Getrude Mollel
JF-Expert Member
- Apr 26, 2022
- 270
- 362
Niliwahi kusema hapa vyama vyama vyote vya siasa vimetokana na CCM. Ni kama vile madhehebu mengine ya dini ya kikristo yalivyomeguka kutoka Katoliki. CCM ni chama kikubwa sana barani Afrika, hivyo hakuna chama hata kimoja Tanzania kinaweza kukitingisha.
CCM ni kweli wamesema kwamba wanategemea kuipatia Tanzania Katiba Mpya, ila wamefanya hivi kwa matakwa yao sio kwa kelele za chama chochote. Ni wao wanajua hiyo katika itakuja lini na itakuwaje, ila za ndani zinasema kwamba Katiba haitotokea kabla ya 2025 bali baada tena kwa mbali mbele ya 2030.
CHADEMA kwenye hatakati zao za kudai katiba walishawahi kususia uchaguzi wa Serikali za mitaa, mfano mwaka 2019. Katika kususia kwao chaguzi ni kushinikiza mabadilko ya katiba wakidai kwamba katiba iliyopo inaipendelea CCM. Hapo kwanza ncheke..
Ila umeshawahi kusikia CHADEMA imesusia uchaguzi mkuu? Uchaguzi ni moja ya chanzo kikuu cha mapato cha CHADEMA. Hiki chama hujipatia fedha za kampeni kutoka kwa rafiki zao wa Ujerumani, Uingereza na Marekani. Hivyo hata Katiba iwe hii hii hadi 2060, bado CHADEMA utawaona tu kwenye uchaguzi mkuu. Wanajua watashindwa, ila hawataki kuacha pesa.
Niwaache na yafuatayo, kwanza Katiba Mpya itakuja CCM ikitaka, pili CHADEMA hata siku moja haiwezi kususia uchaguzi mkuu kisa hakuna Katiba Mpya. Tatu, Katiba Mpya sio mlango wa CHADEMA kushinda uchaguzi, hata ije leo Katiba Mpya, CCM itashinda tu.
Haya narakaribisha matusi..