Katiba inakupa uhuru wa kukosoa/kutoa maoni haikupi uhuru wa kutoa lugha za kuudhi na kuchonganisha

Umenena vema mwandishi. Hao wanaomuunga mkono mhusika na siasa zake za maneno ya kashfa na lugha isiyostahili taaluma aliyo nayo hawamsaidii kitu. Bali wanaendelea kumwekea mwenziwao mazingira magumu sana ya kimahusiano na baadhi ya wananchi ambao walidhani kuwa hapo awali alikuwa na jambo la kusema kwa ajili yao. Huyo ndugu anahitaji mashauri na maoni kama ya mwandishi huyu (Jaruri) ili ajirekebishe. Watanzania wengi mimi nikiwa mmoja wao tunaona nia ya Mheshimiwa Rais ni nzuri sana na tumeamua kumuunga mkono. Hivyo matamshi ya huyo Mheshimiwa mtuhumiwa yanatuumiza sana tukizingatia wajibu wetu kama raia na wazalendo wa nchi hii anayoiombea mabaya.
 
Ulishakemea kauli ya "wapumbavu n.a. malofa?" Au kwa vile ilitolewa n.a.mwana ccm uliona ni sawa?

Magufuli alisema tujitegemee,hahitaji misaada! Ulihoji kwa nini alidai hana shida ya fedha ya REA wakati wengi hawana umeme? Hukuona tatizo kisa Magufuli katamka?

Unavyomwona Lissu haifai ni haki yako,lakini pia kumbuka kuna wengine wana haki pia ya kuona tofauti n.a. wewe! Haki ya nani iko juu ya nyingine?

Tukubaliane kutofautiana kistaarabu.

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Pia katiba does not guarantee the freedom after speech!

"the highest risk should give maximum profit"
 
Ai biliivu umemuandikia magufuli kuwa analugha za kuudhi sana!
 
Ndugu mtoa hoja,

Nadhani ufikiri tena kidogo angalau: Ujinga si tusi, ila upumbavu ni tusi. Kila mtu ni mjinga wa jambo fulani maishani hadi anakufa!!!!! Isipokuwa Ukitaka kulikuza neno ''mjinga'' ndo litakuwa tusi.
Pili: Kama Lissu amefanya uchochezi, ni vyema ikaainishwa kwamba kamchochea nani, na wapi, na kwa namna gani. Sina maana kuwa namsapoti kwa kusema misaada izuiwe, hapana. Nakataa kauli ya misaada kuzuiwa maana ikizuiwa, hata wananchi wake pia watapata shida maana baadhi ya maendeleo yatakwama. Hivyo, nadhani hapo angetafuta lugha ya ''busara'' kuwasilisha ujumbe wake.

Tatu: Mimi ni mwana CCM damu damu. Napinga kitendo cha viongozi wa upinzani kuweka ndani kila wakati ilhali sisi tukiendelea na mikutano yetu, tena mingine inafanyika nje, na tukumbuke mikutano ya nje ilipigwa marufuku. Wao wakifanya hata wa ndani wanakamatwa!!!!! Tunakosea, na jamii inaona.

Nne: Tukubaliane kutokukubaliana ktk baadhi ya hoja, japo kusituzuie kufanya kazi maana nchi ni yetu wote. Hoja za msingi wanazosema wapinzani tuzikubali tuzifanyie kazi nchi isonge mbele. Bila hawa wapinzani, tusingejua tunaibiwa madini, na waliposema miaka mingi huko nyuma, kwa ushabiki huu huu tuliwapinga na kuwatukana ''tumbili'' leo yamekuwa kweli.

Tano: Kimsingi, hakuna mwanadamu aliye mkamilifu, waweza kubali au kukataa. Na kama ndivyo ilivyo: Basi tukubali mtu yeyote kukosolewa. Labda kama tuna ''mahaba'' na hao walioko kwenye madaraka. Na bila kukosolewa, hatuwezi kujiona madhaifu yetu.

Mwisho: Hakuna wakati mgumu ktk maisha kama wakati unapokuwa kwenye ''kilele cha mafanikio'' Sifa Zitakuwa nyingi, na hukawii kuwa na kizunguzungu cha ufahari wa mafanikio na mwisho hujikuta umeanguka!!!!! Hivyo, wanaotukosoa, tusiwabeze na kuwaona hawafai. Tufanyie kazi yale ya msingi, yasiyofaa tuachane nayo.
Barikiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ni kujitoa akili au ni kile Lowasa alikuwa akihubiri-elimu! elimu! elimu!?
 
Samahani Mr Jaruri, ehe baada ya kuchochewa unasema wewe na wenzako ambao hujataja idadi yao mliudhika na kukasilika. Je ni makosa gani ya jinai mlitenda baada ya hapo?
nakushauri wewe na wenzako mripoti kituo chochote cha polisi kilicho karibu ili muweze kutoa maelezo na aina ya makosa ya jinai mliyotenda, mtaisaidia jamhuri kama mashahidi wakosaji waliosababishiwa kutenda makosa na mkosaji mkuu,adhabu yenu ni ndogo tu wala msijari,lakini uzalendo wenu utakuwa ni ule ulio tukuka.
 
Eti katiba inampa uhuru tundu Lisu wa kuongea maneno ya ovyoovyo..sijui kama anajua tofauti ya kukosoa kuhoji na kuudhi. Apimwe tu huo mkojo sio kwa uzwazwa huo.
 
Nenda kesho lumumba, kachukue posho Kazi nzuri Sana umeifanya huku jamii forum, viraza aina yako mpo wengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini katiba hii haikupi uhuru wa kutoa maneno yenye kuudhi na kuchonganisha jamii. 1/4

Kama maoni ni ukweli mtupu ila yanawaudhi watawala inakuwaje? Mfano, sio sahihi kuonyesha majina ya Escrow kupitia Mkombozi Bank bila kuonesha na yale ya StanBic kwani inatoa picha ya upendeleo na kutojali haki. Je, ili watawala wanalifurahia? Je, ni tusi ili?
 
Ni kweli katiba inakupa uhuru wa kukosoa bila kutumia maneno ya kuudhi. Sasa mtoa mada hebu jaribu kukosoa tu uone kama utakuwa salama hata kama katiba inakulinda.
 
Uliye andika thread hii ni mnafiki sana, yaani ww mkapa kawaita watu 'wapumbavu' umepiga makofi na kukenua meno kushangilia, lisu kawambia watu wakae na ujinga wao wa kutokujua umuhimu wa kubadilisha viongozi baada muda fulani....unaona ametumia neno la kuudhi....yule mwingine ametumia neno la kuchekesha!
 
Mkapa alirudia tusi mbele ya JPM kwa mara ya pili akiwatukana watanzania zaidi ya mil 6 kuwa ni wapumbavu na malofa,JPM akakenua meno akichekelea!Kwako hilo sio tusi wala lugha ya kuudhi!
Hawezi kuliona maana kavalishwa miwani ya mbao na ccm

In God we trust
 
Akili yako imejaa ubashite

In God we trust
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…