Katiba inakupa uhuru wa kukosoa/kutoa maoni haikupi uhuru wa kutoa lugha za kuudhi na kuchonganisha

Katiba inakupa uhuru wa kukosoa/kutoa maoni haikupi uhuru wa kutoa lugha za kuudhi na kuchonganisha

jaruri

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2014
Posts
717
Reaction score
459
Nimemsikia mwanasheria wa Lisu akiongea jana baada ya kesi ya Lisu kuahirishwa na yeye(Lisu) kurudishwa rumande.Napenda tu nimkumbushe huyu mama kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa mtanzania yeyote uhuru wa kutoa maoni na kukosoa.Lakini katiba hii haikupi uhuru wa kutoa maneno yenye kuudhi na kuchonganisha jamii.

Nikirejea kauli ya Lisu ambayo leo imemfikisha Rumande,alisikika akisema yafuatayo:

1. Alisema anawaomba wahisani wasimsaidie Rais kwa fedha,kwanza nimkosoe kitu kimoja wahisani hawamsaidii Rais wanawasaidia watanzania maskini.Hizo pesa za donors zikija hali Rais na familia yake ni kwa ajili ya watanzania wote wakiwemo na Iramba mashariki ambako ndiko jimboni kwake.

Sasa alipitisha karatasi akachukua maoni yetu wananchi kuwa hatutaki wahisani? Rais alichaguliwa na watanzani walio wengi, kwa kauli ile ya Lisu alitumwa na watanzania wa wapi? Maana ninajua watanzania walio wengi wanamuunga mkono Rais,Wanataka barabara,wanataka huduma za maji,Elimu na hospitali.

Hii ni kauli ya kuudhi.Mimi kama mtanzania nieudhika na kauli hii na nina imani wapo wengi kama mimi ambao pia wameudhiwa na hii kauli.Kutoa lugha ya kuudhi ni kosa kisheria

2. Bwana huyu pia alisikika akisema mawazo aliyotoa Rais Mwinyi ni ujinga? Hivi hili sio tusi? Unamuitaje mtu kuwa katoa mawazo ya kijinga kisa anatofautiana na wewe? Una uhakika gani kama hakuna mtanzania mwingine ambae angependa Rais Magufuli atawale miaka zaidi ya 10?

Unadhibitishaje hili bila kupata maoni ya wananchi? And then unapata authority wapi ya kuyaita mawazo ya Binadamu mwenzio ni ya kijinga? Ok fine let me agree with you kuwa ni ya kijinga and then Yenye akili/hekima ni yapi? na una uhakika upi kuwa watanzania walio wengi wana kuunga mkono kwa hayo yako unayo dhani ndio yana hekima? ,,,,,

Hapa napo kuna kosa la kujibia, Huyu bwana aliongea lugha ya kuudhi, kaniudhi mimi na Mtanzania mwenzangu ambao tuna mawazo kama ya mzee Mwinyi kwa kutuita tuna mawazo ya kijinga ,,,hili ni tusi pia.Huwezi kuniita kuwa nina mawazo ya kijinga wakati hakuna reference point inayonipa mawazo sahihi.

Ungeweza kuniita mjinga endapo ningeshindwa kujibu 1+1=2,,Hapo sawa coz kila mtu at some point anaweza kuwa mjinga wa jambo fulani.Lakini kwa hili la kutoa maoni and then UNAYAITA YA KIJINGA NI TUSI MUBASHARA.

Kama ni katiba, katiba sio msahafu kama wananchi wakitaka katiba ibadilishwe ili Rais aendelee kutawala miaka dahari na dahari hawawi wajinga kwa kufanya hivyo bali ni hekima coz hekima ndio inawaongoza kuamua hivyo kwa kuona potential alizo nazo Rais in comparison na other presidential candidates.

3. Halafu Bwana huyu alisikika akisema kuwa Rais kafanya ukabila katika teuzi zake,,,Alitoa tuhuma ambazo sio za kweli.Alitaja viongozi wachache ambao Rais aliwataeua and by coincidence wakawa wanatokea kanda ya ziwa.Lakini kuna teuzi nyingi tu Rais kafanya ambazo hazitoki kanda ya ziwa.

Naweza mtajia Teuzi kadhaa hapa: Waziri mkuu,Mh Mwigulu,Mh Kabudi, Mh Mbarawa,Mh Ummy,Mh Kigwangala etc ,....Actually wewe pia unaweza nisaidia kumalizia hii list na mwishoni utagundua kuwa huyu Bwana (Lisu) hakuwa na lengo jingine zaidi ya kuleta chuki za kikanda na kikabila.

Hili nalo ni kosa la kujibu.

Help us spread patriotism by your like and share.
Visit us at:Dr Magufuli For Better Tanzania
 
We mleta ni mnafiki fulani unayeishi kwa kujipendekeza. Sio mara moja au 2 tunasikia viongozi wa serekali na ccm wakiongea lugha za kuudhi na hakuna hatua. Sasa leo unatujia na tapishi refu kutueleza ukidhani unaongea na watoto wadogo. Ni hivi Lissu kaongea ukweli, na wote tunajua ukweli una tabia moja tu ya kuuma. Cha muhimu aliyeambiwa ajirekebishe lakini kumpima Lissu mkojo ni kama kuruka sarakasi huku ukiwa umevaa taulo.
 
Toa vifungu vinavyosapoti haya maandishi yako ambayo kimsingi umesema yana msingi wa kisheria/katiba.

Nikukumbushe tu mambo ya kisheri /katiba hayaandikwi kama unavyoandika barua ya mapenzi. Kuandika hayo uliyoyaandika ili yawe na mashiko ni sharti uambatanishe na supporting authority, vinginevyo kusema haya uyasemayo ni vema useme kuwa hayo ni mawazo yako na si kwa mijibu wa sheria/ katiba.
 
Kesi ipo mahakamani, ngoja tusubiri hukumu siku itakapotolewa.
 
Nimemsikia mwanasheria wa Lisu akiongea jana baada ya kesi ya Lisu kuahirishwa na yeye(Lisu) kurudishwa rumande.Napenda tu nimkumbushe huyu mama kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa mtanzania yeyote uhuru wa kutoa maoni na kukosoa.Lakini katiba hii haikupi uhuru wa kutoa maneno yenye kuudhi na kuchonganisha jamii.

Nikirejea kauli ya Lisu ambayo leo imemfikisha Rumande,alisikika akisema yafuatayo:
1.Alisema anawaomba wahisani wasimsaidie Rais kwa fedha,kwanza nimkosoe kitu kimoja wahisani hawamsaidii Rais wanawasaidia watanzania maskini.Hizo pesa za donors zikija hali Rais na familia yake ni kwa ajili ya watanzania wote wakiwemo na Iramba mashariki ambako ndiko jimboni kwake.Sasa alipitisha karatasi akachukua maoni yetu wananchi kuwa hatutaki wahisani? Rais alichaguliwa na watanzani walio wengi, kwa kauli ile ya Lisu alitumwa na watanzania wa wapi? Maana ninajua watanzania walio wengi wanamuunga mkono Rais,Wanataka barabara,wanataka huduma za maji,Elimu na hospitali.Hii ni kauli ya kuudhi.Mimi kama mtanzania nieudhika na kauli hii na nina imani wapo wengi kama mimi ambao pia wameudhiwa na hii kauli.Kutoa lugha ya kuudhi ni kosa kisheria

2.Bwana huyu pia alisikika akisema mawazo aliyotoa Rais Mwinyi ni ujinga? Hivi hili sio tusi? Unamuitaje mtu kuwa katoa mawazo ya kijinga kisa anatofautiana na wewe? Una uhakika gani kama hakuna mtanzania mwingine ambae angependa Rais Magufuli atawale miaka zaidi ya 10? Unadhibitishaje hili bila kupata maoni ya wananchi? And then unapata authority wapi ya kuyaita mawazo ya Binadamu mwenzio ni ya kijinga? Ok fine let me agree with you kuwa ni ya kijinga and then Yenye akili/hekima ni yapi? na una uhakika upi kuwa watanzania walio wengi wana kuunga mkono kwa hayo yako unayo dhani ndio yana hekima? ,,,,,Hapa napo kuna kosa la kujibia, Huyu bwana aliongea lugha ya kuudhi, kaniudhi mimi na Mtanzania mwenzangu ambao tuna mawazo kama ya mzee Mwinyi kwa kutuita tuna mawazo ya kijinga ,,,hili ni tusi pia.Huwezi kuniita kuwa nina mawazo ya kijinga wakati hakuna reference point inayonipa mawazo sahihi.Ungeweza kuniita mjinga endapo ningeshindwa kujibu 1+1=2,,Hapo sawa coz kila mtu at some point anaweza kuwa mjinga wa jambo fulani.Lakini kwa hili la kutoa maoni and then UNAYAITA YA KIJINGA NI TUSI MUBASHARA.Kama ni katiba, katiba sio msahafu kama wananchi wakitaka katiba ibadilishwe ili Rais aendelee kutawala miaka dahari na dahari hawawi wajinga kwa kufanya hivyo bali ni hekima coz hekima ndio inawaongoza kuamua hivyo kwa kuona potential alizo nazo Rais in comparison na other presidential candidates.

3.Halafu Bwana huyu alisikika akisema kuwa Rais kafanya ukabila katika teuzi zake,,,Alitoa tuhuma ambazo sio za kweli.Alitaja viongozi wachache ambao Rais aliwataeua and by coincidence wakawa wanatokea kanda ya ziwa.Lakini kuna teuzi nyingi tu Rais kafanya ambazo hazitoki kanda ya ziwa.Naweza mtajia Teuzi kadhaa hapa:Waziri mkuu,Mh Mwigulu,Mh Kabudi, Mh Mbarawa,Mh Ummy,Mh Kigwangala etc ,....Actually wewe pia unaweza nisaidia kumalizia hii list na mwishoni utagundua kuwa huyu Bwana (Lisu) hakuwa na lengo jingine zaidi ya kuleta chuki za kikanda na kikabila.,,,,,
Hili nalo ni kosa la kujibu.....

Help us spread patriotism by your like and share.
Visit us at:Dr Magufuli For Better Tanzania
Lissu kasema maneno ya mwinyi ya kijinga, Mkapa akawaita watazania malofa....moja mchochezi, moja shujaa, moja yuko ndani moja yuko huru.

Nchi ya wagagikoko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkapa alirudia tusi mbele ya JPM kwa mara ya pili akiwatukana watanzania zaidi ya mil 6 kuwa ni wapumbavu na malofa,JPM akakenua meno akichekelea!Kwako hilo sio tusi wala lugha ya kuudhi!
katiba hairuhusu rais kustakiwa
 
Back
Top Bottom