Katiba Mpya haipo kwenye Ilani wala ahadi za CCM, Tusimsumbue na tusimuwekee Rais Samia maneno mdomoni

Katiba Mpya haipo kwenye Ilani wala ahadi za CCM, Tusimsumbue na tusimuwekee Rais Samia maneno mdomoni

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Lipo wimbi la waliokosa hoja za maendeleo kutaka kutuyumbisha.

Rais Samia atapimwa kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM tu kwani huo ndio mkataba rasmi na wananchi kati yao na Serikali iliyopo.
Katiba mpya haipo kwenye Ilani ya CCM na mgombea (Hayati Magufuli ) na mwenza wake (incumbet president) hawajibiki kuitimiza.

Wananchi watamdai maji safi na Salama, afya bora, barabara na madaraja na fedha mfukoni.

Kamwe tusitengeneze mahitaji ya viongozi wahuni wala bata wa Dubai.
 
Taasisi kulipwa Mara mbili ipo kwenye ilani.
Ahadi za maji miaka 4 ya mama haimtoshi.msimtwishe mzigo
kukabiliana na ubadhirifu kwenye taasisi ipo kwenye ilani?
 
Tunajua kuwa CCM haitaki katiba mpya

Sisi wananchi tunataka katiba mpya

Sasa kama CCM wana nchi yao binafsi basi wasijushughulishe kuleta hiyo katiba mpya, lakini kama wanaongoza nchi iitwayo Tanzania basi wananchi tunataka katiba mpya na maoni yetu yalishakusanywa mwaka 2013 kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba iliyotungwa mwaka 2012.

Nchi inatawaliwa kwa sheria na siyo Ilani ya CCM.

Nendeni mbadili sheria kwanza kabla ya kukataa mabadiliko ya katiba
 
kupigwa na mwiko ni kawaida

Kenya wana katiba mpya, mbona bado wana maendeleo makubwa kuliko sisi? Uzuri sasa hivi tunajua ccm hawako madarakani kwa kura za wananchi, bali yule dhalimu aliyeko motoni ndio alipora uchaguzi. Hivyo hiyo katiba mpya ni taka msitake lazima ipatikane.

Aanza kuandaa nyuzi za kutoka nazo mchakato huo ukianza. Katika vitu ccm mtajua mko nje ya muda, basi ni hili suala la katiba mpya.
 
Sasa, kama hawataki,
Suluhu ni nini.? Inabidi tulazimishane ndio tuingie Barabarani.
Chama A kinamiliki vifaru,Chama B kinamiliki hoja,nani ananguvu mkiwa barabarani.Katiba hapo itaruhusu hela ya matumizi chama A
 
Katiba ni ya wananchi hivyo ni kubwa kuliko chama chochote cha siasa
 
Lipo wimbi la waliokosa hoja za maendeleo kutaka kutuyumbisha.
Mama Samia atapimwa kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM tu kwani huo ndio mkataba rasmi na wananchi kati yao na Serikali iliyopo....
Kama wewe siyo jingalao kiukweli, basi tumia sababu aliyoitaja mama Samia kuwa “anataka kujenga uchumi kwanza” kabla ya katiba mpya! Na siyo kutoa reference za mwendazake!

Mwendazake yeye alisuspend katiba kwa kutumia sababu ya kujenga, ama kwa maneno yake “kuinyoosha nchi kwanza”. Usianzishe thread bila ya kufikiri kwa kina! Especially mtu kama wewe tuliyekupokea humu kitambo tu.
 
Mtake Msitake, Katiba Mpya lazima ipatikane.
Tutaidai kwa Nguvu na wivu Wote. [emoji58]
Makamanda naona mnataka kumjaribu mama. Nadhani mmesahau kuwa alishasema yeye na Magufuli ni kitu kimoja; na Magu alisema yeye hajaribiwi, kwa hiyo na mama hajaribiwi.
 
Makamanda naona mnataka kumjaribu mama. Nadhani mmesahau kuwa alishasema yeye na Magufuli ni kitu kimoja; na Magu alisema yeye hajaribiwi, kwa hiyo na mama hajaribiwi.
This time, hajaribiwi Atafanyiwa kweli.
Hatutanii
 
Back
Top Bottom