umeona hii nchi ni ya wazee peke yao tu sio??
Hewizet karibu ili uelimike, nchi yetu inawatu wenye mahitaji mbalimbali lakini anza na hii ili ujue makundi hayo yalivyoainishwa na mahitaji yake. Sura ya Tano Ibara ya 32 – 59 ndiyo mahususi inabainisha masuala yote yanayohusu Haki za Binadamu, Wajibu wa Raia, Jamii na Mamlaka ya Nchi. Usifungwe na hoja iliyopo kwenye mjadala. Kama una hoja uliza nipo kwa ajili yako ili uelimike na wengine juu ya umuhimu wa Katiba Inayopendekezwa kwa maendeleo ya nchi yetu na watu wake.
Kwa kifupi yapo mambo yanayohusu Uhuru, utu na usawa wa binadamu, Haki ya kuishi, Haki ya kutobaguliwa, Haki ya kutokuwa mtumwa, Uhuru wa mtu binafsi, Haki ya faragha na usalama wa mtu, Uhuru wa mtu kwenda anakotaka, Uhuru wa maoni, Uhuru wa habari na vyombo vya habari, Uhuru wa imani ya dini, Uhuru wa mtu kujumuika na kushirikiana na wengine, Uhuru wa kushiriki shughuli za utawala wa nchi, Haki ya kufanya kazi, Haki za wafanyakazi na waajiri.
Makundi mengine ni Haki za wakulima, wafugaji, wavuvi na wachimbaji madini, Haki ya kumiliki mali, Haki ya mtuhumiwa na mfungwa, Haki ya mtu aliye chini ya ulinzi au kizuizi, Uhuru na haki ya mazingira safi na salama, Haki ya afya na maji safi na salama, Haki ya elimu, Haki za mtoto, Haki na wajibu wa vijana, Haki za watu wenye ulemavu, Haki za makundi madogo katika jamii, Haki za wanawake, Haki za wazee na Uhuru wa taaluma, ubunifu, ugunduzi na usanii.
Karibu sana kwenye darasa la JF maana hili ni mahusi kwa wasomaji wake na hatimaye wawe walimu bora wa jamii.