KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Sawa kabisa.Kama nimekuelewa ,unachotaka kusema ni kuwa, kwa Sasa nchi yetu haina rais kwa mujibu wa katiba yetu,siyo?
Ila tatizo ni kwamba hata hili la 'mijadala' huenda haliwezekani, kwa sababu "mijadala itatuchelewesha kuwaletea wanyonge maendeleo" kwa hiyo mijadala ikianza tu inapigwa marufuku!Kupitia mijadala ndiyo raia wanaweza kuonyeshana kama kweli katiba na sheria zinakiukwa. Hata mijadala hii haitasaidia kubatilisha ukiukwaji huu basi angalau kumbukumbu zitawekwa kwa ajili ya vizazi vijavyo na historia ya taifa letu. Kama kweli ukiukwaji wa katiba na sheria utadhihirika bila shaka huko mbele ya safari hali hiyo itataxamwa kikatiba.
Katiba na sheria haziusiki na uteuzi wa Ndg Bashiru... labda wameamua kujaribu ubashite ktk vigezo...Pamekuwa na kambi mbili katika uteuzi huu na msaada wa wadau wa katiba na sheria unaweza kutupa mwanga.
Najua kuna jukwaa la mambo ya sheria lakini uteuzi huu una athari za kisiasa ambazo inawezekana kwa sasa hazipo wazi.
Tusaidieni tujue ukweli ni upi?
JPM hata afanye nini wewe huwezi kupongeza. Onyesha mahali popote pale kwenye hii Forum ulipompongeza. Unafiki sio kitu kizuri jipime mkuu, then umri ndio umekwenda hivyo. Kila mtu atalipwa kwa wema wake na mabaya yake...kwenye uteuzi huu Magufuli katoa boko.
..haileti picha nzuri kuteua mwanasiasa kuwa katibu mkuu kiongozi.
..katibu mkuu kiongozi anakwenda kusimamia nidhamu na maadili ya watumishi wa serikali.
..moja ya makatazo ktk utumishi wa serikali ni kushiriki siasa za vyama na majukwaani.
..sasa mtu ambaye anajulikana waziwazi ushiriki wake ktk siasa ataaminika vipi kuwasimamia watumishi wa serikali?
..uteuzi unaweza kuwa wa kisheria, maana wamelazimisha awe balozi kwanza, lakini nadhani hauleti picha nzuri.
..naamini Tanzania ina watu wengi sana wenye sifa na vigezo vya kuwa Katibu Kiongozi, na wasiokuwa na makando-kando ya kisiasa kama Dr.Bashiru. Hakukuwa na ulazima wa kulazimisha uteuzi huu.
NB:
..Hakuna katiba ambayo ni perfect imeeleze kila kitu. wakati mwingine kunahitajika busara na uungwana.
..Wamarekani wana katiba nzuri, lakini walipata matatizo walipochagua Raisi Trump ambaye hakuwa na busara, na si muungwana.
😂Kila kiitwacho katiba kipo compressedMtoa hoja anaongelea katiba gani?vipi tuna katiba au tuna no 1 ambaye kila kitu kinamzunguka yeye?nchi haina katiba ila tuna very very strong statesman.