Laizer Peter unachanganyikiwa nini? Katiba ni msingi wa sheria za nchi yeyote duniani ndiyo maana inaitwa sheria mama. Hivyo Tanzania ikiwa miongoni mwa mataifa ya dunia hii inawajibika kuwa na katiba yake ili kuweza kusimamia nchi katika masuala mbalimbali ya kijamii kwa watu wake.
Katiba Inaypendekezwa ya nchi yetu imeanza kwa kuainisha kwa kutambua Wananchi na kusema Kwa kuwa, sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayoheshimu na kuzingatia misingi ya utu na udugu, uhuru, kujitegemea, haki, usawa, amani na utulivu, umoja na mshikamano katika nyanja zote za maisha yetu. Usichanganyikiwe ndg yangu Laizer uliza utajulishwa maana kuuliza sio ujinga bali mtu ataka kujuzwa.