Lusajo11 kuwa mwangalifu sana unapoandika, jitahidi sana kila unachoandika kiwe na sifa ya jina lako. Vinginevyo unajidhalilisha kwa kutumia jina lako vibaya. Au unataka kuniambia kuwa I should not judge the book by its cover. Please Lusajo11 acha kujidhalilisha...na kuhusu Katiba Pendekezwa weka kumbukumbu zako vizuri angalia kilichotokea wakati wa BMK, ni nani alipewa jukumu la kuiandika, aliandika nini na je ndivyo wananchi walivyotaka au alibadilisha maudhui ili kulinda kitumbua chake dhidi ya mchanga, je, mambo ya muhimu yakoje je itakidhi matakwa ya miaka mia moja ijayo....Zoea kujiuliza maswali magumu na usitake majibu mepesi yasiyo na mashiko