Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Sahihi mkuu, hata nchi zenye katiba bora kama Brazil huwa inahitaji wanajeshi mara nyingine kuingilia kati kuhakikisha mambo yanaenda sawa.Huwa nashindwa kuwaelewa watu wanaofikiri kuhusu ''mwarobaini'' wa jambo fulani kwenye uongozi. Kwenye uongozi wowote duniani, huwezi kukuta jamii inayoishi bila matatizo mbalimbali kwenye uongozi. Matatizo ni sehemu ya uongozi kwa sababu sisi ni binadamu na kila mmoja wetu ana tabia zake. Ni kama ilivyo wizi au kuua, hata uwe sheria kali namna gani, haya mambo hayawezi kuondoka kabisa kwenye jamii. Tunachotilia mkazo ni njia bora na za haki za kukabiliana na matatizo ambayo tunajua lazima yatatokea. Huwezi kuandika katiba halafu ukarudi kukaa kwenye kochi eti umepata mwarobaini wa rushwa. Na huu msemo wa ''watu wanasema katiba ni mwarobaini wa matatizo yetu'' ni propaganda za CCM hizo. Wanaodai katiba hawasemi itakuwa ni mwarobaini wa matatizo yetu.
Nafikiri katiba mpya kwa Tanzania itasaidia zaidi kuweka muundo wa utawala wa nchi na madaraka sawa tu, mambo mengine yote itabidi kuendelea kupambania kwa nguvu zote kama kawaida tu.