Katiba Mpya na Uchaguzi Mkuu 2015

Katiba Mpya na Uchaguzi Mkuu 2015

Getstart

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
6,658
Reaction score
2,235
Katika Salaam za kukaribishamwaka mpya wa 2013, Rais wetu Mh. Jakaya Mrisho Kikwete alitoa taarifa yamaendeleo ya uundwaji wa Katiba Mpya. Katika maelezo yake alionyesha kuwaifikapo Novemba 2013 Bunge la Katiba litakaa kupitisha mapendekezo yatakayo kuwa yametolewa na Tume ya Katiba.

Rais pia alionyesha matumainikuwa April 2014, tutakuwa tayari na Katiba mpya ambayo itatumika katika uchaguzimkuu wa 2015. Mwenyekiti wa Tume ya Katiba pia alithibitisha maelezo haya na kwa muda fulani alisikika akisema kuwa Uchaguzi Mkuu ujao usipofanyika chini ya Katiba mpya tutakuwa na matatizo makubwa.

Swali la kujiuliza, je hata kama kweli April 2014 tutakuwa na Katiba mpya kutakuwa na muda wa kutosha kuandaa mifumo, taasisi n.k za kutekeleza/kusimamia uchanguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2015.

Kwa ratiba yake ya kawaida, Bungela Muungano litatakiwa kuvunjwa mwezi Agusti 2015 ili kuruhusu mchakato wa uchaguzi mkuu kufanyika. Hii inatoa muda wa takriban miezi 15 na vikao kama vinne hivi vya Bunge kuandaa na kupitisha miundo, sheria na taasisi za kutekeleza Katiba mpya.

Mapendekezo tunayoshuhudia ya Katiba mpya yanagusa mambo mengi ambayo kwa kila hali kutakuwa na mabadiliko ya muundo na mfumo wa utawala. Kwa mfano mapendekezo yanagusa muundo wa muungano. Ikiwa kutakuwana Serikali tatu, hii ina maana lazima tuwe na mchakato mwingine wa Katiba yaTanganyika. Ni vigumu kuona hili likifanyika katika muda utakaokuwa umebaki!

Hata kama tukibakiza mfumo waSerkali mbili – kitu ambacho sioni kama itakidhi mapendekezo ya pande zote zamuungano – bado kutakuwa na mabadiliko kwani wapendekezaji wa mfumo huu wanaweka masharti ambayo yatahitaji mchakato mwingine kutekelezwa. Tukichukua mfumo wa Serkali moja halikadhalika itahitaji mchakato.

Tukiacha ya muungano,mapendekezo mengine yanaonekana kujikita zaidi katika muundo wa utawala na taasisi zake. Kuna mapendekezo ya majimbo. Hili likikubaliwa litahitaji mchakato mwingine kuhainisha mipaka, kuweka sheria zitakaongoza mfumo huu n.k. Ni kwa vipi haya yatafanyika katika kipindi kitakachokuwa kimesalia kuweza kufanya uchaguzi mkuu ulio huru na haki, ni kitu cha kujiuliza.

Kwa vyovyote vile hata tusipochukua mfumo huu wa majimbo, ni lazima kutakuwa na mabadiliko ya muundo wautawala ambao utahitaji taasisi na mfumo mpya kusimikwa kabla ya uchaguzi. Vinginevyo tutakuwa hatujatengeneza Katiba mpya!

Suala lingine la muhimu naambalo linahusiana na uchaguzi ulio huru na haki, ni taasisi itakayosimamiauchaguzi. Itashangaza ikiwa Katiba mpya haitaleta mabadiliko makubwa katikaTume ya Uchaguzi ili siyo tu ionekane huru bali pia itende haki katikau simamizi wa chaguzi.

Kikubwa hapa ni kuwa Tume ya Uchaguzi mpya ni lazima iwe na muda wa kuthibitisha uwezo na u-huru wake katika majukumu itakayopewa ili kuwajengea watu imani hiyo. Ni vigumu kuona wataweza kufanya hili katika kipindi hicho kifupi kitakachokuwa kimebaki na ikiwa kutakuwa na chaguzi ndogo za kutosha kuwapa watu nafasi za kuitathimini.

Je kwa hayo na mengine yanayo husiana na mabadiliko yatakayo ambatana na Katiba Mpya, ni rahisi kujiaminisha kuwa uchaguzi mkuu wa 2015 utafanyika chini ya Katiba hiyo mpya? Auni vyema kuanza kujiandaa vinginevyo na kuacha mchakato wa Katiba Mpya uendelee bila kuhuwaisha ili tupate kilicho bora.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Kusema ukweli na bila kutafuna maneno ni kwamba kama tunataka katiba nzuri na ya kudumu itakayoisaidia nchi hii kwa miaka mingi, muda uliobaki utakuwa hautoshi. Kutokana na hali hiyo mimi ningependekeza mambo machache kama ifuatavyo:

1. Kwamba, kwa ajili ya kuepuka vurugu na malalamiko kutoka kwa watu wengi, uchaguzi ujao ufanyiwe marekebisho ambayo yatawezesha kufanyika kwa uchaguzi huru.

2. Kwa hiyo, tume ya uchaguzi ambayo ndiyo imekuwa ikilalamikiwa zaidi ifanyiwe marekebisho makubwa. Yaani ni kwamba, iundwe tume huru kabisa na ambayo muundo wake utatokana na asasi mbalimbali za kiraia, taasisi mbalimbali za kidini na NGOS. Tume hii iwe completely free na isiingiliwe kabisa na mfumo wowote wa serikali
 
Ahsante mtoa mada(Getstart) hapojuu. Hapa nionavyo mm ni kwamba kwa kujua au kutojua mazingira yanatengenezeka ya serikali iliyopo kutofikia kikomo 2015 au kuharibika kwa vyote viwili; katiba mpya na uchaguzi mkuu

Hivo basi tufanye mawili yafuatayo
1. Tuandae mazingira ya kufanya uchaguzi huru na wa haki katika spirit safi kabisa ya kuwa na serikali halali (legitimate government) kwa kuandaa mazingira ie kuundwa Tume Huru ya uchaguzi...tukiwa bado chini ya katiba hii tunayoenda nayo. Hili linawezekana maana political and social atmosphere iliyoko ss ni ya kufanya mageuzi katika jinsi ya tunavofanya mambo yetu kama taifa. Uchaguzi ufanyike chini ya katiba hii, tumalize uchaguzi tuanze kuandaa mazingira ya kuimplement katiba mpya.
Tujipe muda, tufanye jambo moja at a time maana demokrasia yetu bado changa na ss hv iko volatile. Tukiyachanganya haya mawili ya uchaguzi na katiba mpya tutayaaribu yote. Ni muhimu yote mawili yafanikiwe kwa kiasi kikubwa sana. Kuyachanganya kunaweza kwa haraka tu ku-politisize mchakato wa katiba na hivo kuuharibu kabisa. Consequencies za hali hiyo sina haja ya kuzieleza; ziko wazi vizazi kwa vizazi vijavyo.

2. Ni kujitayarisha kuona serikali iliyopo inaendelea kutawala zaidi ya kikomo chake (2015) ili tupate katiba mpya, tuandae mazingiya ya kimifumo halafu ndo tufanye uchaguzi.

Hili la pili silipendi lakini madhara yake si makubwa kama kuyachanganya mawili kwa muda mmoja isipokuwa tu litaweka precidency mbaya.
 
Ahsante mtoa mada(Getstart) hapojuu. Hapa nionavyo mm ni kwamba kwa kujua au kutojua mazingira yanatengenezeka ya serikali iliyopo kutofikia kikomo 2015 au kuharibika kwa vyote viwili; katiba mpya na uchaguzi mkuuHivo basi tufanye mawili yafuatayo1. Tuandae mazingira ya kufanya uchaguzi huru na wa haki katika spirit safi kabisa ya kuwa na serikali halali (legitimate government) kwa kuandaa mazingira ie kuundwa Tume Huru ya uchaguzi...tukiwa bado chini ya katiba hii tunayoenda nayo. Hili linawezekana maana political and social atmosphere iliyoko ss ni ya kufanya mageuzi katika jinsi ya tunavofanya mambo yetu kama taifa. Uchaguzi ufanyike chini ya katiba hii, tumalize uchaguzi tuanze kuandaa mazingira ya kuimplement katiba mpya.Tujipe muda, tufanye jambo moja at a time maana demokrasia yetu bado changa na ss hv iko volatile. Tukiyachanganya haya mawili ya uchaguzi na katiba mpya tutayaaribu yote. Ni muhimu yote mawili yafanikiwe kwa kiasi kikubwa sana. Kuyachanganya kunaweza kwa haraka tu ku-politisize mchakato wa katiba na hivo kuuharibu kabisa. Consequencies za hali hiyo sina haja ya kuzieleza; ziko wazi vizazi kwa vizazi vijavyo.2. Ni kujitayarisha kuona serikali iliyopo inaendelea kutawala zaidi ya kikomo chake (2015) ili tupate katiba mpya, tuandae mazingiya ya kimifumo halafu ndo tufanye uchaguzi.Hili la pili silipendi lakini madhara yake si makubwa kama kuyachanganya mawili kwa muda mmoja isipokuwa tu litaweka precidency mbaya.
Ikiwa tunakubaliana kuwa muda wa maandalizi hautoshi kwa Katiba mpya kutumika uchaguzi wa 2015 basi la muhimu ni kuweka mazingira ya kufanyika uchaguzi huru kwa katiba tuliyonayo. Tatizo Tume huru itaundwaje katika mzingira haya? Sidhani kama uteuzi wa wajumbe tu kutoka taasisi malimbali utaifanya tume hiyo kuwa huru. Hilo la pili (kuongeza muda) tumeshaanza kusikia tetesi, lakini sidhani kama litapitishwa, upepo unavyovuma ndani ya Chama na nje wanaonekana kusubiri 2015 kwa hamu kubwa, ikiwemo na ya uchu mkubwa.
 
Kusema ukweli na bila kutafuna maneno ni kwamba kama tunataka katiba nzuri na ya kudumu itakayoisaidia nchi hii kwa miaka mingi, muda uliobaki utakuwa hautoshi. Kutokana na hali hiyo mimi ningependekeza mambo machache kama ifuatavyo:1. Kwamba, kwa ajili ya kuepuka vurugu na malalamiko kutoka kwa watu wengi, uchaguzi ujao ufanyiwe marekebisho ambayo yatawezesha kufanyika kwa uchaguzi huru.2. Kwa hiyo, tume ya uchaguzi ambayo ndiyo imekuwa ikilalamikiwa zaidi ifanyiwe marekebisho makubwa. Yaani ni kwamba, iundwe tume huru kabisa na ambayo muundo wake utatokana na asasi mbalimbali za kiraia, taasisi mbalimbali za kidini na NGOS. Tume hii iwe completely free na isiingiliwe kabisa na mfumo wowote wa serikali
Mchmlay unafikirti tume huru inawezekana kwa kuhusisha asasi mbalimbali bila kubadili katiba?
 
tatizo siyo tume huru ya uchaguzi tatizo ni kipengele kinacho zuia kuhoji matokeo ya uraisi mahakamani
 
Back
Top Bottom