KATIBA MPYA KWA MAENDELEO YA TANZANIA

KATIBA MPYA KWA MAENDELEO YA TANZANIA

Steven kiss

Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
5
Reaction score
2
KWANINI KATIBA MPYA NDANI YA TANZANIA NI MUHIMU?
Tanzania ni nchi ya demokrasia na inaongozwa kwa kufuata sheria na muongozo wa katiba iliyopo ya mwaka 1977 .kwa mda mrefu wananchi wa Tanzania wamekuwa kweny madai ya kupambania upatikanaji wa katiba mpya

KATIBA ZA TANZANIA HADI SASA

Tanzania ni jamhuri ya muungqno.Muungano wa nchi mbili zilizoungana mnamo tarehe 26 aprili 1964nchi hizi ni Tanzania na Zanzibar awali zilikuwa huru na zenye mamlaka kamili.katika jamhuri ya Tanzania zipo katiba mbili katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 Hivyo kwa upande wa Tanganyika nq jamhurii ya muungano wa Tanzania tumewahi kuwa na katiba zifuatatzo,katiba ya uhuru ya mwaka 1961,katiba ya jamhuri ya mwaka 1962,katiba ya Tanzania ya mwaka 1964(katiba ya muungano),katiba ya muda ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1965,na katiba ya kudumu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977
Kwa kifupi uandishi na maudhui ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake 14 vimekuwa vikilalamikiwa kwa kutoshirikisha wananchi.Wanachi hawakupa nafasi ya kutoa maoni yao wakati wa uandishi wa katiba hizo.Na pia katiba zoote ziliandikwa wakati nchi ikiwa chini ya chama kimoja .Baada ya mwaka 1992 nchi ilitoka kweny mfumo wa chama kimoja na kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi kwa maana hiyo katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 haitosherezi.

HISTORIA YA MCHAKATO WA KATIBA MPYA

Katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ilionekana inamapungufu mengi saana ikapelekea uhitaji wa katiba mpya ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.Mwaka 2010 Zanibar ilipofanya marekebisho kwenye katiba yake ya mwaka 1984 ilipelekea kuhitajika kwa katiba mpya kuongezeka madai yake pia hali ya kisiasa ya mwaka 2010 n nayo ilionesha uhitaji mkubwa wa katiba mpya ili kukabiliana na changamoto zilizojitokeza wakati na baada ya uchaguzi.Dkt Jakaya Mrisho Kikwete raisi wa awamu ya nne wa jamhuriya muungano wa Tanzania kwenye hotuba yake ya kuuaga mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka 2011 aliidhinisha kuanza kwa mchakato wa kutafta katiba mpya.Sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 ilimpa rais mamlaka ya kuteua Tume ya mabadiliko ya katiba .Raisi aliteuwa Tume ya mabadiliko ya katiba ikiongozwa na Mwanasheria nguli Jaji na waziri mstaafu Mhe.Joseph Sinde Warioba ili kupata katiba ya kudumu miaka 50 hadi 100 bila kuhitaji marekebisho makubwa.

Makamu mwenyekiti alikuwa mhe,jaji Augustino Ramadhan jaji mkuu mstaafu.mchakato ulihusisha wajumbe kutoka Tanzania bara na wengine kutoka Zanzibar,wawakilishi wa vyama yya siasa ,Wasomi, asasi za kiraia, madhehevu ya dini na makundi mengine katika jamii.Tume ilipewa mda miezi 18 mpaka 20 ilikukusanya maoni na kuandaa rasimu ya katiba mpya na kupelekwa kwenye bunge maalumu la katiba


KWANINI KUNAUHITAJI WA KATIBA MPYA TANZANIA


Tanzania inahitajika katiba mpya ambayo itakuja kuwa mbadala wa katiba hii ya sasa zifuatazo ni sababu za kwanini kuna ulazima wa kupata katiba mpya?

i/KUMALIZA UTAWALA WA CHAMA KIMOJA KWA MDA MREFU

Toka Tanzania ipate uhuru mwaka 1961 ni chama kimoja tu kilicho itawala Tanzania ambacho ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini urasimishaji wa katiba mpya utapelekea kuwepo kwa uongozi wa kupokezana baina ya vyama mbalimbali vya siasa

Ii/ KUPUNGUZA MRUNDIKANO WA MADARAKA KWA RAISI

Ukisoma katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 sura ya tatu ibara ya 36 ibara ndogo ya kwanz raisi amepewa mamlaka makubwa ya kuteuwa pamoja na kupanfa uongozi hii inaleta utendaji mdogo katika serikali mfano uteuzi wa kindugu kwa watu wa karibu na raisi

Iii/KUPITWA KWA MDA KATIBA YA ZAMANI

Katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ni katiba iliyopitwa na wakati katika mambo mengi kwa mfano wakati katiba hiyo inaundwa haikushirikisha wananchi pia nchi ilikuwa katika mfumo wa chama kimoja lakini saivi mfumo umebadilika saiv nchi inaongoza na vyama vingii.

Iv/UHURU KATIKA MIHIMILI YA DOLA

Katiba ya saivi ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 haitoi uhuru kwa mihimili ya serikali kufanya kazi kwa mfano serikali inqiingilia mahakama pale raisi anapoteua majaji pia pale rais anapoteua wabunge kuwa mawaziri pia ni sababu moja wapo ya serikali kuingilia mihimili mingine.

v/KULINDA HAKI ZA BINADAMU
katiba iliyopo haitoi uthibitieho kulinda haki ya binadamu kwa mfano hukumu ya kifo pia swala la uvunjifu wa haki za binadamu limekuwa likishuhudiwa kwa wingi nchini kuwepo k a katiba mpya kutapelekea kuwepo kwa uheshimu wa haki za binadamu

vi/ITAKUWA KATIBA YA WANANCHI

Katiba mpya itakuwa imetokana na maoni ya wananchi kwa mfano rsimu ya Katiba mpya ya mzee warioba ni mfano wa katiba ambayo itaweka wazi masuala mbalimbali kwa sababu imetokana na wananchi wenyewe.

Vii/KUANZISHWA KWA TUME YA UCHAGUZI HURU NA INAYOJITEGEMEA

Katiba iliyopo sasa inafanya tume ya uchaguzi kuwa na mahusiano makubwa na serikali inayokuwa madarakani kwa sasa mkurugenzi wa tume ya uchaguzi kitaifa au wakurugenzi wa tume ya uchaguzi mkoani woote wanachaguliwa na raisi hii inafanya tume kulalia upande mmja wakati wote.


Viii/KUPUNGUZA MALIMBIKIZO YA MALIPO KWA VIONGOZI WALIOPO MADARAKANI NA WASTAAFU.


Ukisoma katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 sura ya tatu ibara ya 43 ibara ndogo ya (i) na ya (ii) inaeleza malipo anayopokea raisi akiwa madarakani na anapostaafu ni makubwa mnooo ambayo yakizuiwa yanaweza kuelekezwa sehemu nyingne na yakaleta maendeleo

Ix/SUALA LA MUUNGANO NA MUUNDO WAKE


Katiba iliyopo imeshindwa kutatua kitendawili cha suala la muungano kwa mfano muundo wa serikali uliopo haukizi mahitaji ya muungano kwenye rasimu ya katiba ya mzee warioba alitoa mapendezeko kuwe na serikali tatu yaani kuwe na serikali ya Tanzania bara, Zanzibar na serikali ya muungano lakin mimi natamani kuwe na serikali moja yaani kusiwe na Zanzibar wala Tanzania bara bali kuwe na jamhuri ya muungano wa Tanzania tu kumaanisha kuwe na serikali moja tu.


x/MABADILIKO YA KIJAMII NA KIUCHUMI

Ndani ya katiba hii tunayotumia sas inaiongelea Tanzania kama nnchi y ujamaa lkn mambo yamebadilika saivi Tanzania inamifumo yote ya kibepali na kijamaa kwa mbali.


Xi/HAKI NA USSAWA WA KIJINSIA
Tanzania kwenye swala la haki na usawa ipo nyumaa saana kumaanisha ile inshu ya 50 kwa 59 kwa Tanzania imekuwa haipewi kipaumbele kama nchi za wenzetu kama south Africam

VITU VINAVYOPELEKEA KUKWAMISHA UUNDAJIBWA KATIBA MPYA

i/USHIRIKI MDOGO WA SERIKALI
wote tumeshuhudai hasahasa serikali ya awamu ya tano haikuwa tyr kuendeleza swala la uandaaji wa katiba mpya kupelekea ksimama kwa zoezi la katiba mpya
ii/UBINAFSI WA VIONGOZI
katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inawajari saana viongozi kuliko wananchi ndo maana viongozi hawapo tayri kwa kuleta mabadiliko kwa mfano katiba iliopo haimpi kikomo mbunge cha kukaa madarakani lakini rasimu ya katiba mpya ya mzee warioba ilitaka mbunge kukaaa madarakani kwa mda wa miaka kumi tu.


Iii/UMASIKINI WA TAIFA
Kitaifa nchi yetu ni nchi ya uchumi wa kawaida saana kiasi kwamba kuna mambo mengine ni mapka tupate mkopo kutoka nje na suala la katiba linahitaji mtaji mkubwa kutekelezekaa

VITU GANI VIFANYIKE ILI KUFANIKISHA KATIBA MPYA
i/UTOLEWAJI WA ELIMU KWA JAMII KUHUSU UMUHIMU WA KATIBA MPYA
ii/UTAYARI WA SERIKALI
iii/UTAYARI WA JAMII
iv/USHIRIKI MKUBWA WA BUNGE KUDAI KATIBA MPYA
v/UANDAAJI WA BAJETI KWA AJILI YA SUALA LA KATIBA MPYA
 
Back
Top Bottom