kimsingi utawala wa nchi ni mihili mitatu, lakini kwa mujibu wa katiba ya sasa na katiba inayopendekezwa kwa kuangalia mazingira ya tanzania tuna mihimili mitatu kinadharia lakini kivitendo tuna mhimili mmoja tu.
sababu za kuwa na mhimili mmoja kuu ni mbili
1. huwezi kuwa na bunge ambalo ni sehemu ya serikali na ukawa na mahakama inayoteuliwa na serikali ukawa na mihimili mitatu inayoweza kusimamiana katika utendaji.
2. ni kosa kubwa kuwa na mihimili mitatu alafu ukachukua nguvu za jamii zote zikawekwa katika mhimili mmoja. mfano serikali ndio mhimili unaomiliki majeshi na fedha na hizi ni nguvu ambazo zinaifanya serikali kujenga kiburi kwa mihimiri mingine kwa maana hata wafanye maamuzi hawa wengine je serikali isipotekeleza watafanya nini? sababu hii inawafanya mahakama na bunge kuchukua ushauri wa adui usiyeweza kumsinda ungana naye hivyo badala ya kufanya kazi waliyotumwa na wananchi kusimamia utendaji wa serikali ni kuungana na serikali kuwa kitu kimoja.
kosa kubwa jingine tulilolifanya ni kutengeneza kijiwe cha kahawa eti kusimamia serikali.
mfumo wa bunge tulioutengeneza ni kijiwe cha kahawa hakina utaalamu wala mfumo wa kusimamia na kushauri serikali. tunatumia fedha nyingi kuendesha chombo kisichokuwa na tija kutokana na chombo kutokutumia utaalamu wala utaratibu kufanya kazi.
kwa nini baraza la madiwani na bunge kisiwe chombo kimoja lakini watu hawa wanafanya kazi kwa takwimu. diwani kazi yake ni kufuatilia utendaji wa serikali katika kata. kama ni utendaji katika shule, vituo vya afya, ujenzi wa miradi ya maendeleo na katika halmashauri wanakutana katika ofisi ya mbunge kujumuisha takwimu na kuzichambua. ofisi ya mbunge ina wataalamu wa kufuatilia utendaji wa halmashauri na yeye wakati wote yuko jimboni ndiye mtendaji mkuu. ripoti za madiwani katika jimbo pamoja na taarifa za utendaji wa halmaushauri zinajadiliwa na madiwani na kutengeneza ripoti ya mbunge kupeleka bungeni ikiwa ndio utendaji wa serikali.
mwananchi yeyote akiombwa rushwa, kudharauriwa, kunyanyaswa katika ofisi yoyote ya umma anakimbilia ofisi ya mbunge kutoa taarifa.
lakini eti mtu yuko kwenye biashara zake akitoka huko anaenda kujadili utendaji wa serikali kwa hisia tu hivi kweli hiki si kijiwe cha kahawa? tunapolaumu utendaji wa serikali je bunge si ndio linatakiwa kubeba lawama likiwa la kwanza maana msimamiaji yuko wapi?
kuwachukua wanasiasa eti wanapita katika mashirika kukagua hesabu sijui kufanya nini nadhani tunafanya mchezo, kwanini chombo hiki kisiajiri wataalamu waliobobea kufanya kazi hiyo na hawa wawakilishi wa wananchi wanajadili mapendekezo yao.
nadhani bunge letu ni kituko namba moja lakini haya tunaweza kuyarekebisha kupitia katiba.
sasa kiukweli sijui tunafanya nini lakini matokeo ya kutokuwa na mifumo ni kila anayekabidhiwa kitengo akiona kina maslahi ni kujinufaisha mwenyewe maana hakuna mifumo ya kijamii kusimamia.
binafsi nimejiuliza kama katiba hii tumeitunga kwa kuangalia matatizo yetu na kutafuta jinsi ya kuyatatua au tumekusanya materials na kuweka pamoja bila kureflect matatizo yetu kwa maana matatizo mengi tunayolalamikia ya mfumo yanatokana na udhaifu katika mihimili mitatu ya juu au kukosa mihimili mitatu na kuwa na mhimili mmoja.