Katiba Itamke: Kiongozi yeyote wa kisiasa asimfukuze kazi mtumishi wa umma

Katiba Itamke: Kiongozi yeyote wa kisiasa asimfukuze kazi mtumishi wa umma

Private investigator

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2012
Posts
303
Reaction score
287
Taja yangu haijafuata protoko ila ninachomaanisha, katika utumishi wa umma kumekuwa na hawa mabosi ambao wengi wao sio wanataaluma katika nafasi walizonazo ila wana power kubwa sana kwa watu ambao ni wanataaluma.

Unakuta DC anamwagiza DED amsimamishe kazi labda Mhasibu. Hapo unakuta DC hajawahi hata kuwa mtumishi wa umma kabla ya UDC wake, ukute na DED nae hajawahi kuwa DED kabla ya UDED wake.

Shauri linagoma kwa mfano, mtumishi wa umma anaenda kushitaki kwa Katibu Mkuu wa wizara, bahati mbaya hata huyo katibu mkuu hakuwahi kuwa kwenye utumishi wa wizara hiyo, mfano ni mjeda tu aliteuliwa kisiasa.

Ushauri wangu, kiongozi wa kisiasa asiwe na mamlaka ya kutoa maamuzi juu ya utumishi wa mtu wala asiwe na mamlaka yoyote ya kinidhamu kwa mtumishi mwenye ajira ya kudumu.

Uongozi wa kisiasa sio permanent, unakuta mtu anafukuzwa kwa shinikizo la RC au DC au Waziri halafu kesho RC au DC ama huyo waziri anakuja kuonekana kilaza huku ameshaharibu maisha ya mtumishi mwaminifu.
 
Kuteuliwa ni shida, ninaona, mkuu wa mkoa, wilaya na wateuliwa wote wawe na fomu za maombi na CV zao zinaoeleweka. Mf. Mkuu wa mkoa awe na shahada ya business administration , nasema hivyo ili kazi yake aifahamu vizuri na kuondoa "inferiority complex"
 
Jingine Ni Hili la mwanasiasa wa darasa la Saba kumfukuza kazi MTU mwenye PhD.. . .au kumubagaza wakati yeye hata memkwa hakwenda. INAUDHI SANA
 
ukisema hivyo hakutakuwa na haja ya rais maana kila mtu atamvimbia
 
Kuteuliwa ni shida, ninaona, mkuu wa mkoa, wilaya na wateuliwa wote wawe na fomu za maombi na CV zao zinaoeleweka. Mf. Mkuu wa mkoa awe na shahada ya business administration , nasema hivyo ili kazi yake aifahamu vizuri na kuondoa "inferiority complex"

Samahani Mkuu Kwanini Umechagua awe na Business administration na Sio shahada nyingine?
 
ukisema hivyo hakutakuwa na haja ya rais maana kila mtu atamvimbia

Hapana Kaka Rais anaweza toa Order kwa Waliochini yake sio moja kwa Moja kwa mlengwa...
Imagine Rais atoe order kwa Pump Operator wa maji kama Kasababisha maji/Bomba Kukatika.Kumbe angemuagiza Mkurugenzi mkuu wa Dawasco Mkurugenzi angeshushachini mpaka kwa Mkuu wake Wa Idara then angechukuliwa hatua au Uchunguzi wa jambo husika!
Hata DED,DC,RC hatakiwi kwenda Moja kwa Moja kwa Fundi Mchundo au Mhasibu au Mhandisi wakati kuna wakuu wake wa kazi!
 
Ninaona mtu akijua kutawala shughuli yoyote ya kimtazamo, atakuwa na maarifa ya kutawala binadamu na kuwamudu . The one who knows how to lead and direct people to the proper way, (visionary leader) .Nilichagua business administration kwani kuna mambo mengi kuhusu kumiliki na kutawala.
 
Back
Top Bottom