Corona imeleta matatizo makubwa ya uchumi wa dunia na sisi hatuwezi kukwepa huo mdororo. Katiba inaweza kusubiri mpaka 2025.
Wengi wanaoongelea katiba kwa sasa ni wanasiasa na wapambe wao, mwananchi wa kawaida kabisa kule Chunya anataka afikishiwe maji na umeme.
Mwananchi wa kawaida kule Ngara Rulenge anataka afaidike na Kabanga Nickel kuliko kufuatilia mijadala ya vifungu vya katiba kwa muda huu.
Mwananchi wa kawaida kabisa kule Ruangwa Lindi anataka aanze kufaidika na uwepo wa graphite iliyo chini ya ardhi anayoikanyaga kila siku.
Katiba inapigiwa kelele humu jukwaani walipo wanasiasa na mashabiki wao.