Katiba Mpya haipo kwenye Ilani wala ahadi za CCM, Tusimsumbue na tusimuwekee Rais Samia maneno mdomoni

Katiba Mpya haipo kwenye Ilani wala ahadi za CCM, Tusimsumbue na tusimuwekee Rais Samia maneno mdomoni

Lipo wimbi la waliokosa hoja za maendeleo kutaka kutuyumbisha.

Rais Samia atapimwa kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM tu kwani huo ndio mkataba rasmi na wananchi kati yao na Serikali iliyopo.
Katiba mpya haipo kwenye Ilani ya CCM na mgombea (Hayati Magufuli ) na mwenza wake (incumbet president) hawajibiki kuitimiza.

Wananchi watamdai maji safi na Salama, afya bora, barabara na madaraja na fedha mfukoni.

Kamwe tusitengeneze mahitaji ya viongozi wahuni wala bata wa Dubai.
Mbona 2015 ilikuwa kwenye Ilani kwanini Hakutekelezwa? Sio lazima Katiba iwe kwenye Ilani Acha Siasa za Chama kimoja
 
Lipo wimbi la waliokosa hoja za maendeleo kutaka kutuyumbisha.

Rais Samia atapimwa kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM tu kwani huo ndio mkataba rasmi na wananchi kati yao na Serikali iliyopo.
Katiba mpya haipo kwenye Ilani ya CCM na mgombea (Hayati Magufuli ) na mwenza wake (incumbet president) hawajibiki kuitimiza.

Wananchi watamdai maji safi na Salama, afya bora, barabara na madaraja na fedha mfukoni.

Kamwe tusitengeneze mahitaji ya viongozi wahuni wala bata wa Dubai.
Umeanza kwa uzuri na busara kubwa ila mwishoni ukanya.
 
Chama A kinamiliki vifaru,Chama B kinamiliki hoja,nani ananguvu mkiwa barabarani.Katiba hapo itaruhusu hela ya matumizi chama A

Chama A kinategemea chama B:

1. Kupambana lakini hayatakuwapo matumizi ya nguvu.
2. Kususia chaguzi zote.

Yote #1 na #2 ni kwa maslahi ya chama A kwa hiyo katiba mpya haitakaa upatikanaji:

Tungekua na katiba mpya kwa ule ushenzi na ushamba wa October 2020 angenzaje kuufanya??

Kwanini nafasi ya juu kwenye nchi mtu awekewe kinga na na uwezo wa kuteua 90% ya walio chini yake??

Hakuna kifungu cha kumuwajibisha ataachaje kujimwabafai??

Kwanini matokeo ya ubunge na udiwani yanapingika mahakamani ila ya urais hayaruhusiwi kuhojiwa???

Tume ya uchaguzi /uchafuzi inaundwa kwa influence za mtu mmoja posho anawalipa mtu huyo huyo ! Pia wanaapa kuwa waaminifu mbele yake na huyo huyo ni miongoni mwa washindani kwenye box la kura! Hivi CCM bado mnafikiri bado watu wote ni wajinga eeh??

Mnafikiri hizi ni zama zile za Kila mtu Kusikiliza RTD na kuangalia TVT kwamba taarifa na propaganda zote anazipata hapo bila kusikiliza hapo taarifa za kitaifa hatozipata???

Mnafikiri bado watanzania wote wanaipongeza serikali ikipeleka umeme na maji majumbani wakati ni miongoni mwa kazi za serikali kupelekea huduma watu waliolipa kodi mbali mbali??
 
Katiba mpya iko kwenye Ilani ipi na ya mwaka gani? Mvunja sheria hawezi kupenda uwepo wa sheria nzuri
 
Mtukufu rais wetu amalize kipindi chake cha urithi apite kushoto. Yeye ni rais wa sita awamu ya tano. Anayesema hii ni awamu ya sita huyo ni taahira
 
Back
Top Bottom