Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rafiki wewe naona huna mpya zaidi ya kupigia makofi kila atakacho kisema Lisu.Soma uchambuzi wangu hapo ndo utagundua hoja zote alizotoa ni za uongo na uchonganishiWe mleta ni mnafiki fulani unayeishi kwa kujipendekeza. Sio mara moja au 2 tunasikia viongozi wa serekali na ccm wakiongea lugha za kuudhi na hakuna hatua. Sasa leo unatujia na tapishi refu kutueleza ukidhani unaongea na watoto wadogo. Ni hivi Lissu kaongea ukweli, na wote tunajua ukweli una tabia moja tu ya kuuma. Cha muhimu aliyeambiwa ajirekebishe lakini kumpima Lissu mkojo ni kama kuruka sarakasi huku ukiwa umevaa taulo.
cc mleta hojaKwa mantiki yake hata raisi alivyosema atachomoa mwingine mwenye akili na sio wale VILAZA,,,nayo ni lugha ya kuuzi?
Sent using Jamii Forums mobile app
Umenena vyema mkuu,mwambieni Lisu aache kutoa lugha za kuudhi na kuchonganisha.Ulishakemea kauli ya "wapumbavu n.a. malofa?" Au kwa vile ilitolewa n.a.mwana ccm uliona ni sawa?
Magufuli alisema tujitegemee,hahitaji misaada! Ulihoji kwa nini alidai hana shida ya fedha ya REA wakati wengi hawana umeme? Hukuona tatizo kisa Magufuli katamka?
Unavyomwona Lissu haifai ni haki yako,lakini pia kumbuka kuna wengine wana haki pia ya kuona tofauti n.a. wewe! Haki ya nani iko juu ya nyingine?
Tukubaliane kutofautiana kistaarabu.
Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
Soma title ya hiyo post then uatapata majibu hapo,Issue ni kuwa huyo jamaa aache lugha za kuudhi na kuchonganishaNdugu mtoa hoja,
Nadhani ufikiri tena kidogo angalau: Ujinga si tusi, ila upumbavu ni tusi. Kila mtu ni mjinga wa jambo fulani maishani hadi anakufa!!!!! Isipokuwa Ukitaka kulikuza neno ''mjinga'' ndo litakuwa tusi.
Pili: Kama Lissu amefanya uchochezi, ni vyema ikaainishwa kwamba kamchochea nani, na wapi, na kwa namna gani. Sina maana kuwa namsapoti kwa kusema misaada izuiwe, hapana. Nakataa kauli ya misaada kuzuiwa maana ikizuiwa, hata wananchi wake pia watapata shida maana baadhi ya maendeleo yatakwama. Hivyo, nadhani hapo angetafuta lugha ya ''busara'' kuwasilisha ujumbe wake.
Tatu: Mimi ni mwana CCM damu damu. Napinga kitendo cha viongozi wa upinzani kuweka ndani kila wakati ilhali sisi tukiendelea na mikutano yetu, tena mingine inafanyika nje, na tukumbuke mikutano ya nje ilipigwa marufuku. Wao wakifanya hata wa ndani wanakamatwa!!!!! Tunakosea, na jamii inaona.
Nne: Tukubaliane kutokukubaliana ktk baadhi ya hoja, japo kusituzuie kufanya kazi maana nchi ni yetu wote. Hoja za msingi wanazosema wapinzani tuzikubali tuzifanyie kazi nchi isonge mbele. Bila hawa wapinzani, tusingejua tunaibiwa madini, na waliposema miaka mingi huko nyuma, kwa ushabiki huu huu tuliwapinga na kuwatukana ''tumbili'' leo yamekuwa kweli.
Tano: Kimsingi, hakuna mwanadamu aliye mkamilifu, waweza kubali au kukataa. Na kama ndivyo ilivyo: Basi tukubali mtu yeyote kukosolewa. Labda kama tuna ''mahaba'' na hao walioko kwenye madaraka. Na bila kukosolewa, hatuwezi kujiona madhaifu yetu.
Mwisho: Hakuna wakati mgumu ktk maisha kama wakati unapokuwa kwenye ''kilele cha mafanikio'' Sifa Zitakuwa nyingi, na hukawii kuwa na kizunguzungu cha ufahari wa mafanikio na mwisho hujikuta umeanguka!!!!! Hivyo, wanaotukosoa, tusiwabeze na kuwaona hawafai. Tufanyie kazi yale ya msingi, yasiyofaa tuachane nayo.
Barikiwa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuita mawazo ya Mhe Mwinyi ni ya kijinga ni Tusi Mubashara.RAIS MKAPA kuita watu wasio jua kuwa Tanzania ilisha kombolewa na haihitaji tena ukombozi na ni kivumishi cha sifaKusema wahisani wasitoe msaada ni tusi,kusema wazo la kijinga tusi?mkapa kuita wtz malofa,wapumbavu si tusi? Acha ushabiki,
Sent using Jamii Forums mobile app
Tunaheshimu sheria ndio maana tunaomba mahakama itusaidie haki yetu ipatikane ,sisi sio wadau wa ukuta sisi ni watanzania wazalendo tunao tii sheria bila shurutiSamahani Mr Jaruri, ehe baada ya kuchochewa unasema wewe na wenzako ambao hujataja idadi yao mliudhika na kukasilika. Je ni makosa gani ya jinai mlitenda baada ya hapo?
nakushauri wewe na wenzako mripoti kituo chochote cha polisi kilicho karibu ili muweze kutoa maelezo na aina ya makosa ya jinai mliyotenda, mtaisaidia jamhuri kama mashahidi wakosaji waliosababishiwa kutenda makosa na mkosaji mkuu,adhabu yenu ni ndogo tu wala msijari,lakini uzalendo wenu utakuwa ni ule ulio tukuka.
Basi na yeye ujinga ampelekee mke wakeHILO SIO TUSI,,KWANI UKIAMBIWA VIATU MPELEKEE MWANAO UMETUKANWA HAPO?
Waloitwa itwa wapumbavu ni wale ambao hawajui kuwa Tanzania ilisha kombolewa toka kwa wakoloni,,,,soma kamusi ya kiswahili uone mtu ambae hajui kitu na hataki kuelimishwa anaitwaje?Hivi yale ya mkapa yalikuwa ni ya kulijenga taifa?
In God we trust
Watanzania tuliitwa wapumbavu na malofa hivi hiyo ilikuwa ni kujenga taifa?hii Tanzania ni zaidi ya kituko
Waloitwa itwa wapumbavu ni wale ambao hawajui kuwa Tanzania ilisha kombolewa toka kwa wakoloni,,,,soma kamusi ya kiswahili uone mtu ambae hajui kitu na hataki kuelimishwa anaitwaje?
Jesus Christ was human being 100% and God at the same time 100% You cant equate human being with jesusTatizo lako hata wewe ukiitwa kuwa ni "mjinga" waweza kudai ni tusi, umetukanwa....
Ukichagua kuudhika ktk hali yoyote utakuwa umechagua wewe, hujachaguliwa na mtu...
Yesu Kristo (Mfalme wa wafalme wote) alikosolewa sana, alinenewa uongo sana na kusingiziwa sana lakini kamwe hakuchagua kuudhika badala yake aliwapenda wote "waliotaka" audhike...
Kopeni hekima na busara hizi mtaishi maisha marefu na yenye furaha.... lakini mkichagua kuudhika tu hata pasipo na sbb ya kuudhika, hamna haja ya kumlaumu Tundu Lissu... jilaumuni wenyewe kwa sbb kinyago mmekichonga wenyewe haohao !!