wa kuegemea upande wowote) angeweza kumpa nafasi Lissu ya kusema kwa usahihi; lakini kwavile nia yake ni kukomoa upinzani hakufanya hivyo. Mara ngapi tumeona mawaziri na hata wenyeviti wa kamati wanakosea katika namna ya kumalizia hotuba zao, lakini spika anawasahihisha na kuwapa nafasi ya kusema kwa usahihi?

Hivyo ndugu Pasco, labda kama una dhumuni jingine, lakini katika hili sidhani kama utakua na substance ​tena.

Ahsante sana Nyanda kwa kipande hiki cha hotuba ya mh. Tundu Lisu. Bila shaka hakuna ubishi kwamba msemaji wa kambi ya upinzani alikitumia vizuri kifungu hicho isipokuwa spika ndiye alishindwa kutimiza wajibu wake.
 
Back
Top Bottom