Katiba Mpya haipo kwenye Ilani wala ahadi za CCM, Tusimsumbue na tusimuwekee Rais Samia maneno mdomoni

Mbona 2015 ilikuwa kwenye Ilani kwanini Hakutekelezwa? Sio lazima Katiba iwe kwenye Ilani Acha Siasa za Chama kimoja
 
Umeanza kwa uzuri na busara kubwa ila mwishoni ukanya.
 
Chama A kinamiliki vifaru,Chama B kinamiliki hoja,nani ananguvu mkiwa barabarani.Katiba hapo itaruhusu hela ya matumizi chama A

Chama A kinategemea chama B:

1. Kupambana lakini hayatakuwapo matumizi ya nguvu.
2. Kususia chaguzi zote.

Yote #1 na #2 ni kwa maslahi ya chama A kwa hiyo katiba mpya haitakaa upatikanaji:

 
Tungekua na katiba mpya kwa ule ushenzi na ushamba wa October 2020 angenzaje kuufanya??

Kwanini nafasi ya juu kwenye nchi mtu awekewe kinga na na uwezo wa kuteua 90% ya walio chini yake??

Hakuna kifungu cha kumuwajibisha ataachaje kujimwabafai??

Kwanini matokeo ya ubunge na udiwani yanapingika mahakamani ila ya urais hayaruhusiwi kuhojiwa???

Tume ya uchaguzi /uchafuzi inaundwa kwa influence za mtu mmoja posho anawalipa mtu huyo huyo ! Pia wanaapa kuwa waaminifu mbele yake na huyo huyo ni miongoni mwa washindani kwenye box la kura! Hivi CCM bado mnafikiri bado watu wote ni wajinga eeh??

Mnafikiri hizi ni zama zile za Kila mtu Kusikiliza RTD na kuangalia TVT kwamba taarifa na propaganda zote anazipata hapo bila kusikiliza hapo taarifa za kitaifa hatozipata???


Mnafikiri bado watanzania wote wanaipongeza serikali ikipeleka umeme na maji majumbani wakati ni miongoni mwa kazi za serikali kupelekea huduma watu waliolipa kodi mbali mbali??
 
Katiba mpya iko kwenye Ilani ipi na ya mwaka gani? Mvunja sheria hawezi kupenda uwepo wa sheria nzuri
 
Mtukufu rais wetu amalize kipindi chake cha urithi apite kushoto. Yeye ni rais wa sita awamu ya tano. Anayesema hii ni awamu ya sita huyo ni taahira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…