KATIBA MBONA IPO?

KATIBA MBONA IPO?

Kajiarashid

Member
Joined
Jun 2, 2021
Posts
69
Reaction score
27
1. Kwanza tujiulize, KATIBA ni nini?

2. Herufi hizi tatu.....Ka, Te na Be, ukizibadilisha irabu, utasoma maneno mengine. K.v...... KITABU, KATIBU, KUTUBU n.k; badala ya neno LA awali KATIBA

3. Mimi sipingi KATIBA MPYA, bali nataka tuonyeshane hiyo KATIBA MPYA yenyewe iko je, na Pahala ilipo, kwani ilishakuwepo tangu kale na kale. Bali Wazungu watawala wanaificha!!!!

4. Ni kweli KATIBA hii ya zamani, jina "KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA mwaka 77" hata kabla, sio muafaka kutumika kuongoza nchi na au watu. Na mimi nasema, sio kwamba imepitwa na wakati TU, bali SIYO. Huu ni mkenge tuliovikwa na wakoloni ili wadumu kututawala kwa rimoti kontroli. Kwani Katiba ya nchi ni maandiko yaliyopangwa namna ya adui wa watu wetu atakavyoweza kututawala, aibe Mali, utajiri na nguvu zetu umri wa dunia kuwepo.

4.1 Kumbuka muasisi wa katiba hii ni mkoloni pale mwaka 1959, waziri wa mambo ya ndani wa uingerereza alipowasimamia wajumbe wetu 11 wakiongozwa na Bwana Kambona kule London, kuunda na kuiandika na kuja nayo.

4.2 Tambua pia kwamba Waingereza hawana katiba makhususi iliyo andikwa kwa mikono ya watu. Lakini inakuaje wao hawana, lakini sisi wametupachikia dude hili Katiba ya NCHI?

4.3 Wao wametufanyia unyama huo wakiwa na LENGO maalumu. Wametuingiza sisi nchi na WATU wake katika UPUMBAVU.

4.4 Hii ni kwa sababu, mtu ni kiumbe kilichoumbwa na Mtengezaji Aitwaye Mwenyezi Mungu (Wa Wote). Tambua kwamba muunda gari au kifaa chochote kile, ndiye anayewajibika kuandika instruction manual book (kitabu cha maelezo ya namna ya chombo kilivyo, ramani, jinsi ya kukikarabati na vifaa vilivyotumika).

4.5 Kwa hiyo sisi VIUMBWA tunayo Haki ya kudai KITABU hicho kwa Yule Muumbaji wetu Wa Wote (Mwenyezi Mungu).

5. KATIBA NI NINI?

5.1 Katiba ni MWONGOZO kwa watu, unaoweza kuwa Katika mfumo wa KITABU.

5.2 KATIBA MAANA YAKE NI NINI?

5.2.1 KATIBA ni KITABU chenye kuonyesha watu, namna ya KUREJEZA jinsi ya Watu kuishi.

5.3 NI IPI HISTORIA YA WATU?

Watu kumbe tuna mnyambuliko wa MAISHA wenye vituo vitano [5]-
1) maisha mbinguni asili ndipo kwetu,
2) maisha matumboni mwa mama zetu,
3) maisha baada ya kuzaliwa hapa duniani,
4) maisha makaburini (mwili) na mbinguni (roho) kwenye makabati,
5) maisha siku ya kufufuliwa na baada ya kufufuliwa.

5.3.1 Kwa historia hiyo, mbona ni ajabu kuwa, katika kituo cha tatu katika maisha na safari ya mwanadamu, ndio linazuka dude LA kujiandikia mfumo wa namna ya watu waishi; sio waishije ulimwenguni, la. Bali katika nchi husika?

Hivyo vituo vingine KULIKONI?

6. HISTORIA YA UVAMIZI WA BARA LA WATU {WALILOLIITA A FREE CAR (AFRIKA)}:

Wazungu walipovamia bara letu hili LA WATU, waliwakuta babu zetu tayari kwenye maisha haya kwenye kituo cha tatu, wameshika mihimili mitatu ya taifa lao-
1)- MILA
2)- DESTURI na
3)- JADI
UTATU MTAKATIFU ASILI.
Wao wakauponda utatu huu origino na kutuundia mihimili hii~ mi3:
1)- badala ya Mila wakaweka SERIKALI,
2)- badala ya Desturi, wakaweka KATIBA YA NCHI na
3)- badala ya Jadi wakaweka MAHAKAMA YA KIZUNGU.
Mihimili mitatu ya nchi isiyo na Dini/Mungu. (uh! Mbona tunamwaga Michele mbele ya KUKU?)

6.1 Kwa njia hii tuangalie kipengele kimoja tu - hili neno DESTURI ZA WATU, wakaziua kwa kutuvika KATIBA YA NCHI (mbona wao hawana)!
(wao sana lengo tofauti na WAO).

6.2 DESTURI ZA WATU:
Desturi ZETU zilijengwa na Babu zetu juu ya MISINGI mitatu-
1): UAMINIFU,
2): HESHIMA na
3): UTII {KUDUMISHI KUHESHIMU MIIKO}~
MISINGI MITATU HII YA MAISHA HAPA DUNIANI, WAZUNGU KIRAHISI WAKAONDOA KWA KUTUUNDIA KATIBA YA NCHI ISIYO NA MUNGU /MIIKO, HESHIMA wala UAMINIFU..... itaendelezwa
{hapa sio pahala pa mtanange huu. Mimi sio simba wala yanga, wewe je?}

7. Natamani zaidi kutiririka, lakini hapa ni mtandaoni. Wazungu wao wako vitani. Oh! Maisha hapa duniani ni NIPE NIKUPE, au?

8. Ombi!
Raisat Samia, salamu yetu nzuri iongezee neno moja tu "Mola", isomeke 'KWA JINA LA "MOLA" WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA......KAZI INAENDELEA'.


...........aiwaah!
 
Kwa jina la 'Mola' wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, maoni juu ya KATIBA mpya yana zidi kuwekwa bayana.

KATIBA MPYA NI MUHIMU:

Hii haina upinzani. Ukipinga umuongo. Tena unajidanganya mwenyewe kwa kutiwa shemere na elimu yako ya kutaka ajira (secular education). Lakini:

1- Tujiulize, katiba hii ya zamani, tuliipataje?
2- Kama ni wazungu ndio walitusimamia tukaipata, hii mpya ATUSIMAMIE nani?

WANA WA MAMA WEUSI:

1- Sisi ni nani?
2- Dunia kumbe ni daraja, huko tulipotoka ni wapi na ni wapi tunapokwenda?
3- Asili yetu watu weusi ni wapi?
4- Sisi ni WABATU au MANILOTIK kweli au ni MAKUSH {UZAO WA KINABII}?
5- Katiba ya nchi tuliyo nayo ni kitabu chenye muongozo wa namna au jinsi IPI nchi ITAWALIWE. Kitabu hiki kinastahili kuitwa KATIBA?
6- Kwani KATIBA ni mini?
7- Neno LA kimombo CONSTITUTION, kweli tafsiri yake ni KATIBA? Kweli hiyo?
8- Constitution ya taifa LA China ina SURA 4 tu. Humo inaonyeshwa UTAWALA WA WATU (sio utawala wa nchi) uwe vipi, na sio utawala wa serikali kama ilivyo kwetu.

TUJIULIZE TENA NA TENA:

Mbona mazungumzo yetu JamiiForum juu ya KATIBA mpya hayana UGALI? Au ni uwanja wa kuhemka na kucheua tu?

UGALI ni maji yaliyochemka na UNGA ukasongwa humo mpaka UKAIVA. Ndio hupakuliwa na KULIWA.

NAAM! Je malumbano haya ya KATIBA MPYA humu JF, yatasongeka na kuiva link na KULIWA?

......aiwaaah!
 
Back
Top Bottom