Katiba mpya na utawala usiofuata katiba

Katiba mpya na utawala usiofuata katiba

makinikia 101

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
491
Reaction score
876
Kumekua na maoni mengi sana kuhusu suala la katiba mpya Tanzania. Suala hili lilipigiwa sana kelele na wananchi pamoja na wanasiasa hadi pale JK alipoanzisha mchakato huo ambao pia uliishia njiani, oopss.
Nionavyo mimi, Tanzania hatuna tatizo la katiba mpya, tunalo hitaji la msingi la kupata viongozi wanaoheshimu na kufuata viapo vyao vya kuilinda katiba. Kama hii tu iliyopo haifuatwi na viongozi wetu (km kufungia mikutano ya kisiasa, mahakama bunge na serikali kuwa mihimili tofauti, nk), hata ikija mpya kiasi gani na tukakosa viongozi wenye kuiheshimu, bado tatizo litakua palepale
 
Bila katiba mpya kwa mtu mweusi sio rahisi kuheshimu sheria za nchi
 
Kuandika katiba ni jambo moja na kuitumia ni jambo jingine.
Tatizo siyo katiba, watu hawaelewi matumizi ya katiba na umuhimu wake.
 
Katiba hii hii ni nzuri tu sema watu badala ya kuisoma wanafungia vitumbua.
 
Bila katiba mpya kwa mtu mweusi sio rahisi kuheshimu sheria za nchi
Hata tukipewa hiyo katiba ya kenya ambayo tunaamini iko super kuliko yakwetu, bado kwa nature ya mfumo na viongozi tulionao Tanzania iyo katiba itakanyagwa tu. Take my words
 
Lkn si umeona jinsi katiba imefanya kazi nzuri, kama isingekuwa katiba nzuri na kiongoz mwenye kufuata katiba leo kenyatta angekuwa ameshaapishwa, umeelewa sasa mkuu!!!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Uzuri wa ile katiba inaruhusu kuhoji matokeo mahakamni hata kama tume ishamtangaza mshindi
 
Lkn si umeona jinsi katiba imefanya kazi nzuri, kama isingekuwa katiba nzuri na kiongoz mwenye kufuata katiba leo kenyatta angekuwa ameshaapishwa, umeelewa sasa mkuu!!!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ingekua suluhisho kenyatta asingeiba.Hata sie katiba yetu pendekezwa ina kipengele cha kwenda mahakamani lakini chadema hawaitaki,hakuna jinsi tuendelee tu na hii ya sasa
 
Uchaguzi wa 2020 tunataka katiba ya Warioba....! Ama sivyo hatutaki uchaguzi!!! Atawale milele kwa katiba mfu..........ya sasa hatutakiii
 
Back
Top Bottom