Nimemsikia mwanasheria wa Lisu akiongea jana baada ya kesi ya Lisu kuahirishwa na yeye(Lisu) kurudishwa rumande.Napenda tu nimkumbushe huyu mama kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa mtanzania yeyote uhuru wa kutoa maoni na kukosoa.Lakini katiba hii haikupi uhuru wa kutoa maneno yenye kuudhi na kuchonganisha jamii.
Nikirejea kauli ya Lisu ambayo leo imemfikisha Rumande,alisikika akisema yafuatayo:
1. Alisema anawaomba wahisani wasimsaidie Rais kwa fedha,kwanza nimkosoe kitu kimoja wahisani hawamsaidii Rais wanawasaidia watanzania maskini.Hizo pesa za donors zikija hali Rais na familia yake ni kwa ajili ya watanzania wote wakiwemo na Iramba mashariki ambako ndiko jimboni kwake.
Sasa alipitisha karatasi akachukua maoni yetu wananchi kuwa hatutaki wahisani? Rais alichaguliwa na watanzani walio wengi, kwa kauli ile ya Lisu alitumwa na watanzania wa wapi? Maana ninajua watanzania walio wengi wanamuunga mkono Rais,Wanataka barabara,wanataka huduma za maji,Elimu na hospitali.
Hii ni kauli ya kuudhi.Mimi kama mtanzania nieudhika na kauli hii na nina imani wapo wengi kama mimi ambao pia wameudhiwa na hii kauli.Kutoa lugha ya kuudhi ni kosa kisheria
2. Bwana huyu pia alisikika akisema mawazo aliyotoa Rais Mwinyi ni ujinga? Hivi hili sio tusi? Unamuitaje mtu kuwa katoa mawazo ya kijinga kisa anatofautiana na wewe? Una uhakika gani kama hakuna mtanzania mwingine ambae angependa Rais Magufuli atawale miaka zaidi ya 10?
Unadhibitishaje hili bila kupata maoni ya wananchi? And then unapata authority wapi ya kuyaita mawazo ya Binadamu mwenzio ni ya kijinga? Ok fine let me agree with you kuwa ni ya kijinga and then Yenye akili/hekima ni yapi? na una uhakika upi kuwa watanzania walio wengi wana kuunga mkono kwa hayo yako unayo dhani ndio yana hekima? ,,,,,
Hapa napo kuna kosa la kujibia, Huyu bwana aliongea lugha ya kuudhi, kaniudhi mimi na Mtanzania mwenzangu ambao tuna mawazo kama ya mzee Mwinyi kwa kutuita tuna mawazo ya kijinga ,,,hili ni tusi pia.Huwezi kuniita kuwa nina mawazo ya kijinga wakati hakuna reference point inayonipa mawazo sahihi.
Ungeweza kuniita mjinga endapo ningeshindwa kujibu 1+1=2,,Hapo sawa coz kila mtu at some point anaweza kuwa mjinga wa jambo fulani.Lakini kwa hili la kutoa maoni and then UNAYAITA YA KIJINGA NI TUSI MUBASHARA.
Kama ni katiba, katiba sio msahafu kama wananchi wakitaka katiba ibadilishwe ili Rais aendelee kutawala miaka dahari na dahari hawawi wajinga kwa kufanya hivyo bali ni hekima coz hekima ndio inawaongoza kuamua hivyo kwa kuona potential alizo nazo Rais in comparison na other presidential candidates.
3. Halafu Bwana huyu alisikika akisema kuwa Rais kafanya ukabila katika teuzi zake,,,Alitoa tuhuma ambazo sio za kweli.Alitaja viongozi wachache ambao Rais aliwataeua and by coincidence wakawa wanatokea kanda ya ziwa.Lakini kuna teuzi nyingi tu Rais kafanya ambazo hazitoki kanda ya ziwa.
Naweza mtajia Teuzi kadhaa hapa: Waziri mkuu,Mh Mwigulu,Mh Kabudi, Mh Mbarawa,Mh Ummy,Mh Kigwangala etc ,....Actually wewe pia unaweza nisaidia kumalizia hii list na mwishoni utagundua kuwa huyu Bwana (Lisu) hakuwa na lengo jingine zaidi ya kuleta chuki za kikanda na kikabila.
Hili nalo ni kosa la kujibu.
Help us spread patriotism by your like and share.
Visit us at:
Dr Magufuli For Better Tanzania