Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 40,476
- 26,173
Ndugu zangu Watanzania,
Watanzania tunapaswa Kubadilisha katiba ili Rais Samia apate nafasi ya kuendelea kuongoza Taifa letu hata baada ya kumaliza Muda wake 2030. Hii ni muhimu ili kulipa Taifa nafasi na fursa ya kutumia Maono yake makubwa katika kulipeleka Taifa mbele zaidi pamoja na kutekeleza Dira ya maendeleo ya Taifa letu ya 2025-2050.
Rais Samia anapaswa kuendelea kuongoza Taifa letu kutokana na uchapakazi wake na kasi yake katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kuinua maisha ya watanzania. Nyote na sote ni mashahidi wa kazi kubwa iliyofanywa ndani ya muda mfupi wa uongozi wake ambayo hakuna mtanzania ambaye alifikiria kama tungeweza kufikia hatua hizo za kimaendeleo.
Hakuna aliyefikiria kama ndani ya muda mfupi wa uongozi wake ingewezekana kupandisha Bajeti ya kilimo kutoka Billioni mia mbili hamsini hadi Trilioni moja point tisa. Hakuna aliye fikiria kama tungeweza kutoa Elimu Bure hadi kidato cha sita, kujenga vyumba vya madarasa zaidi ya Elfu 20, kupandisha kima cha chini cha mshahara kufikia laki tano.
Kuongeza idadi ya watalii kufikia millioni mbili na point,kuongeza ukusanyaji wa mapato kufikia zaidi ya Trilioni 34 kwa Mwaka ,kutoa ajira kwa vijana maelfu kwa maelfu,kukamilisha Bwawa la mwalimu Nyerere ndani ya muda mfupi lenye uwezo wa kuzalisha megawati 2115,Kumaliza kabisa mgao wa umeme hapa Nchini.
Hakuna aliyefikiria kama ndani ya muda mfupi Tanzania inaweza jizolea heshima katika anga la kimataifa mpaka kupata fursa ya kuongoza Umoja wa Mabunge Duniani pamoja na Ukurugenzi Mkuu wa WHO kanda ya Afrika. Hakuna aliyefikiria kama ndani ya Muda mfupi tunaweza kufikia hatua ya Kumaliza kabisa njaa Nchini na upungufu wa chakula Nchini.
Yote hayo na mengine mengi sana yamewezekana kutokana na nguvu ,juhudi,maarifa ,akili ,maono ,ushupavu, umadhubuti,uimara na uhodari alionao Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan shujaa wa Afrika na jasiri muongoza njia. Imewezekana kwa sababu mbele yetu na kitini amekaa kiongozi mwenye uzalendo ,dhamira njema na upendo kwa watanzania.
Watu kama akina lissu pamoja na Lema hawakutarajia kabisa kama wangeweza kurejea na kuishi Nchini kwa amani na utulivu bila bughudha. Wameweza kurejea Nchini kwa sababu ya upendo na huruma aliyonayo Rais Samia kifuani pake. Leo demokrasia imeshamiri Nchini kwa sababu ya kuwa na mwana demokrasia uongozini.
Sasa kwanini tusibadilishe katiba ili Mama aendelee kuongoza Taifa letu hata baada ya kumaliza muda wake 2030? Rais Samia ndiye Joshua wetu ,ndiye aliyeinuliwa na Mungu kutupeleka nchi ya ahadi , Nchi itiririshayo asali na Maziwa, Nchi yenye kucheua fursa za kila aina. Kwanini tusibadilishe katiba ili kufanya Taifa letu liendelee na kasi hii hii ya maendeleo? Mnataka tukwame na kupunguza mwendo na kasi yetu ya maendeleo? Mnataka tuanze kusuasua na kupitwa na majirani zetu? Hamuoni kasi yetu ya maendeleo imekuwa kubwa sana mpaka kuwapa Homa ,hofu na kiwewe majirani zetu?
Napenda kusema kuwa ni lazima tubadilishe katiba yetu ili Mama aendelee kuongoza Taifa letu. Jua liwake au mvua inyeshe ni lazima katiba ibadilishwe tu. Maana katiba yetu siyo Msaafu au Biblia ambayo huwezi kubadilisha . Katiba imetungwa na sisi watanzania na tunayo nafasi ya kuibadilisha kwa maslahi mapana ya Taifa letu ili kumpa nafasi mbeba Maono Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan kuendelea kuongoza Taifa letu kwa miaka Mingi Zaidi kwa kadri Mungu atakavyoendelea kumjali afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia watanzania.
Kama china Taifa lenye watu zaidi ya Billion moja point nne walifanya hivyo kwa maslahi mapana ya Taifa lao. Kwanini na sisi tusifanye hivyo kwa ustawi wa Taifa na watanzania wote kwa ujumla wake. Mnafikiri wachina ni wajinga waliobadilisha katiba yao na kutoa fursa ya kiongozi wao kuendelea kuwaongoza?
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.