Katiba Mpya: Kusambaratisha Taifa

Katiba Mpya: Kusambaratisha Taifa

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Baada ya tume ya Warioba kuileta rasimu ya Katiba mpya ijadiliwe, ni jambo lisilopingika kwamba Taifa linaelekea kugawanyika kutokana na hoja kubwa iliyozuka ya mfumo wa Muungano na serikali zake.

Ili nchi iweze kusonga mbele ktk nyanja zote ni budi iwe na TAASISI zilizo imara na si kuwa na viongozi imara. Taasisi zikiwa thabiti ni kwamba zitakuwa kwenye mstari mzuri wa kutumikia nchi kwani ni vigumu kupata viongozi imara wakati wote. Ili tuwe na viongozi thabiti ni budi wasimamiwe na taasisi zitakazoundwa na Katiba ili waweze kukidhi vigezo na matakwa ya nchi.

Nchi ikiwa na Mahakama imara, Bunge Imara, Jeshi Imara na Usimamizi imara wa uchumi tutaweza kuondoka kwenye mstari wa mataifa yanayoendelea na kujiunga na klabu za mataifa yanayojibeba kiuchumi.

Tatizo na unafiki wa wasomi wetu ni kujikomba kwa wanasiasa waliopo madarakani kwa minajili ya kujipatia ugali wa siku. Inawezekana hata Great Thinkers wengine wakawa wamenaswa na mfumo wa MAONI-SIASA ambao umefunika uwezekano wa Watanzania kupata Katiba mpya.

Mfumo wa Muungano umeteka nyara maoni ya Katiba mpya kiasi kwamba watu hawajadili tena maadili, usimamizi na mgawanyo wa rasilimali na hata muundo wa taasisi imara za nchi. Tumefika kwenye kupigana vikumbo kuhusu aina ya Muungano na idadi ya serikali. Tusidanganyike na hadaa za wanasiasa.
 
Zanzibar iwe mkoa na tuwe na serikali moja! Tofauti na hapo huo muungano na uvunjike!!
 
Siamini! Katiba mpya ni jambo lisiloepukika kwa wakati huu. Ni kweli ni jambo la kujadiliwa kwa makini na kwa undani kwani katiba ndio sheria mama wa sheria zote lakini ni vema pia kukabiliana na mabadiliko haya ya lazima bila woga. Mfumo ambao umekuwepo kwa miaka 50 iliyopita ni lazima ufumuliwe kwa Katiba mya na kusimikwa mfumo mbadala unaolandana na wakati tulio nao. Tukichelewa hili, mabadiliko yaweza kuja kwa njia zingine zisizo za za amani kama itokeavyo sasa katika mataifa ya kiarabu. Waoga wa mabadiliko wote wanakataa mambo mapya na wanaona heri kuendelea na yale ya kale. Tutoe maoni bila woga wa mabadiliko, huku tukijua kuwa mabadiliko ni lazima na hii ni nafasi ya pekee kuleta mabadiliko haya kwa njia za amani na demokrasia!!
 
Back
Top Bottom